Kifo cha Shireen Abu Aqla: ‘Hakujua ilikuwa siku yake ya kuzaliwa ya mwisho’

Mwandishi wa Al Jazeera Shireen Abu Aqla aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa uvamizi wa kijeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Ilikuwa Mei 11, 2022.

Mwandishi huyo wa habari mwenye umri wa miaka 51 mwenye asili ya Palestina na Marekani wa Al Jazeera alikuwa mmoja wa wanahabari wenye uzoefu na kupendwa zaidi katika eneo hilo.

Al Jazeera imefungua kesi dhidi ya wanajeshi wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu mauaji yake. Mwaka mmoja baada ya kifo chake, mpiga picha wa Shireen, Majdi Bannoura, anaelezea nyakati za mwisho alizomrekodi na jinsi kifo chake kimekuwa na athari ya kudumu kwake.