Kwanini mtoto huyu wa Gaza aliyefanyiwa upasuaji wa moyo anarejeshwa katika eneo la vita?

- Author, Adnan El-Bursh
- Nafasi, BBC News Arabic
- Akiripoti kutoka, Doha
- Author, Lina Shaikhouni
- Nafasi, BBC World Service
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Katika hema ambayo ni makaazi ya muda ya watu katika kambi ya wakimbizi wa Al-Shati, Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Enas Abu Daqqa,33, anaonekana akiwa amempakata mtoto wake mchanga. Kuna mtu anasikika akiimba mara kwa mara nyuma yake angalau kuto kiburudisho licha ya joto kali la asubuhi.
Enas anahofia afya ya Niveen huenda ikazorota wakati wowote. Ana umri wa miezi saba tu, na alizaliwa wakati wa vita aikiwa na tundu kwenye moyo wake.
Mtoti Niveen analiakwa maumivu mama yake anapoelezea hali ngumu anayopitia kujaribu kuokoa maisha yake baada ya miundo mbinu ya afya ya Gaza kusambaratika
"Vita imemuathiri san," Enas aliiambia BBC. "Uzani wake hauongezeki nahofia anaweza kuwa mgonjwa."
Niveen anaweza kupata nafuu akipokea huduma ya dharura ya afya nje ya Gaza. Mnamo mwezi Machi, Jordan ilifanikisha hilo.
Wakati mapigano yalipositishwa kati ya Hamas na Israel, watoto 29 wa Gaza, akiwemo Niveen, walipelekwa Jordan kupokea matibabu katika hospitali za nchi hiyo. Mama yake na dada zake walisafiri pamoja nao.
Walikuwa watoto wa kwanza kupelekwa Jordan baada ya Mfalme Abdullah kutangaza mpango wa kutoa huduma za matibabu kwa watoto 2000 wa Gaza wakati wa ziara yake nchini Marekani mwezi ullioyotangulia. Mpango huo uliratibiwa na mamlaka ya Israel ambao ilikagua wazazi wanaosafiri na watoto wao.
Madaktari wa Jordan walimfanyia Niveen upasuaji wa moyo, na alikuwa ameanza kupata nafuu.
Lakini takribani wiki mbili baada ya watoto hao kupokea matibabu Jordan, makubaliano ya kusitishaji mapigano huko Gaza yaliporomoka wakati Israel ilipoanza tena mashambulizi yake dhidi ya Hamas.
Kwa wiki kadhaa, Enas alifuatilia habari kutoka katika chumba cha hospitali cha bintiye huko Jordan, akiwa na wasiwasi juu ya usalama wa mume wake na watoto wengine ambao walisalia Gaza.
Akiwa bado anahofia usalama wa familia yake Gaza tarehe 12 Mei, mamlaka ya Jordan ilimwambia Enas ajiandaye kurejea nyumbani siku iliyofuata, kwani walisema Niveen alikuwa amemaliza matibabu yake.
Enas alishtuka.
"Tuliondoka huku wakati mapigano yalikuwa yamesitishwa. Wanawezaje kuturudisha baada ya vita kuanza upya?" Anasema, hatua hiyo ilimtatiza sana.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Enas amabaye sasa ameungana na mume wake na watoto wao mjini Gaza, anasema Niveen hakukamilisha matibabu yake kabla warejeshwe nyumbani na anawasi wasi hali yake inaweza kuwa mbaya.
"Binti yangu mchanga yuko katika hali mbaya ambayo inatishia maisha," anasema Enas. "Ana maradhi ya moyo. Wakati mwingine anashindwa kupumua hadi ngozi ayke inageuka rangi na kuwa ya buluu. Anaishi kwenye hema akiwa na hali hii."
Tarehe 13 Mei, Jordan ilitangaza kuwa imewarudisha watoto 17 Gaza "baada ya kumaliza matibabu yao". Na siku baadaye, kundi lingine la watoto wanne wagonjwa lilisafirishwa kutoka Gaza hadi Jordan.
Mamlaka ya Jordan imeambia BBC kwamba watoto wote waliorudishwa walikuwa katika hali nzuri kiafya, na kupinga madai kwamba hawakumaliza matibabu yao.
Wakuu walibaini kuwa ufalme huo ulikuwa wazi tangu mwanzo kuhusu nia yake ya kuwarudisha watoto mara afya zao zitakapoimarika, na kuongeza kuwa hii ilikuwa muhimu "kwa smaslahi ya kisiasa".
"Sera ya Jordan ni kuwatunza Wapalestina katika ardhi yao, na sio kuchangia kuwaondoa katika ardhi yao," taarifa ya wizara ya mambo ya nje iliyowasilishwa kwa BBC ilisema. Kuwarejesha nyumbani watoto hao 17 pia kutatoa nafasi kwa watoto wengine Gaza, iliongeza.
Lakini afisa katika wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza aliambia BBC kuwa watoto hao bado wanahitaji matunzo, na kwamba kurejea kwao vitani kulihatarisha maisha yao.
'Kurejeshwa nyumbani kwa lazima'
Hili ndilo jambo linalomkosesha usingizi Nihaya Bassel mwenye umri wa miaka 30.
Mwanawe, Mohammed, ambaye ana umri wa mwaka mmoja na miezi kadhaa, anaugua pumu na mizio mikubwa ya chakula. Anaamini mwanawe hakupata matibabu aliyostahili.
"Tumerudi kuishi kwa hofu na njaa, tukiwa tumezungukwa na kifo," Nihaya anasema huku akibubujikwa na machozi. "Huyu mtoto nitampatiaje maziwa anayohitaji kunywa, hawezi kula licha kuwa ana umri wa zaidi ya mwaka mmoja, akila chochote ataugua moja kwa moja."
Israel ilizingira na kudhibiti Ukanda wa Gaza wiki 11 zilizopita, na kuzuia kuingia kwa msaada wowote wa kiutu ikiwemo chakula, dawa, malazi na mafuta. Ilisema kuwa mashambulizi yaliyoanza upya yalilenga kuishinikiza Hamas kuwaachilia mateka ambao bado wanaozuliwa huko Gaza.
Mashirika ya kimataifa yanaonya kwamba Wapalestina wanaoishi katika eneo hilo wanakabiliwa na "tishio kubwa la njaa". Siku ya Jumatatu, Israel ilitangaza kuwa itaruhusu kiasi "kidogo" cha chakula kuingia Gaza kufuatia shinikizo la Marekani. Umoja wa Mataifa uliunga mkono hatua ya kuruhusu lori tano zilizobeba msaada ikiwa ni pamoja na chakula cha watoto, lakini inasema ni kama "tone katika bahari".

Sasa Nihaya anaishi katika eneo dogo, lenye mahema katika kambi ya al-Shati pamoja na familia ya shemeji yake. Mumewe na watoto wengine watatu walikuwa wamekimbilia huko kutoka mahali pengine kaskazini mwa Gaza, wakiepuka mashambulizi makubwa ya Israel wakati vita vilipoanza tena alipokuwa Jordan.
"Nimewaacha watoto wangu hapa. Nilimuacha mume wangu hapa. Walipitia madhila makubwa nyuma wakiti nilipokuwa nje ya nchi," Nihaya anasema huku akibubujikwa na machozi.
"Nilikuwa nikifikiria hali yao mara kwa mara huko Gaza nilipokuwa Jordan. Nilipitia yote hayo ili mtoto wangu aweze kutibiwa. Kwa nini nilazimishwe kurudi kabla ya kumaliza matibabu yake?"
Anajitahidi kudhibiti hasira yake anaposimulia safari yake ya kurudi Gaza.
"Hatukuondoka [mpaka] 04:00, na hatukufika Gaza hadi 22:45," anasema. Walipofika kwenye kivuko cha mpaka, Nihaya anasema walinyanyaswa na vikosi vya usalama vya Israel.
"Walianza kututukana, kututishia, kutupiga na kachukua pesa zetu zote, simu zetu, mabegi yetu na kila kitu," anasema N.ihaya
Enas pia alisema alikabiliwa na hali hiyo hiyo, akibainisha kuwa vifaa vyake vya matibabu vilichukuliwa pia.
Jeshi la Israel liliiambia BBC kwamba walinyakua "fedha ambazo hazijatangazwa zilizovuka mipaka ya kawaida" kutoka kwa watu wa Gaza waliokuwa wakirejea kutoka Jordan kutokana na tuhuma kwamba "wangetumika kwa ugaidi ndani ya Gaza". IDF inasema kuwa pesa hizo zinashikiliwa ili kubaini zilikotoka.
Haikueleza kwa nini mali nyingine za kibinafsi zilichukuliwa.
Nihaya anasema amerejea kutoka Jordan "mikono mitupu"; hata rekodi za matibabu za mtoto wake zilikuwa kwenye mifuko ambayo ilichukuliwa na vikosi vya usalama vya Israel.
Jordan inasema imewapa watoto kama Niveen na Mohammed huduma bora zaidi ya afya kadiri ya uwezo wake, na familia zote mbili zinakubali hili.
Lakini wana wasiwasi kwamba maisha katika mojawapo ya maeneo hatari zaidi ya vita kwa watoto yatarudisha nyuma hatua zilizopigwa kuwapa tiba watoto wao katika muda wa miezi miwili iliyopita.
"Nilimfikisha mwanangu katika hatua ambayo nilifurahi sana kumuona akiwa hivyo," Nihaya anasema huku akitokwa na machozi. "Sasa wanataka kumrudisha katika hali aliyokuwa nayo? Sitaki mwanangu afe."
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












