Je, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikosa fursa ya kuwazuia Hamas?

Netanyahu

Chanzo cha picha, Getty Images

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikuwa amekosa fursa ya kusitisha usambazaji wa pesa kwa Hamas.

Kwa mujibu wa Yudi Levi, afisa mkuu wa zamani wa ujasusi wa Israeli, Waziri Mkuu wa Israeli alipata fursa hii miaka kabla ya shambulio la umwagaji damu mnamo Oktoba.

Yudi Levi aliiambia BBC kwamba alimshauri Benjamin Netanyahu kulenga ufadhili wa Hamas.

Wanaamini kwamba kama hili lingetokea, lisingeipa Hamas fursa ya kuongeza nguvu zake za kijeshi. Lakini, Yudi Levi anasema kwamba hakuna hatua iliyochukuliwa kuhusu ujasusi huu.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel haijajibu madai haya.

Tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wenye silaha wa Hamas waliingia katika eneo la kusini mwa Israel, na kuua watu wapatao 1200 na kuchukua zaidi ya watu 250 mateka. Hakuna habari iliyopokelewa hadi sasa kuhusu mateka 130 kati ya hawa.

Katika kukabiliana na shambulio hili, jeshi la Israel lilishambulia Gaza. Kulingana na Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza, Wapalestina 29,000 wameuawa hadi sasa katika harakati za kijeshi za Israeli.

Hamas wanapata wapi fedha?

Yudi Levy anasema alionya kuhusu ufadhili mwingi kwa Hamas

Yudi Levy alikuwa mkuu wa kitengo cha vita vya kiuchumi katika wakala wa kijasusi wa Israel Mossad hadi 2016.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Anasema kwamba alimwambia Benjamin Netanyahu mara kadhaa kwamba Israel ina rasilimali za kutosha kuiangamiza Hamas, ambayo inadhibiti Gaza.

Inaweza kuondolewa tu 'kwa matumizi ya silaha za kifedha'.

Yudi Levi anasema kwamba hakupokea jibu lolote kutoka kwa Benjamin Netanyahu kuhusu pendekezo lake.

Alipoulizwa kama anaamini kulikuwa na uhusiano kati ya kusita kwa Netanyahu kusitisha ufadhili kwa Hamas na mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyofuata, Levy alijibu bila kusita.

"Ndiyo," Levi anasema. Kabisa. Inawezekana kabisa kwamba tungeweza kuzuia mtiririko wa pesa kwenda Gaza. Wakati huo, nguvu hatari na mbaya ambayo Hamas ilikuwa imekusanya isingeifanya kuwa adha kubwa kama ile tuliyokabiliana nayo tarehe 7 Oktoba.

Kulingana na afisa huyu wa zamani wa ujasusi wa Israel, Hamas ingehitaji 'si mamilioni, bali mabilioni ya dola' kuweka mtandao wa vichuguu chini ya Gaza na kulipia gharama za jeshi la wapiganaji wapatao elfu thelathini.

Chanzo kimoja mahususi cha ufadhili wa Hamas ambacho Yudi Levi alimwambia Benjamin Netanyahu kuhusu ni mpango wa uwekezaji wenye thamani ya mamilioni ya dola.

Kulingana na mashirika ya kijasusi ya Israel, akaunti hii ilikuwa inaendeshwa kutoka Uturuki na ilikuwa inadhibitiwa na Hamas.

Yudi Levi anasema licha ya kutoa taarifa hizo, Netanyahu aliamua kutochukua hatua zozote kuhusu taarifa hizo.

Hamas inataka nini?

Hamas inakataa haki ya Israel kuwepo na imejitolea kuiangamiza. Ni zaidi ya nguvu ya kijeshi tu. Hili ni vuguvugu la kisiasa, ambalo pia linapata usaidizi wa kifedha kutoka nje ya Gaza.

Kuhusu mazungumzo na Benjamin Netanyahu, Yudi Levi anasema, "Tulijadili msaada ambao Hamas inapata kutoka Qatar na Iran. Lakini, katika hali nyingi, Uturuki ni muhimu zaidi, kwa sababu Uturuki ni kitovu muhimu katika kusimamia muundo wa kifedha wa Hamas.

BBC imekuwa ikichunguza hati ambazo zilipatikana mwaka wa 2020. Hati hizi zinafichua wigo wa uwekezaji wa Hamas. Nyaraka hizi zinatoa taarifa kuhusu kipindi cha miezi minane, kilichomalizika mwaka wa 2018.

Mashirika ya kijasusi ya Israel yanasema kwamba hati hizi zinaonesha jinsi Hamas inavyopokea baadhi ya mapato yake.

Kwingineko hii inasemekana inajumuisha takribani makampuni 40, yaliyoenea katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Hizi pia ni pamoja na Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Misri, nchi za Ghuba na Uturuki.

Uwekezaji huu unaodaiwa ni kati ya ujenzi wa barabara, dawa na vifaa tiba, utalii, madini, utafutaji wa dhahabu na miradi ya mali isiyohamishika ya kifahari.

Hamas wamewekeza wapi?

Vyumba vya kifahari vilivyojengwa na kampuni ya Kituruki Trend GYO

Moja ya makampuni ambayo Marekani imepiga marufuku kuhusiana na Hamas ni Trend GYO. Hii ni kampuni ya mali isiyohamishika ya Uturuki. Kulingana na hati zilizopatikana mnamo 2018, kampuni hii pia imetajwa mara kadhaa kwa jina la Anda Turk.

Kulingana na hati hizo, hili lilikuwa jina la zamani la kampuni ya biashara na baadaye jina lake likabadilishwa kuwa Trend. Ilisajiliwa katika Soko la Hisa la Istanbul.

Hivi karibuni, mwenyekiti wa zamani wa Trend Hamid Abdullah al-Ahmar alisifu shambulio la Oktoba 7, ambalo Hamas wanaliita 'Operesheni Al Aqsa'. Hamid Abdullah alijiuzulu kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa kampuni hiyo mnamo 2022, lakini bado anabaki kuwa mkuu wa kampuni mama.

Hamid Abdullah anasikika akisema katika taarifa iliyorekodiwa wakati wa mkutano huko Istanbul mnamo Januari 2024, "Tunakutana wakati ... wakati Aqsa inafikia kilele chake, haya ni mafuriko makubwa." , ambayo haitakoma mpaka wale wanaoikalia kwa mabavu Palestina yetu tuipendayo washindwe.

Katika mkutano huu, Hamid Abdullah alikuwa ametoa wito wa 'kuendesha kampeni ya kuthibitisha kwamba Uyahudi wenye msimamo mkali ni vuguvugu la ubaguzi wa rangi na kigaidi'.

BBC ilitafuta maoni kutoka kwa Hamid Abdullah Al-Ahmar kuhusu suala hili, lakini hakuna jibu lililopokelewa kutoka kwake.

Trend alituambia kwamba madai ya Idara ya Hazina ya Marekani kuhusu uhusiano kati ya kampuni yake na Hamas 'hayana msingi na si ya haki'.

Maafisa wa Uturuki wamesema wamechunguza mwenendo huo na wamegundua 'hakuna ushahidi wa matumizi mabaya ya mfumo wa kifedha wa nchi yetu', na kwamba Uturuki inafuata sheria za kimataifa za kifedha.

Misaada inayotolewa kwa Hamas inatumika wapi?

Haiwezekani kukusanya taarifa ni kiasi gani cha fedha hizi zilizochangwa zilitumiwa na Hamas kuongeza nguvu zake za kijeshi na kama ilifanya hivyo au la.

Hamas inakanusha kutumia vibaya fedha zozote zilizopokelewa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. Hamas iliiambia BBC kwamba tawi lake la kijeshi lina vyanzo vyake vya mapato.

Waziri Mkuu wa Israel amesema wazi kwamba anapinga kabisa kuundwa taifa la Palestina. Je, lengo lao hili la kimkakati liliunganishwa vipi na ufadhili wa Hamas?

Netanyahu

Chanzo cha picha, Getty Images

Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu alikanusha kuwa alitaka kuifanya Hamas kuwa na nguvu. Netanyahu alikuwa amesema kuwa ameruhusu pesa alizopokea kutoka Qatar kwenda Gaza ili tu kuzuia majanga yoyote ya kibinadamu huko Gaza.

Benjamin Netanyahu ameapa kuwaangamiza Hamas. Anasema kuwa hakutakuwa na kipengele chochote kitakachosalia Gaza kinachosaidia ugaidi.

Lakini, kuangamizwa kwa Israel huko Gaza na kuwaua Wapalestina kwa wingi hivyo kunaweza kuwa na athari tofauti.