Jinsi akili bandia inavyofufua waigizaji nyota waliofariki katika tasnia ya filamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu mashuhuri kama vile James Dean wanaweza kufufuliwa kama waigizaji wa kidijitali kutokana na uwezo wa akili bandia, lakini inazua maswali ya kutatanisha kuhusu haki ambazo yeyote kati yetu anazo baada ya kufariki.
Waigizaji wengi wana ndoto ya kuendeleza taaluma zao hata baada ya wao kuondoka duniani au kuacha kazi.
Ingawa sio rahisi lakini wanaweza kufanikiwa kufikia aina hii ya maendeleo na kuendelea kuwepo kwenye skrini hata baada ya wao kufariki dunia.
Mmoja wa wasanii hao ni mwigizaji wa filamu wa Marekani James Dean, aliyefariki mwaka 1955 kwa ajali ya gari baada ya kuigiza katika filamu tatu tu ambazo zote zilivuma kweli kweli.
Lakini sasa, karibu miongo saba baada ya kifo chake, Dean ameigizwa kama nyota katika filamu mpya inayokuja iitwayo ‘Back to Eden’.
Mfumo wa kisasa wa uigizaji wa kidijitali - ilioundwa kwa kutumia teknolojia ya AI sawa na uliotumika katika kwenye ‘deepfake’ aina ya akili bandia inayotumiwa kwenye utengenezaji wa video za uongo zinazofanana na ukweli – yaani mhusika atatembea, kuzungumza na kutangamama na waigizaji wengine kwenye filamu katika skrini.
Mfumo huo uko katika hatua ya teknolojia ya juu ya picha zinazozalishwa na kompyuta za Hollywood yaani Hollywood computer generated imagery (CGI).
Lakini pia ndio kiini cha baadhi ya wasiwasi unaoibuliwa na waigizaji na waandishi wa filamu ambao wamegoma huko Hollywood kwa mara ya kwanza katika miaka 43.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wanahofia nafasi zao za kazi zitachukuliwa na teknolojia ya AI - kitu ambacho wanasema kitaondoa ubunifu kwa ajili ya kufaidika.
Mwigizaji Susan Sarandon ni miongoni mwa wale ambao wamezungumza kuhusu wasiwasi wake, akionya kwamba AI inaweza kumfanya "kusema na kutenda mambo ambayo sina chaguo kuyahusu".
Ufufuo wa kidijitali wa Dean sio mara ya kwanza yaani waigizaji walioaga dunia kufufuka na kuanza kuigiza kwenye skrini kwa usaidizi wa teknolojia ya hali ya juu ya kidijitali na kuthibitisha maajabu ya Hollywood.
Carrie Fisher, Harold Ramis na Paul Walker ni watu mashuhuri wachache tu waliorejelea kwenye uhusika wao mashuhuri katika filamu baada ya kufariki.
Mwimbaji wa Brazil Elis Regina pia alifufuka hivi karibuni kidigitali kwa tangazo la gari, ambapo alisikika akifanya maonyesho na binti yake Maria Rita.
Mwonekano wao kwenye skrini unawakilisha kile Travis Cloyd, mtendaji mkuu wa kampuni ya habari ya WorldwideXR (WXR), ambaye anarejelea hilo kama maonyesho ya "skrini ya 2D", sawa na video zinazotengenezwa kwa akili bandia.
Hii ni mara ya pili kwa teknolojia ya dijitali ya Dean kupangwa kwa ajili ya filamu.
Mnamo mwaka wa 2019, ilitangazwa kuwa atafufuliwa katika teknolojia ya CGI kwa filamu inayoitwa Finding Jack, lakini baadaye ikafutiliwa mbali.
Cloyd aliithibitishia BBC, hata hivyo, kwamba Dean badala yake ataigiza kwenye Back to Eden, filamu ya kubuni ya sayansi.
Uwepo tena wa Dean kidijitali pia unawakilisha mabadiliko makubwa katika kile kinachowezekana.
Sio tu kwamba uwepo wake kupitia teknolojia ya Al avatar yaani uwakilishi wa dijitali wa binadamu katika mazingira ya mtandaoni utamuwezesha kushiriki katika filamu ya Back to Eden na pia filamu nyingine kadhaa lakini pia ataweza kushirikiana na hadhira katika majukwaa ikiwemo kwenye mifumo ya ‘augmented reality’ unaochanganya ulimwengu halisi na maudhui yanayozalishwa na kompyuta, ‘virtual reality’ yaani mazingira yanayotokana na kompyuta yenye matukio na vitu vinavyoonekana kuwa halisi, na kumfanya mtumiaji kuhisi kuwa amezama katika mazingira yao na ‘gaming’ yaani mchezo wa video wa kompyuta.
Teknolojia hii inaenda mbali zaidi ya uundaji upya wa kidijitali au teknolojia ya akili bandia ya deepfake ambayo hufunika uso wa mtu mmoja juu ya mwili wa mtu mwingine.
Inaongeza matarajio ya waigizaji - au mtu mwingine yeyote yule - kufikia aina ya kutokufa ambayo isingewezekana katika taaluma zinazoendelea muda mrefu baada ya maisha yao kumalizika duniani.

Chanzo cha picha, Alamy
Lakini pia inazua maswali kadhaa yenye kuibua wasiwasi.
Nani anamiliki haki za uso, sauti na nafsi ya mtu baada ya kufa?
Je, wanaweza kuwa na udhibiti gani juu ya mwelekeo wa taaluma yao baada ya kifo - je, mwigizaji aliyeigiza na kuvuma katika tamthilia za mudhui mabaya anaweza kuonyeshwa ghafla katika simulizi za vichekesho au hata ponografia?
Je, zinaweza kutumika kwa matangazo ya kibiashara bila malipo?
Hivyo basi kunaibuka swali jingine, kwa nini tusiwaache watu mashuhuri wapumzike kwa amani?
Binamu wa Dean, Marc Winslow, ambaye utotoni wake aliishi shambani huko Illinois na Dean, anashuku kuwa ni mvuto wake kwenye skrini na kumfanya kuwa chaguo la kuvutia kwa uhusika mkuu katika sinema ya kisasa.
"Ikiwa kuna watu wengine wawili au watatu kwenye tukio katika filamu, hamu yako moja kwa moja itaelekea kwake," anasema.
"Unajua, sidhani kama kuna mtu yeyote ataweza kuchukua nafasi zao, lakini inawezekana hilo likafanyika kwenye skrini na kuifanya kuwa kama halisi."
Teknolojia mpya inayohusika katika ufufuaji wa waliokufa
Picha ya Dean ni mojawapo ya mamia yanayowakilishwa na kampuni ya WRX na kampuni dada ya kutoa leseni ya CMG Ulimwenguni kote - ikiwa ni pamoja na Amelia Earhart, Bettie Page, Malcolm X na Rosa Parks.
Wakati Dean alipofariki miaka 68 iliyopita, aliacha nyuma mkusanyiko thabiti wa mfano wake katika filamu, picha na sauti - kile ambacho Cloyd wa WRX anakiita "chanzo cha nyenzo".
Cloyd anasema ili kufikia uwakilishi wa picha halisi wa Dean, picha nyingi huchanganuliwa, hupangwa kwa ubora wa juu na kuchakatwa na timu ya wataalam wa kidijitali kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
Sauti, video na Al na nyenzo hizi huwa msingi wa data za kidijitali ambayo mwisho wa siku zinaonekana, kusikika, kusonga na hata kujibu maongezi kama vile ya Dean.
Kile ambacho Dean hakuacha nyuma ni data zake kwenye mfumo wa kidijitali, tofauti na nyota wa siku hizi wanaojihusisha na mitandao ya kijamii, kupiga picha za kibinafsi, kutuma ujumbe na barua pepe, kutumia injini za utafutaji, kununua bidhaa na kununua dawa mtandaoni.
Shughuli hizi hutoa kiasi kikubwa cha data kuhusu jinsi tunavyofikiri na kutenda ambayo inaweza kutumika kuchukua data muhimu kidijitali kutoka kwa picha za kawaida hadi kwa mfumo wa Al ambao unawezesha aliyekufa kuzungumza na walio hai kwa njia ya kushawishi.
Sasa kuna makampuni ambayo huruhusu watumiaji kupakia data ya kidijitali ya mpendwa wao aliyekufa ili kuunda kile kinachofahamika kama "deadbots" data ambayo huwezesha kuzungumza na watu waliokufa kwa kuiga majibu yao.
Nyenzo zikipatikana zaidi, ndivyo mfumo wa akili bandia unaotumia data kupitia deadbot unavyokuwa sahihi zaidi, ikimaanisha kuwa unawezesha mfano wa kweli wa nyota aliyekufa kuendelea kufanya kazi katika tasnia ya filamu - na kuchangamana kwa uhuru - kwa mtindo endelevu.
Mwigizaji Tom Hanks hivi majuzi alitabiri kwamba anaweza kufanya kazi vizuri zaidi hata baada ya maisha yake duniani, akiambia Adam Buxton Podcast, "Ninaweza kugongwa na basi kesho na ikawa hivyo, lakini maonyesho yangu yanaweza kuendelea na kuendelea."
Waigizaji wanaopoteza kazi kutokana na nyota waliokufa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maoni ya Hanks yanadokeza kuhusu wasiwasi wa kweli kwa waigizaji wanaohofia kwamba awamu inayofuata ya ufufuo wa binadamu kidijitali itawasilisha masuala yanayotatiza kimaadili, kisheria na kiutendaji kwa watu mashuhuri na raia wa kila siku.
Hasa waigizaji ambao hutia sauti kwenye kwenye filamu, wamekuwa wakiongoza mazungumzo na kufanyia kazi uundaji wa chama kitakachowezesha kulinda haki na kazi za waigizaji.
"Kwa sauti za Mickey Mouse, Porky Pig, Snow White - kila wakati sauti inapojitokeza, mwigizaji mpya anaajiriwa kuigiza sauti hiyo," anasema Tim Friedlander, rais na mwanzilishi wa Chama cha Kitaifa cha Waigizaji wa Sauti Marekani.
"Lakini vipi ikiwa ungetumia sauti ya Mel Blanc [mwigizaji wa sauti ambaye alitumika kwa wahusika wengi wa katuni ya Loony Tunes] milele?"
Friedlander na waigizaji wenzake wa sauti wanahofia kuwa hali hii inakaribia kutekelezeka, na kwamba waigizaji wa sauti waliofufuliwa kidijitali watahodhi tasnia ya sauti, na kumaliza ajira kwa waigizaji ambao bado wako hai.
"Hakuna fursa kwa mtu mwingine yeyote anayeishi kwa sababu sasa wamepoteza kazi zao kwa mwigizaji wa sauti aliyekufa kwa sababu yeye ndiye sauti asili ya Bugs Bunny, Porky Pig na wengine [wahusika wa Looney Tunes].
Haki za wafu
Ikiwa wafu - au tuseme, digital clones (mfumo wa teknolojia mpya unawezesha kudhibiti sauti, picha na video zilizopo kwa sasa ambazo ni za uhalisia zaidi) - kunasemekana kuwezesha waliofariki kufaidika kifedha na kuwa na haki?
Unaweza kusema, sheria hazieleweki na katika baadhi ya sehemu za duniani, teknolojia hii bado haijafika.
Kwa ujumla, mtu nyota anapokufa, "haki za utangazaji" hupitishwa kutoka kwa mtu huyo mashuhuri hadi kwa jamaa, au kwa yule aliyepewa haki hizi kwa wosia.
Lakini Kahn anasema hata wosia, ambayo kwa kawaida itaamuru nani atafaidika kifedha kutokana na matumizi ya kibiashara ya sura au kitu kingine chochote cha mtu aliyekufa, ina uzito mdogo wa kisheria kwani "sio kama mkataba kwa sababu ni hati ya upande moja".
Uwezo wa jinsi picha ya mtu huyo inavyotumika hupitia kwa mtekelezaji wake aliyehai.
Watu mashuhuri wachache, kama vile Robin Williams, waliweza kutumia wosia kupunguza matumizi ya mfano wao baada ya kifo, lakini kikomo hicho kinaisha baada ya miaka 25.
Matumizi ya watu kibinafsi
Ingawa watu mashuhuri waliokufa wana ulinzi usio wazi katika maeneo mahususi linapokuja suala la kibiashara kwa utumiaji wa sura au mfano wao, raia wa kawaida wanaweza kuwa na udhibiti mdogo sana wa jinsi mfano wao na urithi wao wa kidijitali unavyotumika baada ya kifo.
Nchini Marekani, kuna sheria ndogo inayolinda wafu dhidi ya kufufuliwa kidijitali kwa matumizi ya kibinafsi.
Unapokufa, karibu mtu yeyote anaweza kupakia urithi wako wa kidigitali unaoweza kufikiwa na umma kwenye programu ya AI ili kuweka data kwenye mfumo wa deadbot au AI avatar.
Majimbo yenye ulinzi mpana zaidi wa baada ya kifo, kama vile New York, yanapiga marufuku matumizi ya utambulisho wa watu binafsi kwa madhumuni fulani maovu, lakini Lee ana shaka kuhusu jinsi ulinzi huu unavyotekelezwa.
Cloyd, Friedlander na Kahn wote wanakubali kwamba kuna haja ya kuwa na sheria iliyowekwa mapema badala ya baadaye kulinda haki na urithi wa wafu - watu mashuhuri na vinginevyo.
Teknolojia inasonga mbele kwa kasi kubwa, na mijadala ya kimaadili kuhusu uwakilishi wa kidijitali kwa waliofariki tayari inaongezeka.
Cloyd anakiri mwanzoni kuwa na "wasiwasi kidogo" kuhusu jinsi wafu wanavyohuishwa kidijitali lakini anasema ana imani kuwa WXR inafanya kazi kwa umakini katika kushughulikia masuala haya.
Friedlander, pia, anatetea kikamilifu sheria inayowalinda waigizaji wa sauti kutokana na kupoteza kazi, na anatumai kuwa kazi ya Nava itasaidia vyama vya waigizaji duniani kote kuandaa na kutetea fursa za haki.















