Je, Akili Bandia(AI) inaweza kuchukua nafasi ya DJ kwenye ukumbi wa burudani?

Nooriyah amekuwa akifanya kazi ya DJ na kuzalisha muziki kwa miaaka minane.
Maelezo ya picha, Nooriyah amekuwa akifanya kazi ya DJ na kuzalisha muziki kwa miaaka minane.

Hebu tafakari uko kwenye ukumbi wa burudani, muziki unavuma na taa zinawaka.

Unatazama eneo analofanyia kazi DJ lakini hakuna mtu, kwa sababu ni mchanganyiko wa muziki ulioandaliwa kwa kutumia tenknolojia ya Akili Bandia.

Huku programu za kisasa za kuchanganya muziki zikiendelea kupata umaarufu na kumbi za burudani zikipunguza gharama, baadhi ya watu katika tasnia ya muziki wa dansi wana wasiwasi huenda wakapoteza kazi zao.

Lakini je, programu ya kompyuta inaweza kuchukua nafasi ya muunganisho wa maisha halisi kati ya DJ na watu waojivinjari katika kumbi za burudani?

Hapana. Hii ni kwa mujibu wa maoni ya Nooriyah.

Yeye ni DJ mwenye umri wa miaka 28 anayeishi London. Anacheza miziki kwenye kumbi tofauti za burudani kote duniani, wakati mwingine kwa umati wa zaidi ya watu 40,000.

Programu za Akili Bandia(AI) zimekuwa zikitumika katika tasnia yake kwa miaka, ikipendekeza nyimbo za kuchanganya kulingana na midundo.

Lakini bado haijachukua kazi ya Nooriyah, na anafikiri anajua ni kwa nini.

"Kwa sababu jinsi ninavyojumuika na mashabiki wangu ni ngumu sana kuiga," anasema.

''Hebu tafakari mtu akinitazama wakati nina DJ, akiniona nikitoka jasho na kucheza kama wao.

"Wakati huo wanahisi uhusiano huo wa karibu ambao Akili Bandia haikuweza kifikia."

HANNAH ROSE

Chanzo cha picha, HANNAH ROSE

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hannah Rose alijifunza kuwa DJ wakati wa lockdown na anajitahidi kuifanya iwe chanzo chake kikuu cha mapato.

Anapata kazi nyingi lakini ameona kumbi aq burudani zinabana matumizi huku mzozo wa gharama ya maisha unavyozidi.

"Tangu wakati wa Covid kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa watu wanaouliza kutiririsha muziki," anasema.

"Hasa ikiwa ni sehemu ya nje ya nchi, ikiwa hawana uwezo wa kukusafirisha nchi tofauti ucheze muziki, ni njia rahisi ya wasanii kutumbuiza bila kuwaweka kwenye chumba."

Hannah aligundua kuwa vilabu vingi vya usiku tayari vina kamera iliyowekwa kwa ajili ya kutiririsha muziki badala ya kutumia DJ.

Sasa ana wasiwasi kwamba mfumo huu uhuenda ukaathiri hata seti ya muziki inayochezwa mtandaoni.

"Wana njia ndefu ya kuendana na akili ya mwanadamu, lakini kwa Akili Nandia kutengeneza nyimbo asili, inaweza kuwa habari mbaya kwa Ma-DJ siku zijazo," anasema.

Mnamo Machi mwaka huu, ukumbi wa East London uliandaa tamasha la Akili Bandia lakini hatua hiyo ilipokelewa kwa maoni mseto, baadhi ya watu walifurahia wengine walihisi ''haukuwa na mashiko''.

Muziki wa dansi ni mojawapo ya aina ya muziki inayopendwa sana nchini Uingereza - lakini ma-DJ wanasema uungwaji mkono unaopata hauonyeshi hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muziki wa dansi ni mojawapo ya aina ya muziki inayopendwa sana nchini Uingereza - lakini ma-DJ wanasema uungwaji mkono unaopata hauonyeshi hilo.

Huenda wanadamu wakawa DJ bora zaidi lakini si hadithi ya moja kwa moja kwa watayarishaji.

Pamoja na kuwa DJ, Nooriyah anatengeneza muziki wake mwenyewe.

Mchakato wake wa ubunifu kwa sasa unahusisha kujaribu sauti tofauti kwenye programu, kabla ya kusimamia nyimbo. Ni hatua hii ya mwisho ambapo Akili Bandia inakuja.

"Kwangu mimi, mazungumzo kuhusu teknolojia ya Bandia katika uandaaji wa muziki yamechelewa sana," anasema.

"Tayari kuna karibu programu 10 tofauti za programu zinazochanganya muziki na zinaweza kuwwafanya watayarishaji wakapoteza kazi".

Anataka kuona mazungumzo yenye tija kati ya wale walio katika tasnia ya muziki na watengenezaji wa Akili Bandia.

"Nadhani hatari hapa ni kwamba kuna kazi inafanywa bila majadiliano kuhusu athari ya teknolojia hii kwa tasnia ya muziki."

Suluhu moja, anasema, ni kuzitoza ushuru kampuni za Akili Bandia.

"Kwanza, hebu tupunguze kasi ya uundaji wa programu hizi za Akili Bandia, na kuwatoza kodi watengenezaji, kuwekeza pesa hizo katika kutoa mafunzo kwa watu wanaopoteza kazi zao kutokana na teknoloia hii mpya."

Phil Kear anaunga mkono wazo hilo, kwani yeye pia anafanya kazi na Muungano wa Muziki. Hofu yake ni kwamba Akili Bandia itaweka kikomo kwa kiwango cha pesa ambazo watu wako tayari kulipa kwa rekodi zilizotengenezwa na waundaji wa kibinadamu.

"Muziki wa Akili Bandia utakuwa wa bei nafuu," anasema. "Na nadhani watu shauku ya kuitumia, labda baa."

Ingawa anasema, ushawishi wake kamili utategemea jinsi wanadamu watakavyoruhusu.

"Mengi yataamuliwa na utayari wa umma kukubali Akili Bandia au ubora wa muziki inayoweza kutayarisha."

Laini

Hafikirii kuwa muziki mwingi wa kibiashara utaathiriwa, lakini anaangazia muziki unaochezwa "chini kwa chini" kama eneo lililo hatarini.

"Kwa muziki wa kwenye Televisheni na filamu, nadhani umma utakuwa tayari zaidi kukubali muziki unaozalishwa na AI kwa sababu hakuna utu unaohusishwa nao," anasema.

"Lakini katika baa na vilabu nadhani kuna kiasi fulani cha uwekezaji."

Kama tasnia nyingi, ulimwengu wa muziki tayari umeathiriwa na maendeleo ya teknolojia.

Kwa Nooriyah, maendeleo haya ni sawa.

"Muziki umebadilika kwa kasi bkadiri muda unavyosonga. Tulitoka kwenye kanda hadi CD, hadi kwa redio mpaka sasa tunatoa huduma za utiririshaji, na katika kila ngazi, waliohusika moja kwa moja na utayarishaji wa muziki wa wakati huo waliathiriwa. Hii ya Akili Badia sio tofauti."

"Tunahitaji tu kurekebisha mifumu ya utendaji kazi, kutafuta msingi wetu na kudhibiti mambo ili Akili Bandia iwe mshiriki wa kusisimua badala ya adui."