Dhana tano potofu kuhusu ukuta Mkubwa wa China

FV

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Ukuta Mkubwa wa China ni mojawapo ya kuta na ngome zilizojengwa katika China ya kale, miaka 500 iliyopita. Makadirio ya urefu wake ni kati ya kilomita 2,400 hadi 8,000.

Mwaka 2012, Wizara ya Urithi na Utamaduni ya China ilifichua katika utafiti kwamba urefu wa Ukuta ni kilomita 21,000.

Ukuta huu ni maarufu sana duniani kote. Lakini kuna mawazo mengi na habari potofu kuuhusu. Zijue imani tano potofu kuhusu ukuta wa China.

Unaweza kuonekana kutokea mwezini

DC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mchoroji wa Marekani, Robert Ripley ndiye wa kwanza aliyekuja na dhana kwamba Ukuta wa China unaonekana kutokea mwezini.

Moja ya filamu zake 'Believe it and not!' Aliutaja Ukuta Mkubwa wa China kuwa 'kazi kubwa zaidi ya mwanadamu', akadai unaweza kuonekana kwa jicho la mwanadamu hata mwezini.

Bila shaka, dai hilo halikutegemea uthibitisho wowote, kwani lilitolewa miaka 30 kabla ya mwanadamu yeyote kutembea juu ya mwezi.

Joseph Needham, mtaalamu wa historia na utamaduni kutoka China na mwandishi wa kitabu cha 'Science and Civilization in China,'' alisema 'ukuta wa China ni ujenzi pekee wa binadamu unaoweza kuonekana hata na wanaanga.'

Madai yake yalikataliwa na wanaanga. Lakini madai kuwa ukuta huo unaonekana kutokea mwezini bado yanaaminiwa na baadhi ya watu.

Wakati wa safari ya kwanza ya anga za juu ya China 2003, mwanaanga Yang Liwai aliizika dhana hii, alisema hakuona chochote duniani kutoka angani.

Ni ukuta mmoja

FVC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Dhana hii inadai ukuta huu ni kama jengo moja kutoka mwanzo hadi mwisho, lakini hilo si kweli. Ukuta huu ni mkusanyiko wa kuta mbalimbali, ngome, vizuizi, minara na vituo.

Zipo sehemu zake zilizotunzwa vizuri na zipo sehemu zinazopita kwenye misitu ya nyika na hazipitiwi na watembea kwa miguu. Kuna vichaka, magofu na ukuta umepita kwenye maji.

Kuna sehemu za ukuta huu zimeundwa kwa tabaka mbili, tatu au hata nne na sehemu hizi hukutana.

Sehemu ya Ukuta unaouona karibu na Beijing una mabaki ya kiakiolojia, baadhi ya mabaki yapo chini ya Ukuta wenyewe.

Ulijengwa ili kuwazuia Wamongolia

DC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Ukuta wa China uliamriwa kujengwa na mfalme wa China ambaye alikufa 210 BC. Mfalme huyo aliishi kabla ya Wamongolia kuja kwenye eneo la China.

Vita na Wamongolia vilianza mwishoni mwa karne ya 14 wakati Mfalme Ming alipowafukuza Wamongolia kutoka China.

Miili ya wafanyakazi imezikwa kwenye ukuta

Kuna uvumi kuhusu Ukuta wa China kwamba miili ya wafanyakazi walioujenga imezikwa katika Ukuta huo.

Hadithi hii huenda ilitoka kwa Sima Qian, mwanahistoria wa wakati wa Ufalme wa Han, ambaye alimkosoa Mfalme wake mwenyewe kwa kumtusi mtangulizi wake, Mfalme Qin Shi Huang

Hata hivyo, hakuna mifupa ya binadamu ambayo imewahi kupatikana kutoka kwenye ukuta huu na hakuna ushahidi uliopatikana. Wala uvumi huu hautajwi na wanakiolojia au kumbukumbu za zamani.

Marco Polo hakuwahi kuuona

DC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mfanyabiashara, mvumbuzi na mwandishi wa Vietnam, Marco Polo hakuwahi kuutaja Ukuta wa China. Ilitumiwa hoja ya kutoutaja Ukuta wa China kama hoja kwamba hakuwahi kwenda China.

Mwishoni mwa karne ya 13, China yote ilitawaliwa na Wamongolia, kwa hivyo ukuta haukuwepo kwani wavamizi hao waliuharibu huko kaskazini mwa China wakati wa utawala wa mfalme wao Genghis Khan miaka 50 mapema.

Huenda Marco Polo aliuvuka mara kadhaa alipokuwa akitoka Beijing kuelekea kasri ya Kublai Khan huko Shangdu, lakini asingekuwa na sababu ya kuuzingatia.