Yafahamu maeneo 5 'matakatifu' ya kale zaidi duniani

CHRIS RAINIER

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Kuanzia mawe ya siri ya Mongolia hadi miji iliyoanzishwa kuheshimu wafu, maeneo ya kale matakatifu yalijengwa na watu kujaribu kuelezea maana ya maisha, kifo na dunia yanapatikana katika maeneo mbali mbali ya sayari dunia.

Maana ya maisha ni siri ambayo tamaduni nyingi ziumekuwa zikihangaika kuijua katika miaka yote.

Siri hii imepelekea kubuniwa kwa sehemu takatifu, huku watu duniani wakijenga majengo ya kuvutia ya kuheshimu miungi yao, huku wengine wakiamini ukuu wa vitu asili, wakitafuta jinsi ya kuwa na mahusiano na misitu mitakatifu, milima mitakatifu na miamba mitakatifu.

 Kuanzia kujengwa kwa Stonehenge katika England hadi piramidi za Chichen Itza nchini Mexico,ustaarabu wa kale ulifikia kiwango cha kuweka misimu ya kipupwe hadi kiangazi, kukusanyika kwa mababu au kuwepo kwa uhusiano baina ya binadamu hai na roho za wafu.

Mambo yote haya yana uhusiano wa ukweli kwamba watu wamekuwa wakitaka kutafuta ukweli kuhusu maisha, kifo na dunia.

 Neno "utakatifu" bila shaka limepotoshwa. Lakini kutokana na upatikanaji wa intaneti, huwa tunasahau kwamba bado kuna kitu ambacho hakijulikani kuhusu dunia yetu. 

Hatuwezi kusahau kwamba bado kuna maeneo matakatifu na maeneo tambarare .

Utakatifu unaweza kuwa njia tu iliyopo kwenye mto au kutembea kwenye eneo la bustani, kutafuta sauti asilia za nyikani." Rainier anasema. 

G

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Uchochoro cha mifupa ya Nyangumi ,Urusi

Kwenye kisiwa cha Yttygran , aneo la mbali , kisiwa chenye upepo kilichopo kwenye Bahari ya Siberia ya Bering, zinapatikana mifupa iliyopangwa ya mbavu za nyangumi na uti wa mgongo inayofahamika kama "Uchochoro wa mifupa ya nyangumi’’.

Eneo hili ambalo ni njia yenye urefu wa mita 550, iliyopo kando ya bahari ni eneo la kuvutia sana, anasema Chris Rainier, mtafiti wa masuala ya historia ya binadamu

 Majengo haya ya mifupa ya nyangumi yalijengwa na watu wa jamii ya Yupik, na inakadiriwa kuwa yamekuweko kwa miaka 2,000 ," Wanasema wataalamu

 Nadharia ya Kiakiolojia inaelezea kuwa eneo hilo lilikuwa ni mahala ambapo watu walikuwa wakikutana.

Walijenga mifupa ya nyangumi na kuiwekea Ngozi saw ana ile ya ng’ombe au dubu, juu ya jengo ili kubuni ukumbi wa mkutano. Walitumia eneo hilo kufanya mikutano mitakatifu. Kile kilichobakia kwa sasa ni mifupa ya nyangumi."

Getty

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Hegra, Saudi Arabia

Hegra ulikuwa ni mji wa pili wa watu wa jamii ya Nabataea , ambao walijenga mji wao maarufu wa , Petra, zaidi ya kilomita 500 kaskazini magharibi mwa Jordan ya sasa. 

Ukiwa katika jimbo la AlUla la Saudi Arabia, mji huo wa kale wa mawe (unaofahamika kwa Waislamu kama Al-Hijr na Mada'in Salih) ulijengwa tangu Karne ya 1 BC ( Kabla ya Kristo). Ni eneo la kwanza la nchi hiyo la urithi la Shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO, eneo ambalo lina makaburi yaliyohifadhiwa vyema zaidi ya 100 yaliyomo katika mawe.

"Haya ni maeneo ya makaburi ya wafalme, Malkia na waheshimiwa, sawa tu Petra," anasema Rainier.

Getty

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Mwamba wa kale uliochongwa kwa ustadi wa hali ya juu unapatikana eneo lote la Kusini magharibi mwa Marekani, ikiwa ni pamoja na Utah, New Mexico, Arizona, na Colorado. Ikijulikana kama miamba iliyopinda-petroglyphs, picha hizi – ambazo nyingi zilibuniwa na tamaduni za Fremont na Anasazi - mara nyingi huonyesha maumbile ya binadamu, wanyama, silaha za kuwinda na alama za mikono.

Maeneo haya yanachukuliwa kama maeneo matakatifu na Wamarekani wazawa, ambao ndani yake wanaiona kama viunganishi vinavyowaunganisha na nyakati zilizopita na urithi wa utamaduni wao.

"Nikiishi katika Santa Fe, New Mexico, nimekuwa kila mara nikivutiwa na watu wa Mataifa ya kwanza," Rainier anasema.

"Picha hii ilichukuliwa katika Utah. Alama hizi za mikoni zinadhaniwa kuwekwa miaka ipatayo 4,000, lakini iko katika hali ya maridadi.

Getty

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Mawe ya kale ya kulungu, Mongolia

“Mongolia ni nchi ya ajabu yenye historia ya kuvutia na ya muda mrefu,” anasema Rainier. "Kuna maeneo ya makaburi ya kale yaliyotawanyika katika maeno mbali mbali ya kaskazini mwa Mongolia.

Wakati unapovuka eneo lenye savana, utaona rundo kubwa la mawe.

Ndani ya maeneo haya ya kuzika walizikwa mashujaa wa vita walioheshimiwa zaidi. Katika makaburi hayo vimezikwa vitu kama mikuki, maboksi ya vipuri, na mali nyingine mbali mbali ambazo wapiganaji hao jasiri walizimiliki wakati wa uhai wao."

CHRIS RAINIER

Chanzo cha picha, CHRIS RAINIER

Maelezo ya picha, Jengo maarufu la hekalu ya Angkor Wat ni mojawapo ya minara mikubwa zaidi duniani

Jengo maarufu la hekalu ya Angkor Wat

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jengo la maarufu la hekalu ya Angkor Wat ni mnara mkubwa zaidi wa kidini duniani. Linachukua kilomita za eneo 400, nje kidogo ya Siem Reap. Hekalu hilo lililojengwa karibu karne ya 12 kama makao makuu ya Himaya ya Khmer Empire, ambalo ni urithi wa UNESCO kwa sasa, mwanzoni lilitumika kama hekalu la Hindu , lakini liligeuzwa kuwa hekalu la Budha mwishoni mwa karne na hivi sasa ni mojawapo ya maeneo ya hija ya Wabudha.

 Makasisi, watawa, Wakambodia na wageni wa Kibudha huja hapa kila siku kufanya ibada na kutoa sadaka, huku wasafiri mara kwa mara wakikusanyika kila asubuhi kutizama jua likiwasha mwangaza hekalu – uzoefu wa kiroho kwa wengi.

Eneo la Angkor linajumuisha hekalu 70 na karibu majengo 1, 000 , na kuwapa wasafiri wanaokuja kulizulu mengi ya kujifunza na kugundua. Kuna sanabu zisizohesabika za Budha, pamoja na sanamu na vinyago vinavyoelezea hadithi za Kibudha, ingawa kwa heshima ya sanamu za Wahindu na vinyago pia vimehifadhiwa .