Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 27.10.2024

Mario Balotelli

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mchezaji huru Mario Balotelli anakaribia kurejea Serie A, West Ham wanaweza kumnunua Ben Chilwell wa Chelsea mwezi Januari, kuongeza mkataba wa Jamal Musiala ni kipaumbele kwa Bayern Munich.

Mshambulizi wa zamani wa Italia Mario Balotelli, 34, anakaribia kujiunga na Genoa ya Serie A kama mchezaji huru. (Sky Italy)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham wanaweza kumnunua beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell, 27 kutoka Chelsea mwezi Januari. (Inside Track podcast, via Team talk)

,

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuongeza mkataba wa kiungo mkabaji Jamal Musiala, 21, ambao unadumu hadi 2026, ni kipaumbele kwa Bayern Munich. (Bild - in German)

Borussia Dortmund kwa sasa hawana mpango wa kuchukua nafasi ya Nuri Şahin kama meneja licha ya klabu hiyo kuwa katika nafasi ya saba kwenye Bundesliga kufuatia kushindwa Jumamosi na Augsburg. (Sky Germany)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace wanasitasita kuanzisha tena mazungumzo na Newcastle United kuhusu mlinzi wa Uingereza Marc Guehi, 24, wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari. (Football Insider)

Juventus wako tayari kufanya mazungumzo mapya na Udinese kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Italia Lorenzo Lucca, 24. (Rudy Galetti)

Raphinha

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanaamini kwamba mkataba mpya na winga wa Brazil Raphinha utafanyika. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 utaendelea hadi 2027. (Diario Sport - in Spanish)

Wakati huo huo, majadiliano kuhusu mkataba mpya kati ya kiungo wa kati wa Barca na Uhispania Pedri, 21, yanaendelea vyema. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Porto wa Ureno Diogo Costa, 25, ambaye pia anasakwa na Manchester City, lakini kitita cha kumsajili kichoongezeka hadi euro 45m (£37.5m) inafanya dili kuwa gumu. (Sport - in Spanish)

Fowadi wa Ghana Antoine Semenyo alitia saini kuongeza mkataba wake msimu wa joto lakini vilabu kama Newcastle na Tottenham vinavyomwinda huenda vikaona ofa ya Bournemouth kwa mchezaji huyo wa miaka 24 kama mpango mwingine wa kumbakisha katika klabu hiyo. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Asha Juma