Fahamu uzuri na ubaya wa utamaduni wa kubadilishana jezi katika soka

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati mlinzi wa Inter Milan, Francesco Acerbi alipomwomba nyota wa Manchester City, Erling Haaland kwa utani, jezi mbili baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumatano usiku, huenda alikuwa akijaribu bahati yake.
Kubadilishana shati kwa muda mrefu umekuwa utamaduni katika soka, hata hivyo, na wachezaji wengi wanaona fahari kubwa katika makusanyo ya kuvutia wanayoweza kuweka majumbani mwao..
Baadhi ya mashati, kwa kawaida, yanahitajika zaidi kuliko mengine, huku timu moja ikisafiri kwenda kwenye mechi ikiwa na mifuko kadhaa iliyojaa shati zake ili kuzitoa kwa niaba ya mchezaji wao nyota.
Lakini wachezaji hufanya nini hasa na mashati wanayopata? Na je shati hizo hutendewa usawa mara tu ubadilishanaji unapofanywa mbele ya kamera?
Nani anayejivunia mkusanyiko mkubwa zaidi wa jezi?

Chanzo cha picha, Lionel Messi
Wachezaji wengi wameonesha mkusanyiko wao wa jezi za soka kwenye mitandao ya kijamii, huku vyumba vizima vikitengwa kwa ajili ya kuonyesha jezi zinazoheshimika zaidi.
Lionel Messi, ambaye si mgeni katika mahitaji ya kubadilishana shati kama mchezaji bora zaidi wa wakati wote, alichapisha picha ya mkusanyiko wa jezi zake ambao ulionyesha mashati yaliyofunika kuta .

Chanzo cha picha, Gerard Pique
Beki wa zamani wa Barcelona, Gerard Pique alisema "alikuwa akikagua chumbani mwake" alipokutana na mashati ya watu wengi, ambao unajumuisha jezi za Messi, Andrea Pirlo na David Beckham.
Pique aliongeza kuwa alikuwa ameitengenezea fremu jezi aliyobadilishana baada ya fainali ya Kombe la Dunia 2010, ambapo timu yake ya Uhispania iliifunga Uholanzi, kutoka kwa mshambuliaji wa Uholanzi Klaas-Jan Huntelaar.

Chanzo cha picha, Spaletti Luciano
Lakini mkusanyiko wa tuzo uliovutia zaidi kati ya yote kwa hakika unakwenda kwa meneja wa Italia Luciano Spalletti.
Baada ya kuiongoza Inter Milan kurudi kwenye shindano la klabu kuu Uropa mwaka 2019, Spalletti alijumuishwa katika mkusanyiko wa "majina kutoka Ligi ya Mabingwa", ya wababe wengi wa mchezo huo.
Je, jezi nyingine ni muhimu zaidi?
Wachezaji wengine lazima washughulikie mahitaji makubwa zaidi ya shati zao kuliko wengine.
Messi anajua hili kama mtu yeyote, lakini nyota huyo wa Argentina ameunda mifumo ya kukabiliana nayo tatizo hilo wakati wa kipindi chake cote cha soka.
Kipa Emiliano Martinez aliiambia Prime Sport kwamba mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina hutayarisha jezi 650 za Messi kwa kila mechi mbili, zitakazogawanywa kati ya wachezaji, wafanyakazi, wafadhili na hata wasimamizi karibu na siku za mechi.
Martinez mara kwa mara huombwa jezi za Messi na, kwenye Kombe la Dunia la 2022, alipunguza pigo la kushindwa kwa Poland na Argentina kwa mchezaji mwenzake wa Aston Villa Matty Cash kwa kumpa moja.

Chanzo cha picha, Matty Cash
Lakini sio majina makubwa tu. Wayne Rooney alikiri kwamba kiburi chake wakati akicheza kilimaanisha kwamba hatawahi kuomba shati kutoka kwa mpinzani; hata hivyo, daima angemheshimu mchezaji yeyote ambaye angeomba shati yake.
Na kwa hivyo, ingawa hana jezi za wachezaji kama vile Zinedine Zidane, nyota huyo wa zamani wa England na Manchester United anamiliki jezi ya Andorra kutoka kwa Ildefons Lima - ambaye alifurahi kugundua Rooney alikuwa ameiweka.
"Siku zote nilimheshimu mchezaji yeyote aliyekuja na kuniuliza shati yangu," Rooney aliambia BBC 5 Live mapema mwaka huu.
"Nimeona wachezaji ambapo wanaitupa tu kwenye mkusanyiko wa jezi walionao na hawapendezwi, ambapo mara zote mimi huonyesha heshima na kuipeleka nyumbani ili kuihifadhi''.
Fahamu uzuri na ubaya wa utamaduni wa kubadilishana jezi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Utamaduni wa kubadilishana jezi unasemekana ulianza nchini Ufaransa, baada ya kuishinda Uingereza, ilipoomba kubadilishana na wapinzani wao ili kukumbuka ushindi wao wa 1931.
Mojawapo ya mazungumzo mashuhuri katika historia yalifanyika mnamo 1970, wakati nyota wa Brazil Pele na nyota wa Uingereza Bobby Moore walibadilishana mashati kufuatia mechi ya makundi ya Kombe la Dunia kati ya mataifa hayo mawili nchini Mexico.
Mkusanyiko wa mashati siku hizi ni chanzo cha kupendeza na faraja kwa wengi.
Lakini kitu ambacho hakijaonekana katika miaka ya hivi karibuni ni kubadilishana kwa shati wakati wa muda wa mapumziko.
Mario Balotelli alikemewa na Liverpool baada ya kubadilishana shati na Pepe wa Real Madrid wakati timu yake ilipokuwa nyuma kwa magoli 3-0 kufikia kipindi cha mapumziko mwaka 2014, na 2016 Eden Hazard alizomewa na mashabiki wa Chelsea kwa kubadilishana shati na winga wa Paris St-Germain Angel di Maria. .
Wakati wa kampeni za Ligi ya Mabingwa mwaka jana, Haaland aliombwa wabadilishane jezi wakati wa mapumziko na nahodha wa Young Boys, Mohamed Ali Camara, baada ya kupoteza 3-0 " na meneja wake alisema atakuwa na mazungumzo naye ".
Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson pia hakufurahishwa na mshambulizi Ruud van Nistelrooy aliporejea kwenye chumba cha kubadilishia nguo akiwa na jezi ya Manchester City baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 3-1.

Chanzo cha picha, Reuters
Sio yote kuhusu makusanyo ya ujenzi pia.
Kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Steve Hodge alijipatia £7.14m baada ya kuuza jezi ya Diego Maradona 'Hand of God' katika robo fainali ya Kombe la Dunia 1986 katika mnada mwaka 2022.
Wakati huohuo, jezi inayosemekana kuwa ya Phil Foden kutoka kwa England katika robo fainali ya Euro 2020 dhidi ya Ukraine, aliyopewa kipa Georgiy Bushchan, iliorodheshwa hivi majuzi kwenye mtandao wa eBay kwa pauni 2,999.
Mshambulizi wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Chris Sutton alisema kuhusu mkusanyiko wa jezi zake: "Watoto wangu wana baadhi yazo, lakini nina shati ninayoipenda zaidi, ambayo ni shati ya Henrik Larsson aliporudi Celtic akiwa na Barcelona.
"Sijawahi kupenda kubadilishana shati kama tungepoteza. Sikuwa mmoja wa wachezaji ambao wangemwomba mtu shati wakati wa mapumziko, pia.
"Kwa hivyo sikujisumbua sana kufanya hivyo, ingawa nimebadilisha mtazamo wangu sasa nimeacha kucheza.
"Ningetamani ningekuja zaidi kuhusu kufanya hivyo baada ya kuona jinsi Steve Hodge alivyovaa shati ya Diego Maradona lakini, kuwa makini, ni mambo mazuri kuwa nayo unapoangalia nyuma kwenye kazi yako."
imetafisiiwa na Seif Abdalla












