Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 26.10.2024

Erik ten Hag

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Uninted Erik ten Hag
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United wanafanya mazungumzo na wagombea wa ukocha kuchukua nafasi ya Erik ten Hag, Kevin de Bruyne anaweza kuondoka Manchester City na kujiunga na klabu ya MLC, na Eintracht Frankfurt yatangaza thamani ya Omar Marmoush anayenyatiwa na Liverpool.

Manchester United tayari wamefanya mazungumzo na makocha kadhaa miongoni mwao Xavi Hernandez na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon huku shinikizo la kumtimua Mholanzi Erik ten Hag, likizidi kuongezeka. (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 33, anaweza kuhamia San Diego FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Marekani, mkataba wa Mbelgiji huyo ukikamilika mwezi Juni mwakani. (GiveMeSport)

Eintracht Frankfurt wameweka thamani ya kati ya euro milioni 50-60 kwa mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush, 25, ambaye wawakilishi wake wamefanya mazungumzo na Liverpool. (Sky Germany)

 Kevin de Bruyne

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne

Arsenal wameandaa orodha fupi ya washambuliaji wanaolengwa na viwango vya kimataifa na mshambuliaji wa Newcastle na Uswidi Alexander Isak, 25, yuko juu kwenye orodha hiyo. (TeamTalk)

Beki wa Chelsea Ben Chilwell, 27, huenda akahamia West Ham huku Muingereza huyo akiendelea kutatizika kucheza chini ya Enzo Maresca. (Metro)

Inter Milan wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Athletic Bilbao Mhispania Oihan Sancet, 24, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Aston Villa. (Fichajes - kwa Kihispania)

Tottenham wana nia ya kumzuia beki wa Uhispania Pedro Porro, 25, kujiunga na Manchester City, ambao wanamuona kama mbadala wa beki wa Uingereza Kyle Walker, 34. (Football Insider)

Liverpool na Arsenal wanawania saini ya Mhispania na Barcelona Lamine Yamal, 17, kwani klabu hiyo ya La Liga inaweza kulazimika kumuuza mshambuliaji wao chipukizi kutokana na matatizo ya kifedha yanayoendelea. (Miguel Delaney via TeamTalk)

Winga wa Brazil Raphinha, 27, anasema alifikiria kuondoka Barcelona zaidi ya mara moja katika misimu yake miwili ya kwanza na klabu hiyo alipohama kutoka Leeds. (ESPN)

Liverpool wanapanga kumnunua mlinzi wa Celta Vigo Muhispania Oscar Mingueza, 25, kuchukua nafasi ya Muingereza Trent Alexander-Arnold, 26. (Fichajes - kwa Kihispania)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Chris Rigg, 17. (GiveMeSport)

Lamine Yamal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Liverpool na Arsenal wanawania saini ya Mhispania na Barcelona Lamine Yamal

Manchester United imeongeza juhudi za kumsaka mlinzi wa Bayern Munich Alphonso Davies kwa kukusanya taarifa kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa siku kadhaa. (Sky Germany)

Real Madrid na Chelsea pia wanavutiwa na Davies, ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao. (Express)

Manchester City wanamfuatilia mlinzi wa RB Leipzig Castello Lukeba, 21. Mfaransa huyo alisaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Bundesliga hivi majuzi. (Fichajes - kwa Kihispania)

AC Milan wameanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, kuhusu kuongeza mkataba wake. (Fabrizio Romano)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi