Mambo matano ya Ten Hag kuzingatia Man Utd

Aston Villa 0-0 Manchester United: Erik ten Hag 'amefurahi sana' baada ya sare tasa

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Phil McNulty
    • Nafasi, Chief football writer at Villa Park
  • Muda wa kusoma: Dakika 7

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag atajivunia hatua yoyote atakayopiga hata kama ni ndogo kiasi gani anapopambana kuwashawishi waajiri wake kwanini anapaswa kusalia Old Trafford kwa muda mrefu.

Mechi ya United huko Porto katika Ligi ya Europa na mechi ya ugenini dhidi ya Aston Villa katika wiki iliyopita, zilitarajiwa kutoa mwelekeo wakati wasimamizi wa United wakijiandaa kwa hatua itakayofuata.

United huenda haikushinda mchechi yoyote kati ya hizo - kupunguzwa kwa faida ya mabao mawili kwa sare ya 3-3 huko Porto kama kawaida ya machafuko ambayo yamesababisha muda mwingi wa Ten Hag - lakini sare ya kutofungana na Aston Villa angalau inamaanisha hakupoteza yoyote.

Mmiliki mwenza wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe alihudhuria Villa Park pamoja na Sir Dave Brailsford na wanachama wengine wa kundi jipya la watendaji wakuu wa United kama vile Dan Ashworth, Omar Berrada na Jason Wilcox. Sir Alex Ferguson pia alikuwepo..

Lakini Je, Ten Hag amefanya vya kutosha kudumisha imani inayoendelea kudidimia ya Ratcliffe na wenzake - na ni nini kitakachokuwa muhimu katika mashauri yao wiki hii?

Pia unaweza kusoma:

Je, sare na Villa ilionyesha dalili za kuimarika kiulinzi?

Uamuzi wa Ten Hag kurejea kwa wachezaji wawili wakongwe wa Jonny Evans na Harry Maguire mwenye umri wa miaka 36 ili kuzuia wimbi dhidi ya Aston Villa uliashiria mengi kuhusu mchangamoto ambayo imemkabili kuifanya United kuwa na mshikamano wa aina yoyote.

Mholanzi huyo alimwacha Matthijs de Ligt, usajili wake wa hivi majuzi wa pauni milioni 45 kutoka Bayern Munich, na Lisandro Martinez katika uamuzi ambao huenda haukufikia lengo la kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Tangu Ten Hag ateuliwe majira ya joto ya 2022, hakuna timu yoyote ya Ligi Kuu ambayo imekubali kufungwa mabao matatu au zaidi katika katika michuano yote mara nyingi zaidi ya jumla ya mabao 24 ya United. Na katika mechi 62 tangu kuanza kwa msimu uliopita, United wamefungwa mara mbili katika mechi 31. mara nyingi zaidi ya timu yoyote ya Ligi Kuu.

De Ligt aliingia uwanjani kipindi cha pili badala ya Maguire aliyeumia, lakini Ten Hag kushindwa kupanga safu ya ulinzi imekuwa kosa kubwa katika mkakati wake.

Ubora wa Evans ulitokana na uzoefu wake wa kudumu, lakini ni tafakari mbaya kwa wale walio karibu naye kwamba Ten Hag bado anatakiwa kutafuta huduma ya mchezaji ambaye alirejea Old Trafford kwa dharura msimu uliopita na kusalia kuwa kiungo muhimu.

Mshambulizi wa zamani wa Jamhuri ya Ireland Clinton Morrison aliiambia BBC Radio 5 Live: "Jonny Evans alikuwa mahiri. Alipata nafasi chache katika kipindi cha kwanza na alifanya vyema.

"Huenda asiwe na kasi lakini anachofanya Evans ni kusoma mchezo vizuri sana. Amekuja na kufanya kazi nzuri. Uamuzi mzuri wa Erik ten Hag."

Ikiwa anataka kusalia kama kocha wa Manchester United, Ten Hag atahitaji kuongeza juhudi zaidi.

Lakini mabao yanatoka wapi?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiwa mpango wa safu ya ulinzi ya Manchester United utachangia matatizo yanayowafanya wabaki nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England huku Ten Hag akipigania kibarua chake, basi safu ya ushambuliaji pia itaathirika.

United wamefunga mabao matano katika mechi saba za kwanza za Ligi ya Premia. Ni Southampton pekee ambao wanatajikokota, wakiwa na mabao manne, huku Crystal Palace nayo ikiwa na matano.

Kubaini hali ni mbaya kiasi gani lazima urejee 1972-73, wakati United walifunga mabao manne pekee kutoka kwa mechi saba za kwanza za ligi.

Jumla ya mabao yaliyotarajiwa kwa pamoja kati ya Villa na Manchester United katika mchezo wa jana yalikuwa 1.05 tu, idadi ya chini zaidi katika Ligi ya Premia msimu huu.

Rasmus Hojlund alirejea uwanjani Villa Park, lakini juhudi zake zote hazikufaulu na nafasi yake kuchukuliwa na Joshua Zirkzee baada ya saa moja.

Zirkzee ana bao moja pekee katika mechi 10, wakati Antony ana 12 kati ya 86 na Hojlund 17 anayeheshimika zaidi katika mechi 48 - lakini bado hana mafanikio.

Takwimu za jumla za malengo chini ya Ten Hag pia ni mbaya. Ana uwiano mbaya zaidi wa mabao kwa kila mchezo kuliko meneja wa kudumu wa Manchester United kuchukuliwa na Sir Alex Ferguson na kuendelea, akiwa na idadi ya mabao 1.45 kwa kila mchezo.

Ferguson anaongoza chati hiyo bila kustaajabisha akiwa na 2.01, huku David Moyes (1.65) na Jose Mourinho (1.62) wakifanikiwa kufikia wastani mzuri wa mabao kwa kila mchezo wakilinganishwa na Ten Hag.

Kwa hivyo unaweza kupuuza kiwango duni cha United?

Manchester United na Ten Hag wanaweza kufurahishwa na sare tasa uwanjani Villa lakini hatua hiyo haiwezi kuficha ukweli kwamba kikosi cha Ten Hag kinaendelea kutatizika.

United kutoshinda mechi ya jana kunamaanisha kuwa kiwango cha mchezo wao kiko chini zaidi baada ya mechi saba za Ligi Kuu.

Huu ni mwanzo wao mbaya zaidi tangu 1989-90, walipomaliza katika nafasi ya 13 katika Ligi Daraja la Kwanza, na kuona kwa wachezaji Ten Hag wenye thamani ya zaidi ya £300m wakianzia kwenye benchi kunatoa picha mbaya ya mkakati wa klabu hiyo kuwa na dosari kubwa ya kusajili wachezaji chini yake. .

Walifanya, angalau, kuonyesha mpangilio na kupigana na kukosa katika kipigo cha aibu cha 3-0 nyumbani kwa Tottenham Jumapili iliyopita na uimara wa safu ya ulinzi ambao ulitoweka baada ya kuanza vizuri huko Porto.

United sasa wamecheza mechi tano bila kushinda, mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano hii imetokea, na ingawa huu ulikuwa mchezo ulioboreshwa bado unawaacha na ushindi mara mbili pekee wa ligi hadi sasa msimu huu.

Hiki sicho ambacho Ratcliffe na wadakuzi wa United walikuwa nacho akilini wakati hatimaye waliamua kusimama na Ten Hag msimu huu wa joto, baada ya kutikisa nyavu zao lakini wakashindwa kupata mbadala mzuri.

United angalau walikuwa na sura na mwonekano wa kupanga, tofauti kubwa na Spurs na Porto, lakini bado hakuna ushahidi wa utambulisho wa wazi ambao Ten Hag anajaribu kuutengeneza.

Ratiba ya mechi baada ya mapumziko ya kimataifa inaanza na mchezo wa nyumbani dhidi ya Brentford kabla ya safari ya kucheza na Fenerbahce ya Jose Mourinho katika Ligi ya Europa, West Ham United ugenini, kisha Leicester City nyumbani.

Ikiwa Ten Hag atasalimika - na bado alionekana kujiamini baada ya sare hii dhidi ya Villa - matokeo chanya zaidi lazima yaje mara moja.

Je, mapumziko ya kimataifa ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko?

Mapumziko ya kimataifa mara nyingi yameleta wakati mwafaka wa mabadiliko ya usimamizi, lakini Ten Hag anatumai sare mbili zitaahirisha mpango kama huo miongoni mwa wale walio na uwezo wa kufanya hivyo Old Trafford.

Hali ya hatari ya Ten Hag ingekuwa kubwa zaidi kama mojawapo ya mechi mbili zilizopita, hususan dhidi ya Villa, ingeishia kuwa kichapo.

Mapumziko haya ya msimu yanatoa nafasi kwa United - na kwa hakika Ten Hag - kuchukua muda na kufanya tathmini, kuwapa nafasi ya kuchunguza chaguo zao.

Kabla ya mechi dhidi ya Villa, Ratcliffe aliiambia mhariri wa michezo wa BBC Dan Roan kuwa mustakabali Ten Hag "sio wito wangu", akisema uongozi ambao ameweka pamoja lazima "uchunguze na kufanya maamuzi ya busara".

Aliongeza: "Ni timu ya usimamizi inayoendesha Manchester United ambayo na ndio inapaswa kuamua jinsi tunavyoendesha vyema timu katika nyanja tofauti."

Nani mwingine anapatikana?

Hii ilikuwa tatizo la Manchester United katika majira ya joto kabla ya wapate ushindi wa kushtukiza dhidi ya Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA ulitosha kuendelea na Ten Hag.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alipigiwa upatu kuchukua usukani Old Traford baada ya kujiuzulu kufuatia Euro 2024, lakini pendekezo hilo halikuwavutia hisia za mashabiki wa Manchester United.

Thomas Tuchel alifanya mazungumzo na klabu hiyo majira ya joto baada ya kuondoka Bayern Munich lakini hakushawishika kuchukua nafasi hiyo. Mjerumani huyo ana sifa za kiwango cha juu, kama vile kushinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Chelsea.

Aliyekuwa kocha wa Brighton na Chelsea Graham Potter alikuwa na wasiwasi kuhusu kuhusishwa na United majira ya joto lakini ameweka wazi kuwa sasa yuko tayari kurejea kwenye uongozi baada ya kutimuliwa Aprili 2023 baada ya kuwa Stamford Bridge kwa miezi saba pekee .

Ruud van Nistelrooy alirejea Manchester United kujiunga na timu ya Ten Hag baada ya meneja huyo kuhakikishiwa nafasi yake majira ya joto. Je, angeweza kushikilia dau la United huku uongozi wake ukiendelea kutafuta mkufunzi wa kudumu?

Kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi anajivunia sifa ya kuwapeleka kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mnamo 2023 na anaendelea kufanya kazi nzuri huko San Siro.

Mkufunzi wa Ipswich Town Kieran McKenna anasifika sana tangu alipokuwa na wafanyakazi wa Ole Gunnar Solskjaer huko United lakini kazi yake, lakini juhudi zake Portman Road kuwapeleka Vijana wa Trekta kwenye Ligi ya Premia, bado ni mpango unaoendelea, kwa hivyo inaweza kuwa. mapema sana kwake kuchukuwa mikoba Man U.

Ten Hag anatumai kuwa juhudi zake za kuimarisha timu hata kama ni kidodo namna gani zilionekana katika siku saba zilizopita na zinaweza kuzima mjadala wa kumfukuza kazi.

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi