Uamuzi ambao 'haukutarajiwa' wa Papa Francis kumfukuza kwenye makazi yake Kardinali anayemkosoa

Chanzo cha picha, Getty Images
Papa Francis aliamua kumfukuza Kardinali wa Marekani Raymond Leo Burke, ambaye amekuwa akiukosoa waziwazi usimamizi wake, kutoka kwenye makazi yake mjini Vatican na kuondoa mshahara wake.
Burke ni sehemu ya kundi la wahafidhina wa Marekani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipinga mipango ya Papa ya kufanya mageuzi ndani ya Kanisa Katoliki.
Chanzo cha habari cha Vatican kimeiambia BBC kuwa Papa Francis bado hajafanya kazi ya kumfukuza kiongozi huyo wa kanisa mwenye umri wa miaka 75.
Aliongeza kuwa uamuzi huo haukusudiwi kama adhabu binafsi na unatokana na imani kwamba mtu hapaswi kufurahia marupurupu ya kardinali huku akimkosoa kiongozi wa Kanisa.
Uwe mfano mpya"

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, hatua hiyo "haikuwahi kutokea katika enzi za Francis," Christopher White, mwangalizi wa Vatican anayeandikia gazeti la National Catholic Reporter, aliiambia BBC.
"Kwa ujumla, makadinali wastaafu huendelea kuishi Roma baada ya kuondoka madarakani, na mara nyingi huendeleaa kuhudumu katika majukumu ya kawaida ya kikanisa," White alielezea.
Kwa maana hii, aliashiria kwamba "kumfukuza mtu kutoka kwenye nyumba yao huko Vatican kunaweka mfano mpya ."
White amebainisha kuwa uamuzi huo unaweza "kuchochea kuibua hisia kubwa za kumuunga mkono " na kuzidisha mgawanyiko kati ya Vatican na Kanisa la Marekani, ambako tayari kuna "mgawanyiko."
Kadinali Burke bado hajazungumzia suala hilo na BBC imewasiliana na ofisi yake kwa ajili ya kutoa maoni.
Papa Francis amefichua nia yake ya kuchukua hatua dhidi ya kardinali huyo katika mkutano na wakuu wa ofisi za Vatican wiki iliyopita.
Mvutano ndani ya Kanisa

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kukatishwa tamaa kwa Francis na wapinzani wake wa Marekani ambao wana mtazamo wa jadi au wa kihafidhina juu ya masuala mbalimbali inaonekana kufikia kilele.
Mapema mwezi huu alimfuta kazi Joseph Strickland, askofu wa kihafidhina wa Texas ambaye alikuwa amekosoa juhudi zake za kulisogeza Kanisa katika nafasi za maendeleo zaidi kuhusu utoaji mimba, haki za watu wa jinsia moja na ndoa za jinsia moja. Kufukuzwa kwa kanisa hilo kulikuja baada ya uchunguzi wa Kanisa kuhusu usimamizi wa jimbo katoliki.
Miezi michache kabla, Papa aliwaambia viongozi wa kidini wa shirika la Jesuit nchini Ureno kwamba kulikuwa na "mtazamo wenye nguvu, uliopangwa na wa kujibu" katika Kanisa la Marekani, ambalo alilielezea kama lililobaki "nyuma," kulingana na The Guardian.
Mvutano na Kardinali Burke, aliyeteuliwa na Papa Benedict XVI, umekuwa ukiongezeka kwa karibu muongo mmoja.
"Hali ya Burke ya Cardinal inaonekana kutokana na kujitenga kwake taratibu na Papa," White alitafsiri.
" Ni wazi Papa anaona kwamba Burke anaendeleza mawazo yanayozingatia mila au mawazo ya kizamani. Kitendo chake kinaonekana kuwa na lengo la kupunguza ushawishi wa Burke, akikata uhusiano wake na Roma.
Michael Matt, mwandishi wa makala wa gazeti la kihafidhina la Katoliki la The Remnant, aliandika kwamba hatua ya hivi karibuni dhidi ya Kardinali Burke inaonyesha kwamba Francis "anawachanganya watangulizi waaminifu ambao hutoa wanaunga mkono familia na wanaounga mkono misimamo mikali ya zamani kitamaduni ya Kanisa."
Alimshutumu Papa kwa kuwalazimisha wakosoaji wake "kutengwa kwa lazima."
Kardinali Burke ni nani?

Chanzo cha picha, Getty images
Raymond Leo Burke ni mmoja wa wapinzani wakubwa wa Papa ndani ya Kanisa Katoliki.
Mfuasi mkali wa miongozo ya Ukatoliki, Burke hata alimwambia waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry wakati alipokuwa mgombea wa urais kwamba hawezi kupata ushirika kwa sababu hapo awali alionyesha kuunga mkono utoaji mimba.
Kardinali amejitolea maisha yake mengi kujifunza sheria za Kanisa na anataka kuhakikisha kwamba zinatumika kwa dhati.
Anaamini Papa huyu anahatarissha utamaduni wa Kikristo wa miaka 2,000 na hata kutishia kutoa "kitendo cha marekebisho" dhidi ya Francis.
Hiyo itakuwa hatua ya ujasiri sana, isiyo ya kawaida, kitu ambacho hakijatokea katika karne nyingi.
Kardinali huyo anaishi katika nyumba kubwa karibu na uwanja wa St. Peter's mjini Roma.
Kutoka mahali hapo, ambapo Papa anataka kumfurusha, anaongoza operesheni yake ya kukuza kile anachokiita "ufafanuzi wa mafundisho . "
Wawili hao walitofautiana miaka sita iliyopita kuhusu kutimuliwa kwa kiongozi wa Knights of Malta, kusanyiko la kidini la karne ya 11, baada ya kugunduliwa kuwa tawi la shirika hilo la misaada lilikuwa limesambaza mipira ya kondomu nchini Myanmar.
Burke aliungana na wenzake wahafidhina katika chapisho la "kutangaza ukweli" mwaka 2019, ambalo lilielezea Kanisa Katoliki kuwa limepotoka na kuchanganyikiwa chini ya uongozi wa Papa Francis, akisema kuwa limepotoka na kutoka kwenye mafundisho ya msingi juu ya talaka, uzazi wa mpango, mapenzi ya jinsi moja na jinsia.
Zaidi ya hayo, hakukubaliana na hatua ya Papa Franciscis ya kupigia debe ya chanjo dhidi ya covid.
Hivi karibuni, mwezi uliopita, kardinali alifanya mkutano unaoitwa Sinodi Babel mjini Roma usiku wa synodi ya Papa - au mkutano wa maaskofu.
Papa amemshusha cheo Kardinali Burke ndani ya uongozi wa kanisa na kumhamishia katika nafasi zenye ushawishi mdogo kwa miaka mingi.
















