Nathaniel Becquart: Papa Francis amemteua mwanamke wa kwanza katika Sinodi ya Maaskofu

Baraza la maaskofu huchunguza masuala muhimu katika mafundisho ya kikatoliki

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Baraza la maaskofu huchunguza masuala muhimu katika mafundisho ya kikatoliki
Muda wa kusoma: Dakika 1

Kiongozi wa kanisa katoliki dunia Papa Francis amemchagua mwanamke wa kwanza kuwa katibu katika baraza la mkutano wa maaskofu.

Nathaniel Becquart , ambaye anatoka Ufaransa atakuwa na haki za kupiga kura katika baraza hilo ambalo hutoa ushauri kwa papa na kushiriki katika mijadala inayohusisha masuala tata katika kanisa hilo.

Bi Becquart amefanya kazi katika baraza la mikutano hiyo kama mshauri tangu 2019.

Katibu mkuu wa bodi hiyo , kadinali Mario Grech , alisema kwamba uteuzi huo umeonesha kwamba 'mlango umefunguliwa'.

Amesema kwamba uamuzi huo unaonesha lengo la Papa la kutaka wanawake wengi zaidi kushiriki mchakato wa utambuzi na maamuzi katika kanisa hilo.

Mwandishi wa BBC John McManus anasema kwamba hatua hiyo sio sababu ya kuwafanya wanawake kuwa makuhani, ijapokuwa wanaopinga wanasema kwamba ni hatua inayoelekea upande huo.

Luis Marin de San Martin , ambaye ni kuhani kutoka Uhispania pia aliteuliwa kuwa katibu katika baraza hilo linalompatia ushauri Papa.

Katika miaka ya hivi karibuni Sinodi ya Maaskofu imejadili mada za mafundisho ikiwemo jinsi ya kuwachukulia Wakatoliki waliotalakiana mbali na wale walioolewa.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

White space

Habari hii inakuja chini ya mwezi mmoja baada ya Papa Francis kubadilisha sheria katika Kanisa kuwaruhusu wanawake kuhudumu katika madhabahu ingawa amri hiyo ilisisitiza kwamba ukuhani utabaki wazi kwa wanaume pekee.

Mwaka jana, wakati huo huo, Papa huyo aliwateua wanawake sita kwa baraza linalosimamia fedha za Vatican.

2px presentational grey line