Tetesi za Soka Ulaya: Jackson asakwa Bayern, Isak haeleweki bado

Muda wa kusoma: Dakika 2

Bayern Munich wameulizia kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Senegal, Nicolas Jackson, 24, ambaye Chelsea wanataka pauni £48m ili kumuuza, anasakwa na Newcastle United. (Sky Sports Germany)

Mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak, hatacheza mechi za maandalizi ya msimu dhidi ya Espanyol na Atletico Madrid mwishoni mwa hii kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wake, anataka kwenda Liverpool. (Mail)

AC Milan wana nia ya kumchukua Rasmus Hojlund kutoka Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapatikana kwa takriban pauni £30m lakini Milan wanataka kumchukua kwa mkopo. (Gazzetta dello Sport)

Tottenham wamekataliwa ofa ya pauni £30m kwa ajili ya kumsajili Nico Paz na Como, ambao thamani ya kiungo mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye miaka 20 ni pauni £52m. (Sky Sports Italia)

Aston Villa wamekataa ofa ya pauni £18m kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wa Scotland, John McGinn, 30, ambaye pia anaivutia klabu ya Newcastle. (Sky Sports News)

Klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia wako tayari kutoa kitita kinachohitajika na Brentford kwa ajili ya mshambuliaji wa DR Congo mwenye miaka 28, Yoane Wissa, ambaye pia anasakwa na Newcastle na Tottenham. (L'Equipe - in French)

Beki wa Hispania, Inigo Martinez, 34, anatarajiwa kuvunja mkataba wake na Barcelona na kuhamia Al-Nassr bila malipo. (Mundo Deportivo)

Manchester City wamekataa ofa kutoka Roma kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Argentina, Claudio Echeverri, 19, kwani wanataka kumpeleka kwa mkopo Girona, ambao wapo chini ya umiliki wa City Football Group. (Calciomercato)

Preston North End wako karibu kukamilisha uhamisho wa mkopo wa kiungo mshambuliaji wa Uingereza wa Tottenham, Alfie Devine, 21. (Lancashire Post)

Coventry City wanataka pauni £15m kwa ajili ya beki wao wa kulia kutoka Uholanzi, Milan van Ewijk. Wolves na Wolfsburg ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia mchezaji huyo mwenye miaka 24. (Coventry Telegraph)