Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Manchester City mbioni kumsajili Guehi

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City inajiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili mlinzi wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 25, kabla ya uhamisho wa Januari wa wachezaji kukamilika, lakini huenda wasifikie bei ya zaidi ya pauni milioni 35 inayotakiwa na Palace. (Talksport)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl amekuwa akipiga simu katika siku za hivi karibuni kujaribu kumshawishi Guehi ajiunge nao msimu wa joto. (Sky Germany)

Licha ya kutimuliwa kwa kocha mkuu Ruben Amorim, Manchester United haina mpango wa kumrejesha mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, wakati usajili wake wa mkopo katika Barcelona utakapokamilika. (Talksport)

Mshambuliaji wa Manchester United na England aliye na umri wa chini ya miaka 20 Ethan Wheatley, 19, atajiunga na Bradford City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Manchester Evening News)

Nottingham Forest inamuulizia winga wa Bournemouth Muingereza Marcus Tavernier, 26, lakini Cherries hawana mpango wa kumuuza. (Daily Mail)

Tottenham Hotspur haia nia ya kumuuza mshambuliaji Mfaransa Mathys Tel, 20, licha ya Paris FC kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Florian Plettenberg)

Klabu ya Bournemouth inaendelea kujadiliana na Ferencvaros kuhusu dili la kiungo wa Hungary Alex Toth, 20, baada ya ofa yao ya awali ya pauni milioni 8.6 kukataliwa. (Sky Sports)

Newcastle inafikiria kumsajili mlinzi mwezi huu baada ya beki wa pembeni wa Uingereza Tino Livramento, 23, kupata jeraha la misuli ya paja ambalo litamweka nje ya uwanja kwa wiki nane. (Sky Sports)

Manchester City, Brentford na Tottenham huenda wakamkosa winga wa Nigeria aliye na umri wa chini ya miaka 20 Suleiman Sani, 19, huku RB Leipzig ikikamilisha mkataba wa £4.5m na Trencin ya Slovakia. (Daily Mail)

Liverpool haitamtoa mlinzi wa Uingereza Joe Gomez, 28, mwezi huu baada ya beki wa Ireland Kaskazini Conor Bradley, 22, kupata jeraha la goti. (Football Insider)

Meneja wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp ni miongoni mwa makocha wanaongoza orodha ya Real Madrid kurithi mikoba ya Xabi Alonso, huku Antonio Conte na Enzo Maresca pia wakizingatiwa. (Fichajes - kwa Kihispania)

Arsenal haina nia ya kumtoa mlinzi wa Uingereza Ben White, 28, licha ya mchezaji huyo kukosa muda wa kucheza mchezo na kutakiwa na vilabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Everton na Manchester City. (Team talk)