Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Man United yawasliana na Brighton kuhusu Baleba
Manchester United imewasiliana na Brighton kupitia waamuzi kutafuta uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba, 21. (Athletic - Subscription Required).
Everton wameanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa England Jack Grealish, 29, kutoka Manchester City. (Sky Sports)
Mshambulizi wa Uswidi Alexander Isak ameambiwa afanye mazoezi peke yake katika klabu ya Newcastle United huku Liverpool ikitaka kumsajili hatua ambayo ilimfanya mchezaji huyo kukosa siku ya familia kwa wachezaji ambayo iliwekwa na klabu hiyo. (Mirror)
Newcastle wametoa ofa ya takriban euro 30m (£26.2m) kwa mlinzi wa Ujerumani Malick Thiaw lakini AC Milan hawajakubali ofa hiyo kwa vile wanataka kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Gazzetta dello Sport - In Itali)
Nottingham Forest inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 27, kutoka Juventus, ambapo inaweza kumnunua kiungo wa kati wa Forest na Ivory Coast Ibrahim Sangare, 27. (Gazzetta dello Sport - in Italian), .Everton pia wanavutiwa na Douglas Luiz na iwapo, wanaweza kuangalia mkopo kama chaguo au wajibu wa kumnunua. (Mail)
RB Leipzig inajadili suala la mkataba na kiungo wa kati wa Liverpool na England chini ya umri wa miaka 21 Harvey Elliott, 22, kabla ya kutoa ofa rasmi ya uhamisho. (Fabrizio Romano)
Inter Milan wanaweza kufikiria kumnunua winga wa Manchester United na England Jadon Sancho, 25, ikiwa watashindwa kumsajili fowadi wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta. (Gazzetta dello Sport - In Italy)
Mchezaji wa Manchester City Mateo Kovacic, 31, amefuatiliwa na klabu za Saudi Pro League msimu huu, lakini kiungo huyo wa kati wa Croatia anataka kusalia. (Fabrizio Romano)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla