Tetesi za Soka Jumatano: Newcastle na Man Utd wanapanga kumsajili Jackson

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United na Newcastle zote zinamtazama mshambuliaji wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24, kama mchezaji mpadala iwapo watamkosa mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Slovenia, Benjamin Sesko, 22. (The Athletic)

Aston Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Manchester United ya Uingereza Ollie Watkins, 29, iwapo Mashetani Wekundu watashindwa kukamilisha dili la kumnunua Sesko. (Teamtalk)

RB Leipzig wamewasiliana na Liverpool kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Harvey Elliott, 22, huku Reds wakitaka pauni milioni 40 pamoja na chaguo la kumnunua tena, au zaidi ya pauni milioni 50 bila ya chaguo la kuweza kumnunua tena. (The Athletic)

Manchester United imekataa ofa tano kutoka vilabu vya Ligi Kuu England (Ligi ya Premia) na Italia kwa ajili ya beki wa Uingereza Harry Maguire, 32. (Mail)

Juventus wako tayari kumuuza beki wa kati wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, na kumsajili mlinzi wa Arsenal Jakub Kiwior, 25, kama mbadala wake. (Gazzetta dello Sport)

Sunderland wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Everton Dominic Calvert-Lewin kwa uhamisho wa bure, ingawa Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kusubiri kuona kama kuna klabu nyingine za Ligi ya Premia zinavutiwa naye. Talksport

West Ham bado wanavutiwa na mchezaji wa Aston Villa, Jacob Ramsey, 24, huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza akiwa bado hajafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake wa baadaye (Mail)

Liverpool imekuwa ikitafuta mabeki wa kati vijana barani Ulaya akiwemo Mtaliano wa timu ya Parma, Giovanni Leoni, 18. (Times)

Newcastle wanatazamiwa kuwasiliana na AC Milan kumnunua beki wa Ujerumani Malick Thiaw, 23. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest itafanya mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Juventus na Brazil, Douglas Luiz kujaribu kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Italia)

Kiungo wa kati wa RB Salzburg na Denmark, Mads Bidstrup, 24, anaongoza orodha fupi ya wachezaji wanaolengwa na Nottingham Forest. (Florian Plettenberg)

Beki wa kushoto wa zamani wa Manchester United, Brandon Williams, 24, anasakwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Championship, ikiwa ni pamoja na Hull City, licha ya kuwa bila klabu kwa miezi 12. (Mail)

Derby County wanakaribia kumsajili kiungo wa zamani wa Liverpool, Bobby Clark huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 20 akitarajiwa kujiunga na Rams kwa mkopo wa msimu mzima kutoka RB Salzburg. (Sky Sports)

Tottenham wanataka kuongeza safu yao ya ushambuliaji na kuwa na mshambuliaji wa AC Milan na Ureno, Rafael Leao, 26, na winga wa Real Madrid na Brazil, Rodrygo, 24, miongoni mwa malengo yao. (GiveSport)