Matokeo ya uchaguzi Uganda 2026

Muda wa kusoma: Dakika 2

Shughuli za kuhesabu kura zimeanza katika baadhi ya maeneo ya Uganda licha ya mtandao wa intaneti kuzimwa na upinzani kudai uchaguzi wa rais na wabunge ulikumbwa na visa vya udanganyifu.

"Matukio ya masanduku kujazwa kura yameripotiwa kila mahali," alidai mgombea wa urais wa chama cha upinzani cha NUP Ssentamu Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii, bila kutoa uthibitisho madai hayo.

Mamlaka inayosimamia uchaguzi huo haijatoa kauli yoyote kuhusu madai ya udanganyifu katika uchaguzi, wala madai ya Bobi Wine kwamba mawakala "wengi" wa wapiga kura na wasimamizi wa chama chake cha NUP "walitekwa nyara, na wengine kufukuzwa katika vituo vya kupigia kura".

Hapo Jana tarehe 15 .01.2027 changamoto za kiufundi zilichelewesha shughuli ya upigaji kura .

Kwa matokeo zaidi ya uchaguzi Uganda Bonyeza hapa