Wagner, Prigozhin, Putin na Shoigu: Uhasama uliosababisha uasi

.

Chanzo cha picha, Press Service of Concord

Maelezo ya picha, Uasi mfupi wa Yevgeny Prigozhin ulichochewa sana na mashindano ya kibinafsi kama tofauti zozote za kisiasa na Kremlin.

Hatimaye uwasi wa Wagner umedumu chini ya masaa 24. Lakini visa vya uadui, wivu na malengo yaliyochangia uasi huo vimekuwepo kwa miezi, ikiwa siyo kwa miaka.

Wahusika wakuu wa tukio zima ni Yevgeny Prigozhin, mwasisi na kiongozi wanamgambo wa kundi la Wagner na wakuu wa Jeshi la Urusi, Sergei Shoigu na Valery Gerasimov.

Prigozhin - mhalifu wa zamani anaehusishwa na matukio ya uhalifu wa kupangwa mnamo miaka ya 1980, ambapo alitumikia miaka kadhaa gerezani - ametengenezwa na Kremlin na utajiri wake.

Tangu kuundwa kwa Wagner mwaka 2014, amekuwa kiungo muhimu Kwa matakwa ya Rais Putin kueneza ushawishi wa Urusi ulimwenguni. Kundi lake linaundwa na vikosi vya wanajeshi wa zamani wa Urusi. Vimefanikiwa kumlinda rafiki wa Putin, rais Bashar Al Asad wa Syria na kuondosha ushawishi wa Ufaransa nchini Mali.

Hadi mwaka jana Prigozhin amekuwa akiukana mara kwa mara ushahidi wa kwamba anamiliki kundi Hilo, na alifungua kesi nchini Uingereza dhidi ya mwandishi habari, Elliot Higgins ambaye alumtuhumu kuendesha kundi la kijeshi.

Mwanaume mwenye faraja na vurugu, rushwa na malengo kukuwa kwake ni nembo katika taifa la sasa lililojengwa na Rais Putin kwa takribani miaka 24.

Licha ya nguvu zake kukuwa amebaki kuwa mtu wa nje miongoni mwa wa washauri wa karibu wa Putin, haogopi kuwakosoa maafisa wa Mascow na anawaona ni wala rushwa na wavivu.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sergei Shoigu na Valery Gerasimov wameendesha jeshi kubwa la Urusi pamoja kwa zaidi ya muongo mmoja.

Maadui zake

Si kama washauri wengi muhimu wa Putin, waliozaliwa katika jiji alilokulia rais St Petersburg, bwana Shoigu alizaliwa katika kijiji kidogo katika mpaka wa Urusi na Mongolia. Licha ya kuongoza kundi hilo, Shoigu hajawahi kuwa mwanajeshi. Alitokea katika nyadhifa za chama cha kikomunist kabla ya kuwa mkuu wa wizara ya dharura ya Urusi miaka ya 1990.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bwana Gerasimov, mtu watatu katika sakata hili ni mwanajeshi. Alikomesha uasi huko Chechnya miaka ya 1990, na ndiye mkuu wa majeshi wa muda mrefu tangu kudondoka kwa Usovieti.

Baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na hasa baada ya umwagaji damu katika mapigano ya Bakhmut, vita ambavyo maelfu ya wapiganaji wa Wagner wanaaminika waliuwawa. Chuki za Prigozhin Kwa wakuu wa Jeshi zikaongezeka.

Mara Kwa mara akimtuhumu bwana Shoigu na bwana Gerasimov kwamba wanajaribu kuiba ushindi wa Wagner katika jiji kama Soledar, ambako maelfu ya wapiganaji wa kundi hasa wale walioandikishwa kutoka magerezanu, waliuawa.

Lakini bwana Putin aliacha ushindani na uadui huo uendelee.

Profesa wa sayansi ya siasa wa chuo kikuu cha California, Los Angeles, Daniel Triestman, aliandika mwaka jana, "mfumo ulioundwa na Putin upo kuzuia mapinduzi, maafisa wenye dhamana ya kuongoza vikosi wanakosa kuaminiana kuandaa njama ya mapinduzi."

Katika utawala huu bwana Shoigu anaangaliwa na Wagner, wakati Wagner wakiangaliwa na Jeshi. Juu ya piramidi yupo Putin, mkuu wa sataranji (chesi), akiendesha vipande juu ya ubao na akidhibiti mfumo.

Daima Prigozhin amekuwa mwangalifu kuto mkosoa rais Putin moja kwa moja, na badala yake husema kufeli kwa Urusi tangu uvamizi kunatokana na kupotoshwa Putin na makamanda wake.

Kwa Putin ilikuwa na maana kwa mkuu wa Wagner kushindwa kampeni ya kijeshi. Za chini ya kapeti zinasemq Putin amewakosoa Shoigu na Gerasimov.

Katika video Moja akiwa na makumi ya miili ya wapiganaji wa Wagner, alisema, "Nyinyi musiotupa silaha, mutakula nyama zao ahera. Shoigu! Gerasimov! Silaha ziko wapi? Alifoka Prigozhin.

Kwa mujibu wa ripoti ya taarifa za kitelejinsia ya Marekani, Prigozhin aliitwa katika mkutano na Putin na Shoigu Februari 22 - siku hiyo hiyo aliyochapisha video akizungukwa na miili ya wanajeshi wa Wagner waliokufa. Ingawa mkutano huo waonekana haukuzaa matunda.

Juni 10 bwana Shoigu akiweka wazi mpango wake, wanajeshi wa kujitolea wataumbwa wasaini mkataba na wizara ya ulinzi na kuwajumuisha katika Jeshi la nchi. Ingawa tangazo hili halikuita Wagner, ila lilitafsiriwa kuwa linalenga kupunguza nguvu za Prigozhin.

Na likapelekea kuamsha hasira za mkuu huyo. "Wagner haitosaini mkataba wowote na Shoigu. Hana uwezo wako wa kusimamia shughuli za kijeshi."

Baada ya miezi ya ukosoaji na kufoka operesheni ya kijeshi. Rais Putin hayimaye ameamua kuunga mkono wakuu wa kijeshi na kumweka kando rafiki yake wa zamani.

Taasisi ya kintelejinsia ya Marekani ya Study of War (ISW) inasema, alicheza kamari ya kutaka kulifanya Wagner kama kundi huru, ni kufanya mkusanyiko dhidi ya wizara ta kijeshi ya Urusi.

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maswali yataulizwa kuhusu urahisi ambao askari wa Wagner walipitia Kirusi na kuchukua tovuti muhimu

Punde kampeni yao ikaongezeka dhidi ya Jeshi la wakamteka kamanda wa Urusi, wakimtuhumu kushambulia vikosi vya Wagner. Chombo cha habari Marekani, maafisa wa intelejinsia walichambua mwenendo wa Wagner Kwa siku kadhaa, na wakamtaarifu Rais Biden kwamba Prigozhin alipanga jambo.

Baadhi wanashuku Prigozhin alikubali kumializa uasi baada ya makubaliano na Rais Putin, ikiwemo kubadilisha wakuu wa wizara ya ulinzi. Ikiwa hili ni la kweli bado haiko wazi.

Utiifu wa makundi ya wapiganaji ya upande wa Urusi, kwa sasa unatia shaka na inaweza kudhoofisha dhana kwamba serikali ya Putin Ina uwezo wa kuendesha vita kwa muda mrefu kuliko uwezo wa serikali ya Kyiv.

"Matumaini kwamba wakuu wa Urusi, akiwemo rais mwenyewe kwamba vita vya muda mrefu ni faida Kwa Urusi ni mawazo ya hatari. "Kuendeleza vita kunabeba hatari kubwa Kwa siasa za ndani za Urusi," anasema mchambuzi wa kituo cha uchambuzi wa mikakati na teknolojia, kilichopo Urusi, bwana Ruslan Pukhov.