Kwa nini Niger inaipungia mkono Ufaransa na sio Marekani

''

Chanzo cha picha, AFP

    • Author, Paul Melly
    • Nafasi, Mchambuzi Afrika

Chini ya miezi mitano baada ya Rais wa Niger Mohamed Bazoum kuondolewa madarakani kwa mapinduzi, koloni la zamani la nchi hiyo Ufaransa, inawaondoa wanajeshi wa mwisho waliosalia iliowatuma katika taifa hilo la Afrika Magharibi kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali wanaotishia utulivu katika eneo lote.

Uhusiano na Paris umezoroteka kabisa - balozi wa Ufaransa Sylvain Itté aliondoka mwezi Septemba kufuatia shikizo la utawala wa kijeshi - wakati Umoja wa Ulaya (EU) pia umepuuzwa.

Utawala wa kijeshi, unaongozwa na Jenerali Abdourahmane Tchiani, imefuta kwa upande mmoja makubaliano ambayo wataalamu wa Umoja wa Ulaya kwa miaka mingi wametoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Niger.

Bw Bazoum aliiona Ufaransa kama mshirika muhimu wa kijeshi. Wakati wanajeshi wa Ufaransa na vikosi vingine maalum vya Uropa vilipoondoka Mali mnamo 2022, aliwataka kupeleka tena katika maeneo dhaifu ya mpaka wa magharibi wa Niger yaliyokumbwa na mashambulio ya wanamgambo wa kijihadi, ambapo walifanya kazi chini ya amri ya Niger.

Lakini baada ya Rais Emmanuel Macron kulaani mapinduzi ya Julai 26 na uungaji mkono wake wa umma kwa Bazoum, ambaye bado anazuiliwa katika makazi yake ya rais, watawala wapya wa kijeshi wa Niger waliamua kufanya mabadiliko makubwa ya sera, na kuwataka Wafaransa kujiondoa.

Wengi wa wanajeshi 1,500 wameondoka na 157 waliosalia wataondoka ifikapo Jumamosi.

Utawala wa kijeshi umechagua kutegemea muungano mpya wa ulinzi na nchi jirani za Burkina Faso na Mali. Nchi hizi mbili pia ziko chini ya utawala wa kijeshi na zinapinga matakwa, ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi Ecowas, ya kurejesha utawala wa kidemokrasia inayoongozwa na kiraia haraka.

Hata hivyo wakati Ufaransa na EU ziko katika hali ya utulivu, huku Paris ikilaumiwa kwa migogoro ya kila aina na hata kushutumiwa kuunga mkono uasi wa 2007 wa waasi wa Tuareg waliojitenga, Marekani inasalia na uwepo mkubwa, ikituma balozi mpya mjini Niamey mwezi Agosti.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Na utawala wa kijeshi haujataka kufungwa kwa kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Niger, ambapo zaidi ya wanajeshi 600 wa Marekani wamesalia. Haya ni muhimu kwa Washington kwani mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wako karibu tu na mpaka wa Mali ili kusaidia utawala wa kijeshi katika eneo hilo na kupambana na wanamgambo wa kijihadi.

Hakuna shaka kwamba Ufaransa, na Bw Macron binafsi, ndio chanzo cha chuki kubwa dhidi ya Ufaransa miongoni mwa vijana wa mijini kote Afrika Magharibi, na sio tu mataifa yaliyo katika ukanda wa Sahel kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akiwa anachukuliwa kuwa mtu wa hali ya juu na mwenye uthubutu kupita kiasi, anachukizwa kwa kiwango ambacho si kweli kwa wakuu wa zamani wa Ufaransa, hata Nicolas Sarkozy, ambaye alikuwa na uchungu wa kuwaambia wasikilizaji wa Senegal kwamba Afrika haijaingia vya kutosha katika historia.

Kipaumbele ambacho Bw Macron ametoa kwa Afrika Magharibi, iwe ni katika juhudi za kijeshi za kupambana na makundi ya wanamgambo wa kijihadi, kurejesha hazina za kitamaduni zilizoporwa au bajeti ya maendeleo iliyopanuliwa kwa njia ya kuvutia, imelemazwa.

Ushawishi wa Ufaransa katika Afrika Magharibi umepungua tangu kutokea kwa mapinduzi katika makoloni yake ya zamani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ushawishi wa Ufaransa katika kanda ya Afrika Magharibi umepungua tangu kutokea kwa mapinduzi katika makoloni yake ya zamani

Wanajeshi ambao wamenyakua mamlaka nchini Niger, Burkina Faso na Mali katika kipindi cha miaka mitatu wametumia karata ya chuki dhidi ya Ufaransa ili kujiongezea umaarufu.

Wakati nchi zao zinavyohisi shinikizo la kuongezeka kwa kutengwa kiuchumi, na kupungua kwa usaidizi wa maendeleo na usalama, ukoloni wa zamani umekuwa chambo cha kujitetea.

Paris, na hata Brussels, poa wamegharamia msaada wao mkubwa kwa Ecowas.

Itifaki ya demokrasia na utawala bora wa umoja huo wa mwaka 2001 ndiyo msingi wa msimamo wake usiobadilika dhidi ya viongozi wa mapinduzi na juhudi zake za kuwashinikiza kuchukua hatua za kurejesha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia, huku Niger ikikabiliwa na vikwazo vya kibiashara na tishio la kuingilia kijeshi.

Hata hivyo Ecowas yenyewe haipendelewi na wengi, mara nyingi inaonyeshwa kama klabu ya marais ambayo imefumbia macho wizi wa uchaguzi na ukiukaji wa katiba huku wakuu wa nchi wakitaka kuongeza muda wa kusalia madarakani.

Katika muktadha huu mseto, ambapo Jenerali Tchiani na wenzake wa Mali na Burkina faso, Kanali Assimi Goïta na Kapteni Ibrahim Traoré, wanaingia kwenye chuki kali ya utaifa, Marekani imetumia furasa hiyo kuingiza guu katika eneo hilo.

Ilisubiri kwa wiki kadhaa kabla ya hatimaye kukubali kupinduliwa kwa serikali iliyochaguliwa ya Niger, ambayo moja kwa moja, chini ya sheria za Marekani, ilisababisha kusimamishwa kwa misaada mingi ya kimaendeleo.

Ikiwa na taswira nzuri au isiyoegemea upande wowote katika Afrika Magharibi, ambapo haina historia ya ukoloni na Vita Baridi haikuacha urithi wa migogoro, Washington imeweza kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia na tawala za kijeshi kwa njia ambayo Paris isingeweza kufanya bila kufedheheka kwa kukataliwa kwa sera zake za msingi na rekodi ya utendaji.

Viongozi wa mapinduzi wamekuwa tayari kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na kuwasikia wakitoa kauli za umma ambazo sio za kuridhisha.

Katika mji mkuu wa Niamey wa Niger wiki iliyopita, Katibu Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika Molly Phee alitoa wito kwa mamlaka ya kijeshi kurejelea mazungumzo na Ecowas baada ya Umoja huo kutoa msamaha wa vikwazo ili kurudisha maendeleo ya wazi ya kurejea kwa utawala wa kikatiba - na alitoa fursa ya kuwatia motisha endapo hatua hiyo itazingatiwa.

Baada ya mapinduzi hayo Marekani ilisitisha ushirikiano wake wa kijeshi na vikosi vya usalama vya Niger, lakini Bibi Phee alisema Washington ina nia ya kurejesha ushirikiano na usaidizi wa kimaendeleo "kwa awamu", na kutathmini upya hatua zilizochukuliwa na utawala wa kijeshi kuelekea kurejesha demokrasia.

Marekani imetoa mafunzo kwa wanajeshi wa mataifa ya Burkina Faso, Niger, Mali, ambayo yako chini ya utawala wa kijeshi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani imetoa mafunzo kwa wanajeshi wa mataifa ya Burkina Faso, Niger, Mali, ambayo yako chini ya utawala wa kijeshi

Kando na mipango ya muda mrefu ya mafunzo na vikosi vya Niger, Marekani ina vituo vya ndege vya Niamey na Agadez kwenye ukingo wa Sahara, ambayo inachukulia kuwa muhimu kwa ufuatiliaji wa shughuli za vikundi vya jihadi katika kanda hiyo na mamluki wa Wagner nchini Mali na Libya. .

Kwa hivyo utawala wa Jenerali Tchiani unahisi kuwa katika nafasi nzuri ya kujadiliana. Akitoa sauti ya uthubutu, Waziri Mkuu Mahaman Lamine Zeine alisema Jumatano: "Ikiwa Wamarekani wanataka kubaki hapa na majeshi yao wanapaswa kutuambia wanachotaka kufanya."

Bw Zeine hakuchelea kudokeza kuwa Niger ina washirika na marafiki mbadala ikiwa Marekani haitatoa ushirikiano. Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Jenerali Yunus-Bek Evkurov alizuru Niamey mapema mwezi huu.

Zaidi ya hayo, Sahel inaweza kuwa uwanja wa majaribio wa kipaumbele kwa kuunganishwa tena kwa vikosi vya Wagner katika muundo wa kawaida chini ya udhibiti mkali na uanzishwaji rasmi wa ulinzi wa Urusi. Mtindo huo wa kihafihina unaweza kuwa na mvuto kwa Niger, ambayo ina utaratibu dhabiti za kijeshi.

Moscow pia inajaribu kupanua "toleo" lake kwa mataifa ya Sahel hasa katika nyanja ya usalama, ingawa haijatayarishwa kuendana na mchango wa wafadhili wa kimaendeleo wa EU, Marekani, Ujerumani au Ufaransa.

Niger, ambayo ina raia wapatao milioni 24.5, ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Niger, ambayo ina raia wapatao milioni 24.5, ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani

Mwezi uliopita ilituma kundi la madaktari kusaidia Burkina Faso kukabiliana na milipuko ya homa ya dengue na chikungunya.

Kwa hivyo Washington inajua inafanya kazi katika mazingira ya kidiplomasia yenye ushindani.

Huenda ikawa imechukua mkondo wa kidiplomasia wa umma kuliko Paris, lakini haitaepukana na mizozo mibaya na chaguzi ngumu katika kushughulikia tawala za kijeshi ambazo kwa sasa hazihisi kuwa lazima ziangalie Magharibi au hata, katika hali zingine, Umoja wa Mataifa. .

Hata hivyo, watawala wa kijeshi wa Niger pia wanakabiliwa na matatizo yasiyo ya kawaida. Ingawa maasi kutoka Urusi na matamko ya mshikamano kutoka Burkina Faso na Mali yanatoa kiwango fulani cha faraja ya kisiasa, hali halisi ya kibinadamu na usalama ni mbaya.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi