Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 14.03.2023

Jude Bellingham

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwakilishi wa Real Madrid hivi majuzi alizuru Ujerumani kukutana na Jude Bellingham na familia yake baada ya kumfanya kiungo wa kati wa Borussia Dortmund wa Uingereza, 19, kuwa shabaha yao ya kwanza msimu ujao wa joto. (AS - kwa Kihispania)

Real Madrid wako tayari kulipa Dortmund euro milioni 100 (£88m) kumpata Bellingham, pamoja na nyongeza ya 40m (£35m). (Sport1, via Sport - kwa Kihispania)

Manchester United haitahatarisha kumsaka kwa muda mrefu mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29, msimu wa joto, kwa matarajio ya kukabiliana na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ikimaanisha kwamba wanaangazia wachezaji mbadala, akiwemo mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, na. Mshambulizi wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 23. (ESPN)

Harry Kane

Chanzo cha picha, Reuters

Christopher Nkunku atakuwa mchezaji wa Chelsea msimu ujao baada ya The Blues kufikia makubaliano kamili na RB Leipzig kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 25. (Football Insider)

Tottenham wana nia ya kumnunua Emiliano Martinez wa Aston Villa na wanaweza kuwasilisha ofa kwa mlinda mlango huyo wa Argentina, 30, wiki zijazo. (TyC Sports, kupitia Goal)

Rais wa La Liga Javier Tebas anasema anataka kumuona mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 24, akiichezea Real Madrid. (Sport - kwa Kihispania)

Christopher Nkunku

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Christopher Nkunku atakuwa mchezaji wa Chelsea msimu ujao

Mshambulizi wa Brazil Neymar, 31, hatarajii kuondoka PSG kwa vile anataka kumaliza soka yake na klabu hiyo ya Ufaransa. (Athletic)

Manchester United wanaweza kufanya uhamisho mwingine msimu huu wa joto kwa mmoja wa walengwa wao wa muda mrefu, beki wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 26. (Football Insider)

Man United pia wanapanga kumwacha winga wa Uruguay Facundo Pellistri, 21, kwenda nje kwa mkopo msimu ujao. (Evening sports Manchester)

Neymar

Chanzo cha picha, Reuters

Kiungo wa kati wa zamani wa Ujerumani Toni Kroos, 33, ameamua kusalia Real Madrid kwa walau msimu mmoja. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Wiga wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 30- Wilfried Zaha, ambaye kandarasi yake katika klabu ya Crystal Palace inamalizika msimu huu wa joto, amepewa ofa ya pauni milioni 9 kwa msimu na klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia . (Mail)

West Ham wakotayari kumenyana na RB Leipzig na Atletico Madrid kupata saini ya kiungo wa kati wa Norwich City Mbrazil Gabriel Sara, 23, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Zaha

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham pia wanaongoza katika mbio za kumsaka beki wa Bournemouth wa Zimbabwe Jordan Zemura, 23, ambaye alitemwa wikendi kutokana na hali yake ya kandarasi. (Dakika 90)

Borussia Dortmund wameamua kumuuza beki wa Ubelgiji Thomas Meunier msimu huu wa joto, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuwa na mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Kocha wa Fulham Marco Silva anaibuka mshindani mkuu kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama kocha wa Tottenham. (Sun)

Marco Silva

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Kocha wa Fulham Marco Silva anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama kocha wa Tottenham

Mshambulizi wa zamani wa Real Madrid, Raul, ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya akiba ya klabu hiyo, amejidhihirisha kuwa ni mshindani mkubwa kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti kama kocha wa kikosi cha kwanza wakati mkataba wa sasa wa Muitaliano huyo utakapomalizika 2024. (AS - kwa Kihispania).

Wachezaji wote katika kikosi cha West Ham wanakabiliwa na 'punguzo kubwa la mishahara' ikiwa klabu hiyo itashushwa daraja kutoka kwa Ligi Kuu msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)