Ni nini husababisha mtu kuwa mrefu au kuwa mfupi?
Na Philippa Roxby,
Mwandishi wa BBC wa Masuala ya Afya

Chanzo cha picha, FIB TV
Je! unajua kwamba mtu wa kale au Neanderthal kwa wastani wastani alikuwa na urefu wa sm165? Tangu kuzaliwa kwa mwanadamu, urefu wake umeongezeka kwa sentimita 10. Urefu wa wastani wa wanaume nchini Uingereza ni sm178 , kwa wanawake - sm 164 .
Kitendawili cha kwa nini wanadamu wanakua warefu na kufikia kipindi cha balehe mapema zaidi kuliko hapo awali kinaweza kuelezewa na king;amuzi katika ubongo, wanasayansi wanasema.
Wastani wa urefu nchini Uingereza uliongezeka kwa 3.9in (10sm) wakati wa Karne ya 20, na hadi inchi 7.8 katika nchi nyingine, wakati afya ya lishe ilipoimarika.
Lakini jinsi hali hii inavyotokea haijawahi kueleweka.
Nchini Korea Kusini , kwa mfano, urefu wa watu wazima umeongezeka huku taifa likibadilika kutoka nchi maskini hadi kuwa jamii iliyoendelea. Katika sehemu za Asia Kusini na Afrika, watu wameongezeka urefu kidogo tu kuliko miaka 100 iliyopita.
Nchini Marekani, urefu wa wanaume ni sentimita 176 , wanawake wakiwa na - sentimita 163 kwa wastani. Urefu wa Wairani umeongezeka kwa sentimita 16.5 ikilinganishwa na karne iliyopita. Urefu wa wanawake wa Korea Kusini ulikua hadi sentimita 20 katika kipindi hiki.
Watu warefu zaidi duniani wanaishi Uholanzi. Urefu wa wastani wa wanaume katika nchi hii ni cm 183, na ule wa wanawake ni karibu Sm 170. Tangu katikati ya karne ya 19, urefu wa Uholanzi umeongezeka kwa sentimita 20.
Wanasayansi wamefahamu kwa muda mrefu kwamba wanadamu wenye lishe bora na uhakika wa upatikanaji wa chakula huwa wanakuwa na ongezeko la urefu, na kukomaa kwa haraka zaidi kimwili.
Ugunduzi huo unaweza kuwezesha upatikanaji wa dawa za kuboresha misuli na kutibu uchochezi wa ukuaji , watafiti wa Uingereza wanasema.
'Zaa watoto wengi'
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Inajulikana kuwa mawimbi yanayotokana na chakula hufika sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus, ikiufahamisha kuhusu afya ya lishe ya mwili, na kuchochea ukuaji.
Kwa hivyo, wacha tuchunguze kwa nini tunakua warefu. Kadiri mtu anavyozeeka, mifupa yake hukua. Homoni za binadamu ni sababu ya hii. Jenetiki pia huathiri urefu wa mtoto. Watoto warefu huzaliwa kutoka kwa wazazi warefu. Lakini hii haielezi kila kitu.
Kulingana na utafiti, lishe ya mtoto huathiri moja kwa moja ikiwa atakuwa mrefu au mfupi. Watu wanaoishi katika nchi zilizo na chakula bora na tabia nzuri ya kula wana uwezekano wa kuishi muda mrefu.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Nature, na kuongozwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge pamoja na timu kutoka Chuo Kikuu cha Malkia Mary cha London, Chuo Kikuu cha Bristol, Chuo Kikuu cha Michigan na Chuo Kikuu cha Vanderbilt, umegundua king'amuzi cha ubongo nyuma kinachosababisha mchakato huo.
Kinaitwa MC3R na ni kiungo muhimu kati ya chakula na ukuaji wa kingono na ukuaji wa mwili kwa ujumla.
"Huufahamisha mwili kuwa sisi tuko vizuri sasa, tuna chakula kingi, kwa hivyo kua haraka, balehe hivi karibuni na uzae watoto wengi," Anasema Profesa Sir Stephen O'Rahilly, mwandishi wa utafiti, kutoka Cambridge.
"Sio uchawi tu - tuna mchoro kamili wa jinsi inavyotokea."

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati king’amuzi cha ubongo hakifanyi kazi kama kawaida kwa wanadamu, watafiti waligundua kuwa watu walikuwa na kimo kifupi, na walichelewa kuanza kubalehe baadaye kuliko watu wengine.
Timu ilitafuta muundo wa vinasaba wa wafanyakazi wa kujitolea nusu milioni waliojiandikisha katika Biobank ya Uingereza - hifadhidata kubwa ya habari za kijenetiki na afya - ili kudhibitisha iwapo hii ilikuwa kweli.
Watoto waliopatikana na mabadiliko ya jeni ambayo yanatatiza king’amuzi cha ubongo, wote walikuwa wafupi na walikuwa na uzito mdogo kuliko watoto wengine, jambo ambalo linaonyesha athari huanza mapema maishani.
Timu ya utafiti iligundua mtu mmoja ambaye alikuwa na mabadiliko katika nakala zote mbili za jeni za MC3R, ambayo ni nadra sana na inadhuru. Mtu huyu alikuwa mfupi sana, na alianza kubalehe baada ya umri wa miaka 20.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












