Kuna hatari gani kwa mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa?

Chanzo cha picha, DISCLOSURE/SES-AM
Hivi karibuni mwanamke mmoja huko Brazil alijifungua mtoto wa kiume ambaye ana urefu wa sentimita 59 na uzani wa kilo 7.3.
Angerson Santos alizaliwa kwa upasuaji katika hospitali ya Padre Colombo, huko Parintins katika Amazon ya Brazil.
Mtoto aliyewahi kurekodiwa kuzaliwa na uzito mkubwa zaidi duniani kote alikuwa na kilo 10.2 na ilikuwa mwaka 1955 huko nchini Italia.
Kwa kawaida, wavulana huwa wanazaliwa na uzito wa wastani wa kilo 3.3 na wasichana 3.2 kg.
Mtoto yeyote aliyezaliwa akiwa na uzito zaidi ya kilo 4 , bila kujali umri wa ujauzito, anachukuliwa kuwa mtoto aliyezidi uzito.
Watoto wenye uzito mkubwa zaidi huwa takriban 12% ya watoto wanaozaliwa. Kwa wanawake walio na ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito (sukari ya juu wakati wa ujauzito), asilimia hii huongezeka hadi kati ya 15% na 45% ya watoto wanaozaliwa.
Nini kinatokea?
Sababu fulani huongeza hatari ya mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa, mojawapo ikiwa ni uzito wa mwili.
Akina mama wanene wana uwezekano mara mbili wa kupata mtoto mchanga aliye uzito mkubwa kupita kiasi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Na kupata uzito kupita kiasi wakati wa ujauzito pia huongeza hatari ya mtoto kuwa na uzito mkubwa.
Ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito ni sababu nyingine ya hatari. Madaktari katika hospitali ya Padre Colombo wanahusisha ukubwa wa Angerson na ukweli kwamba mama yake ana kisukari.
Sehemu ya hali hii inatokana na kuongezeka kwa upinzani wa sindano za kisukari kwa mama wakati wa ujauzito (hata kwa wale wasio na ugonjwa wa kisukari wa ujauzito), ambao huongeza kiasi cha glukosi.
Hali hiyo pia husaidia kuongeza uzito kwenye ukuaji wake tumboni.
Mimba iliyochelewa pia huongeza uwezekano wa kuwa na mtoto wa mwenye uzito mkubwa.
Umri wa uzazi zaidi ya miaka 35 hufanya uwezekano wa 20% wa mtoto kuwa na uzito kupita kiasi.
Umri wa baba pia unahesabiwa. Umri wa baba zaidi ya miaka 35 huongeza hatari ya uzito kwa mtoto kuongezeka kwa 10%.
Mimba za awali huongeza hatari ya mtoto anayefuata kuwa na uzito mkubwa zaidi.
Mimba za muda mrefu zaidi (zinazozidi wiki 40 za kawaida) pia huongeza hatari ya mtoto kuwa na uzito mkubwa, haswa katika wiki 42 na zaidi.
Kuwa na mvulana pia huongeza uwezekano wa uzito kuwa mkubwa. Wavulana wana uwezekano mara tatu zaidi wa kuzaliwa uzito mkubwa kuliko wasichana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatari wakati wa kujifungua
Watoto wenye uzito mkubwa wana uwezekano mkubwa wa kuwa na ugumu wa kuzaliwa kupitia njia ya uzazi kutokana na ukubwa wao.
Ni kawaida kabisa, kwa mfano, kwa bega la mtoto kukwama na hivyo kufanyiwa upasuaji.
Akina mama pia wako katika hatari kubwa ya kuchanika uke wakati wa kujifungua, jambo ambalo huongeza hatari ya kuvuja damu baada ya kujifungua.
Kuvuja damu baada ya kuzaa ndio chanzo kikuu cha vifo vya uzazi duniani kote, na kwa hiyo kadiri mtoto anavyokuwa mkubwa ndivyo hatari ya kuumia inavyoongezeka wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida ya uke.
Uzito mkubwa kwa watoto wachanga pia husababisha hatari kubwa ya kuongeza muda wa hatua ya pili ya leba, ambayo hutokea wakati njia imepanuliwa kikamilifu na kichwa cha mtoto kinahamia kwenye uke.
Kwa sababu ya ukubwa wa watoto wa wenye uzito mkubwa harakati hii inaweza kuwa polepole kuliko kawaida, ambayo inaweza kuongeza hatari ya mama ya kupata maambukizi na kutokwa damu kwa ndani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jambo moja ambalo hatujui kuhusu watoto wachanga walio na uzito mkubwa zaidi ni kwamba wanabaki wakubwa katika maisha yao yote.
Takwimu chache zilizopo zinaonyesha kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito kupita kiasi au wanene zaidi wakiwa na umri wa miaka 7 na pia kupata kisukari cha aina ya 2 baadaye maishani.
Tunaweza kuona watoto wengi "wenye uzito mkubwa" wakizaliwa, kwani wale waliozaliwa baada ya 1970 wanaonekana kuwa na uzito wa karibu 450g zaidi ya watoto wachanga kabla ya hapo.
Pia, kwa kuongezeka kwa viwango vya uzito uliopita kiasi pia ni sababu kuu katika kuongezeka kwa watoto wenye uzito mkubwa.









