Gorbachev aliweka historia lakini alikuwa na 'mapenzi' na Magharibi: Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mikhail Gorbachev - kiongozi wa mwisho wa Usovieti, ambaye alifariki Jumanne - alikuwa na "athari kubwa katika historia ", anasema rais wa Urusi Vladimir Putin.
Alielewa mageuzi yalikuwa muhimu, alisema Bw Putin - huku Mkuu wa Umoja wa Mataifa , António Guterres, akimsifu kwa "kutetea amani bila kuchoka".
Msemaji wa Bw Putin, hatahivyo, alisema kuwa Bw Gorbachev alikosea kuamini katika "mapenzi ya kudumu" na nchi za Magharibi .
Bw Gorbachev alichukua mamlakaka katika mwaka 1985, kabla ya kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti mwaka 1991.
Alianzisha mageuzi, lakini hakuweza kuzia kuvunjika taratibu kwa muungano huo - na Warusi wengi wanamlaumu kwa miaka mingi ya msukosuko uliosababishwa na kuvunjika.
Katika ujumbe wake Bw Putin alisema: Alielewa fika kwamba mageuzi yalikuw amuhimu, alipigania kutoa suluhu zake mwenyewe kwa ajili ya matatizo ya dharura."
Bw Putin na Bw Gorbachev walikuwa na uhusiano mgumu - mkutano baina yao uliripotiwa kwa mara ya mwisho katika mwaka 2006.
Hivi karibuni kabisa, Bw Gorbachev alisemekana kutofurahia uamuzi wa Bw Putin wa kuivamia Ukraine ingawa aliunga mkono kutwaliwa kwa jimbo la Crimea katika mwaka 2004.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Msemaji wa kiongozi wa Urusi , Dmitry Peskov, alisema kuwa Bw Gorbachev "kwa nia njema aliamini kwamba Vita Baridi vingemalizika, na kwamba hilo lingewezesha kuingia katika kipindi cha mapenzi ya kudumu baina ya Muungano mpya wa Usovieti na dunia , nchi za Magharibi. Mapenzi haya yaligeuka kuwa kosa".
Bw Peskov alizilaumu chini za Magharibi ambazo zilipinga uvamizi wa Ukraine, kuiwekea vikwazo vikali Urusi, na kutoa silaha kwa Kyiv.
Katika rambi rambi zake Waziri mkuu wa uingereza Boris Johnson nalisema kuwa aliheshimu ujasiri na maadili ya Bw Gorbachev , na kuongeza kuwa :
Wakati wa uvamizi wa uchoozi wa Putin katika Ukraine, juhudi zake za bila kuchoka za kufungua jamii ya Usovieti ''zilisalia kuwa mfano kwetu zote."
Rais wa Marekani Joe Biden alimuita "kiongozi wa nadra", huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema: "Dunia imempoteza kiongozi kinara wa dunia, aliyejitolea katika mambo mengi, na ambaye hakuchoka kutetea amani.
Katika hospitali mjini Moscow ambako Gorbachev alifariki ilisema kuwa amekuwa na ugonjwa wa muda mrefu na kwamba aliugua sana.
Katika miaka ya hivi karibuni, afya yake ilizorota na amekuwa akienda hospitali mara kwa mara.
Mwezi Juni, chombo cha habari cha kimataifa kiliripoti kuwa alikuwa anaumwa ugonjwa wa figo, ingawa sababu ya kifo chake bado haijatangazwa.
Atazikwa katika makaburi ya Novodevichy mjini Moscow, eneo wanakozikwa Warusi wengi maarufu. Haijafahamika wazi iwapo atafanyiwa mazishi ya kitaifa.
Bw Gorbachev alikuwa katibu mkuu wa chama cha Kikomunisti cha Usovieti, na kiongozi mwenye mamlaka zaidi ya nchi, katika mwaka 1985.
Wakati huo, alikuwa na umri wa miaka 54 - mjumbe mweney umri mdogo zaidi katika baraza la utawaka lililofahamika kama Politburo,na aliangaliwa kama mtu mwenye kuleta matunaini miongoni mwa viongozi kadhaa wazee.
Mtangulizi wake, Konstantin Chernenko, alifariki akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja na miezi mamlakani.
Viongozi wachache wamekuwa na athari kubwa katika dunia , lakini Bw Gorbachev hakuingia mamlakani kutafuta kumaliza Usovieti kwa ajili ya Ulaya Mashariki. Badla ayake , alitumai kuimarisha jamii yake.
Uchumi wa Usovieti ulikuwa unahangaika kwa miaka kuendelea kukabiliana na kai ya Marekani na sera yake ya perestroika ilitaka kuanzisha mageuzi fulani ya masoko katika mfumo unaoongozwa na taifa.
Kimataifa alifikia mikataba ya udhibiti wa silaha na Marekani, alikataa kuingilia kati wakati mataifa ya Ulaya mashariki yalipoamka dhidi ya viongozi wao wa Kikomunisti, na alimaliza vita vya Usovieti vilivyosababisha mauaji katika Afghanistan, vita ambavyo viliibuka mwaka 1979.
Wakati huo huo, sera yake ya glasnost, au uwazi, iliwaruhusu watu kukosoa serikali kwa njia ambayo haikufirikika awali.
Lakini pia ilipelekea kuibuka kwa hisia za utaifa katika maeno mengi ya Muungao wa Usovieti ambayo hatimaye yalishusha utabiti wake na kuharakisha kuvunjika kwa muungao huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Anaonelewa na Magharibi kama muasisi wa mageuzi ambaye alibuni hali kwa ajili ya kumaliza Vita Baridi katika mwaka 1991 – katika muda ambapo kulikuwa na hali ya wasi wasi baina ya Muungano wa Usovieti na matafa ya Magharibi.
Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel katiika mwaka 1990 "kwa nafasi yake ya kuongoza mabadiliko makubwa katika mahusiano ya Mashariki na Magharibi ".
Bw Gorbachev alifanya jaribio moja baya la kurejea katika maisha ya siasa mwaka 1996, ambapo alipata 0.5% tu ya kura katika uchaguzi wa urais.
Henry Kissinger, ambaye alihudumu kama Waziri wa mambo ya nje wa Marekani chini ya utawala wa raus President Richard Nixon, alikiambia kipindi cha BBC cha Newsnight kwamba Bw Gorbachev ‘’atakumbukwa katika historia kama mwanaume aliyeanzisha mabadiliko ya kihistoria ambayo yalikuwa ya manufaa kwa binadamu na kwa watu wa Urusi".
Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel katiika mwaka 1990 "kwa nafasi yake ya kuongoza mabadiliko makubwa katika mahusiano ya Mashariki na Magharibi ".
Bw Gorbachev alifanya jaribio moja baya la kurejea katika maisha ya siasa mwaka 1996, ambapo alipata 0.5% tu ya kura katika uchaguzi wa urais.
Henry Kissinger, ambaye alihudumu kama Waziri wa mambo ya nje wa Marekani chini ya utawala wa raus President Richard Nixon, alikiambia kipindi cha BBC cha Newsnight kwamba Bw Gorbachev ‘’atakumbukwa katika historia kama mwanaume aliyeanzisha mabadiliko ya kihistoria ambayo yalikuwa ya manufaa kwa binadamu na kwa watu wa Urusi".
Vladimir Rogov,ambaye ni afisa aliyeteuliwa na Urusi katika eneo la Ukraine lililonyakuliwa, alisema Bw Gorbachev alikuwa "aliongoza kimakusudi Muungano wa Usovieti hadi kifo chake " na alimuita msaliti.
Ni nini Warusi wa kawaida wanamfikiria labda waliozingira nyumba ya matangazo ya kuoka mikate ya Pizza - iliyotengenezwakwa ajili ya soko la Marekani – kwamba alishiriki ndani yake katika mwaka 1997.
Katika tangazo la biashara, walaji walijadili kuhusu vurugu zilizotokea – au fursa zilizobuniwa – mwishoni wa muungano wa usovieti, kabla ya kusherehekea kwa pamoja maisha yake.















