Kwa picha: Maisha ya kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev

Chanzo cha picha, Getty Images
Mikhail Gorbachev, mwanaume ambaye aliendelea na hatimaye kuwa mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa zaidi katika karne ya 20, alizaliwa katika hali ya umasikini tarehe 2 Machi 1931 katika jimbo la Stavropol rkusini mwa Urusi
wazazi wake wote walifanya kazi katika mashamba ya pamoja na utoto wake Gorbachev alifanya kazi hiyo pamoja na wavunaji akiwa na umri wa kubalehe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati anasoma katika Chuo kikuu cha Kitaifa cha Moscow, alikutana na mke wake, Raisa, na kuwa mjumbe wa chma cha kikomunisti . Baada ya kuhitimu, alirejea Stavropol na kuanza kupanda kwa haraka vyeo katika Chama cha kikomunisti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika mwaka 1985, kiongozi wa Usovieti Konstantin Chernenko alifariki mwaka mmoja tu baada ya kuingia mamlakani , na Mikhail Gorbachev ambaye alikuwa kijana zaidi akawa kiongozi wa USSR.
Wakati ule, uchumi wa Muungano wa Usovieti ulikuwa mashakani kuweza kuhimili kasi ya Marekani, na Gorbachevtafuta suluhu mbili kuu. Alisema nchi inahitaji "perestroika" - au mpango mpya - na zana yake ya kukabiliana nao ni "glasnost" - uwazi .
Silaha yake nyingine ya kukabiliana na mkwamo wa mfumo wa uchumi ni demokrasia. kwa mara ya kwanza kulikuwa na uchaguzi huru katika bunge la watu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Gorbachev pia alitaka kumaliza Vita Baridi, ambavyo vilikuwa vinaigharimu nchi yake mamilioni ya dola kila mwaka ili kuendeleza kasi ya ukuaji wa haraka wa matumizi ya jeshi la Marekani.
Katika mwaka 1985, alikutana na rais wa Marekani Ronald Reagan kwa mazungumzo kuhusu kuweka ukomo wa uzalishaji wa makombora ya nyuklia na kuanzisha upya mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo yenye nguvu zaidi .
Pia alimaliza vita vya muda mrefu vya Usovieti katika Afghanistan, ambavyo vilikuwa vimegharimu maisha ya maelfu ya watu tangu Moscow ilipoingilia kuunga mkono serikali ya kisopale katika mwaka 1979.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makubaliano hayo yaliwezesha kusitishwa kwa utumiwaji wa maelfu ya makombora.
Huku mageuzi yake yalikuwa maarufu miongoni mwa viongozi wa Magharibi, USSR ilianza kugawanyika taratibu chini ya uongozi wake , na katika usiku wa kuamkia Krismasi mwaka 1991, Gorbachev alikubali kuvunjwa kwa Muungano wa Usovieti.
Gorbachev aliendelea kuwa na jukumu la kuwa mzungumzaji wa masuala ya Urusi na ya kimataifa, lakini alisifiwa sana nje ya nchi kuliko nyumbani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alipatwa na pigo la kibinafsi mwaka 1999, wakati Rais alipofariki kwa saratani ya damu . Uwepo wake wa wakato wowote kando na mumewe ulionyesha sura ya ubinadamu katika mageuzi ya kisiasa.
Baada ya Vladimir Putin kuingia katika mamlaka ya dunia, Gorbachev alikuwa mkosoaji wa wazi, akimshutumu kuendesha utawala wa ukandamizaji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Gorbachev alifariki mjini Moscow huku Urusi ikiivamia Ukraine, operesheni ambayo baadhi wanasema ni jaribio la Putin la kujenga upya ushawishi wa Usovieti .

Chanzo cha picha, Getty Images















