Vita vya Ukraine: 'Watoto wangu walikuwa wakilia kila usiku wakiuliza kama tutakufa’

ggg

Kuwafanya watoto wake wasilie kila usiku na kuuliza kama watauawa ndiyo sababu ya Kateryna Halenda kujua kuwa ni wakati sahihi wa kutoroka Ukraine.

Kuiacha nchi iliyosambaratishwa na vita inaweza kuonekana kuwa uamuzi rahisi lakini hakutaka kuondoka na kumuacha mume wake nyuma hivyo mume wake Oleh alilazimika kumshawishi aondoke na watoto wao wawili wachanga.

Kateryna sasa anajua yeye na watoto wake wako salama lakini bado anapata taarifa kwa simu ya mkononi wakati mashambulizi ya anga yanapofanyika nyumbani.

Wasiwasi bado anao, akitumai Oleh yuko sawa.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 32 na wanawe wawili wa kiume Oleksander miaka tisa na Artem mwenye umri wa miaka minne ni watatu kati ya wakimbizi zaidi ya milioni tano ambao wameikimbia Ukraine huku wakiwa na wasiwasi kuhusu familia ambayo wameiacha.

bbb

Lakini tofauti na wakimbizi wengi 60,000 wa Ukraine ambao wamewasili Uingereza tangu Urusi ilipovamia Ukraine, Kateryna na watoto wake hawajachukuliwa na familia zinazojitolea kusaidia.

Kambi ya kipekee 'kama familia'

Wao ni mojawapo ya familia 60 ambazo ziko katika jumuiya ya kipekee ya Kiukraine maelfu ya maili kutoka nchi yao katika kambi maalum inayotoa mahali pa kukaa, chakula, elimu na ushauri – sehemu patakatifu Wales.

"Ni kama familia kubwa hapa. sote tunaangaliana," Kateryna alisema.

"Tulishangaa tulipokuja hapa. Ni mpya sana lakini sasa wana furaha kabisa, wanacheza na watoto wengine kila siku na kwenda shule kila siku. Na wanahisi salama hapa na hilo ni muhimu."

ggg

Kateryna ni mmoja wa wakimbizi 222 wa Kiukreni kwenye kambi inayoendesha shirika la vijana la Wales Urdd Gobaith Cymru na kuungwa mkono na serikali ya Wales ambapo zaidi ya watoto 100 waliofurushwa majumbani mwao sasa wanaweza kucheza na kujifunza kwa usalama.

'Mume wangu alinifanya niendoke na watoto'

Hata hivyo wakati wazazi na babu na babu zao wanafurahia eneo hili mbali na vita, nyumba na familia ziko mawazoni mwao na hiyo inaeleza kwa nini hawakuta kukimbia mapema.

ggg

"Tulisubiri kwa siku 100 kwa sababu hatukutaka kuondoka mwanzoni lakini mume wangu alitulazimisha kwenda," alisema Kateryna.

"Haikuwa salama. Tulikuwa mara kwa mara chini kabisa ya nyumba yetu kwa sababu ya milio ya mashambulizi ya anga wakati wote ikiwa ni pamoja na usiku nilipolazimika kuwaamsha watoto wangu.

"Lakini tuliamua kuondoka ili kutafuta mahali salama kwa watoto wangu."

ffgf
Maelezo ya picha, Artem mwenye umri wa miaka minne na Oleksander, 9, wanamkosa baba yao Oleh ambaye ilibidi abaki Ukraine.

Kateryna hakumfahamu Olena Andrshchuk kabla ya kufika kituoni hapo Wales wiki mbili zilizopita.

Lakini sasa akina mama hao wamekuwa marafiki na kusaidiana huku waume zao wakiwa bado wapo Ukraine

'Kulikuwa na bomu karibu usiku tulipoondoka'

Mume wa Olena Pavlo pia alimfanya mkewe kuondoka nyumbani kwao katika mji mkuu wa Kyiv kwa ajili ya usalama wake na watoto wao wawili.

"Bado si salama," alisema mwandishi wa maudhui ya tovuti mwenye umri wa miaka 36.

bbb

“Siku hiyohiyo tunatoka, karibu sana na tunapoishi niliamka usiku wa manane kwa sababu ya mlipuko mkubwa sana wa mabomu. 

"Bado haukuwa uamuzi rahisi kuondoka kwa sababu bado nililazimika kuacha mji wangu wa nyumbani, mume wangu, kila kitu nilicho nacho - lakini niliondoka kwa watoto wangu."

Olena anasema "anapenda" kuwa Wales na anafananisha kituo hicho na "mapumziko ya likizo" yenye marafiki wengi wapya walio na uzoefu wa pamoja lakini ukumbusho wa kile kinachotokea nyumbani haviko mbali sana.

"Nina programu kwenye simu yangu na bado ninapata tahadhari ya milio ya mashambulizi nchini Ukraine na vinasikika mara kwa mara," alisema Kateryna, ambaye mume wake Oleh ni mfanyakazi wa kujitolea katika jiji lao la Ternopil, magharibi mwa Ukraine.

hhh

"Kwa hivyo najua ni wakati gani wa kumpigia simu mume wangu kumuuliza hali yake."

Kurudi shule

Kituo cha Urdd kwa kawaida huwa na shule za Wales lakini watoto wake wa Kiukraine ambao wamekuwa wakiishi, wakisoma na kucheka katika Eneo hili dogo la mashambani la Wales kwa muda wa miezi miwili iliyopita wakifurahia ukweli kwamba wako huru kucheza na kufurahia kwa usalama tena.

"Watoto wangu hawakuhudhuria shule kwa hadi miezi mitatu kwa sababu haikuwa salama," Kateryna alisema.

"Lakini sasa wana furaha kwani wanaenda shule kila siku na wanahisi salama."

ggg

Olena alikubali huku mdogo wake Leonard, mwenye umri wa miaka minne, akikabiliana na ukosefu wa mwingiliano wa kijamii na watoto wa rika lake kwa sababu wengi walikuwa wakilia ndani kwa sababu watu "waliogopa sana" kuwaruhusu kucheza nje huku mashambulizi ya angani yakisikika pande zote.

"Ilikuwa shida kubwa kwa mdogo wangu huko Ukraine," alisema.

“Sasa tumefika hapa, watoto wanaweza kujumuika, kuwasiliana wao kwa wao na wako wazi kwa shughuli za kila aina, ambazo walikuwa wamezikosa kwa muda mrefu hivyo wanafurahi tu.

bbb

Bila shaka wanamkosa baba na babu na bibi zao lakini huu ndio ukweli bora kuliko ule tuliokuwa nao huko Ukraine."

Wakimbizi wanafikiria nini kinachofuata

Ingawa watoto wanafurahia kuna masomo ya kila siku katika Kiingereza na Kiwelshi na ulimwengu wa shughuli, wazazi wao wanaweza kuelekeza nguvu zao katika kutafuta kazi, kupata manufaa na kufahamu wanakoenda.

Usaidizi huo wote wa kitaalamu kwa familia za wakimbizi hutolewa kwenye tovuti katika duka moja ambalo pia lilitoa ukaguzi wa afya kwa kila mtu aliyefika kiasi cha kufurahishwa na bibi Marta Burak.

"Nilifurahi sana kwa sababu mjukuu wangu alipimwa ugonjwa hapa na hatukuweza kufanya nyumbani," alisema mwalimu huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 64.

"Sasa anatumia dawa za miezi mitatu. Hilo lilikuwa muhimu sana kwangu."

ggg

Wakati binti yake Khrystyna anapata masomo ya kina ya Kiingereza yanayotolewa na chuo cha eneo hilo, Marta, ambaye yuko katika wiki yake ya tano katika kituo hicho, anapata usaidizi na ushauri kutoka kwa mamlaka ya tovuti ili kubaki Uingereza.

"Wakati tunafanya mambo muhimu ya kisheria kukaa Uingereza, tungependa kukaa hapa milele," alisema. "Lakini siku moja, itabidi tuendelee."

Hata hivyo Marta anasema "wakati nusu ya moyo wake iko Wales, nusu imesalia nchini Ukraine".

bbb

“Mwanangu, binti-mkwe wangu na mkwe wangu wamebaki Ukraine na wajukuu zangu wanamkosa baba yao kila siku.

“Hawawezi kuongea naye vizuri kwa sababu wanaanza kulia lakini tuko salama hapa, hilo ndilo jambo la muhimu zaidi.

"Jana nilipata habari za kusikitisha kwa sababu mtoto wa pekee wa familia ya rafiki yangu aliuawa na alikuwa na umri wa miaka 30. Alikuwa kijana mzuri, mwenye mtazamo mzuri na inasikitisha vijana bado wanakufa katika vita hivi na hii lazima ikomeshwe. "

ggg
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nyumbani hakupo mbali na mawazo ya watu vichwani mwao lakini uungwaji mkono wa wenyeji wanaoweka bendera ya Ukraine kwenye madirisha yao kunawapa wakimbizi matumaini.

Na katika maegesho ya kambi kuna magari machache yenye nambari za usajili za Kiukraine huku familia moja ikilazimika kupita Urusi ili kuepuka mapigano kwenye mstari wa mbele kabla ya kupata njia ya kuelekea Wales.

Watu nchini Wales hadi sasa wamechangisha mamilioni ya pauni kwa ajili ya msaada kibinadamu kwa Ukraine na Wales imehifadhi zaidi ya wakimbizi 2,500.

Serikali ya Wales imefadhili moja kwa moja karibu watu 3,000 kuja Wales na wengi wao bado hawajafika lakini mpango huo umesitishwa ili kuruhusu watu kuendelea kutoka katika 'vituo vyao vya kukaribishwa'.

Mark Drakeford anataka Wales kuwa "taifa takatifu" na kuwasaidia wakimbizi wa Ukraine "kuanzisha upya maisha yao".

Lakini waziri wa kwanza wa Wales alikubali kuwa "changamoto kwa wiki zijazo" ni kusaidia watu wengi zaidi kuondoka kituo hicho na kupelekwa katika maeneo ya kudumu zaidi ili wakimbizi zaidi waweze kuhifadhiwa na kusaidiwa.

bbb