Vita vya Gaza: Nini hatma ya Hamas baada ya mashambulizi mapya ya Israel?

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Brigedi za Izz ad-Din na al-Qassam ambazo ni tawi ya kijeshi ya kundi la Hamas, zilirusha makombora na kuzielekeza katika mjiw a Tel Aviv Alhamisi Machi 20 kama majibu ya mashambulizi kutoka kwa jeshi la Israel kwenye ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Ukanda wa Gaza inayosimamiwa na kundi la Hamas, idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi haya mapya imepita watu mia sita kwa muda wa siku tatu huku wengine 1000 wakijeruhiwa – Idadi kubwa ya waathiriwa ikiwa ni wanawake na Watoto.

Majibu haya kutoka kwa Hamas, yametajwa kuwa ya kwanza ya aina yake tangu Israel kurejelea mashambulizi yake ya kijeshi katika baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza. Mashambulizi haya yalianza upya alfajiri ya Jumane Mach 18,2025, wakati ambapo Israel ilikuw apia inatoa vitisho na onyo kwao, ambalo lilitolewa na Waziri wa Ulinzi, Israel Katz ambaye alitangaza katika taarifa iliyopeperushwa kwenye runinga siku ya Jumatano Machi 19 akilenga matamshi yake kwa raia wa Gaza:

"Kinachokuja kitakuwa kigumu zaidi..Wakazi wa Ukanda wa Gaza, hili ndilo onyo la mwisho..Mutalipia gharama ya juu..Ikiwa mateka wote hawatarejeshwa na Hamas haijamalizwa Gaza, Israel itachukuwa hatua ya nguvu ambayo hamujaishuhudia awali."

Kwa sasa , kundi la Hamas linajipata katika njia panda na linakabiliwa na hali ya kulazimika kufanya uchaguzi wa hatua watakazozichukuwa , hasa baada ya Israel kurejelea mashambulizi yake ya angani huko Gaza. Kwa mujibu wa taarifa za kutoka kwa vyanzo vilivyokaribu na kundi hilo, Hamas inaangazia suala la kutatua mzozo huu kisiasa ili kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi zaidi yanayotishia maisha na usalama wao. Aidha Hamas inaangazia kufanya uamuzi ambao inasema hautadunisha haki za tawil lake la kijeshi kujibu mashambulizi kutoka kwa jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.

Katika muda wa miezi kumi na mitano ya vita, kundi hilo limepoteza uwezo wake mkubwa wa kijeshi, hasaa makombora yenye uwezo wa kusmabulia masafa marefu ambayo imekuwa ikirusha kuelekea mji wa Telaviv na maeneo ya ndani ya Israel.

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Israel imeanza tena operesheni ya kijeshi kwenye ukanda wa Gaza, Jumanne Machi 18, 2025

Hata hivyo, taarifa za vyombo vya Habari vimesema kwamba Brigedi ya Qassam, wakati wa kusitishwa kwa mapigano, iliweza kujenga idadi ndogo ya makombora ya masafa marefu na wakati huo huo pia walitoa vifaa muhumi vya kutumia katika vita kwenye mahandaki yaliyochimbwa chini ya ardhi.

Wapiganaji wa kundi hilo la Hamas walifanyia ukarabati vifaa hivyo, japo hakuwa na viungo muhimu vya kutekeleza kazi hiyo vyema, ila wamefanikiwa kuhakikisha kwamba wako tayari kwa mapigano.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kundi la Hamas limekiri kwamba uwezo mkubwa wa kivita upo kwa upande wa jeshi la Israel, na kwamba wapiganaji wake wana silaha ambazo hazina uwezo mkubwa kama zile za jeshi la Israel. Hamas pia inaelewa kwamba hahawezai kuyategemea mataifa ya Kiarabu kuwapa usaidizi kukabiliana kijeshi na Israel.

Hata hivyo, kundi hilo limesema kwamba ikiwa watalazimishwa kukabiliana kivita, liko tayari na kwamba haliwezi kukubali matakwa ya Israel na Marekani ya kudhibiti ukanda wa Gaza.

Wapalestina wameweka Imani yao mara kw amara katika shutuma ya jamii ya kimataifa kwa Israel na vile vile shinikizo la ndani dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kumaliza vit. Hata hivyo ombi lao kwa jamii ya kimataifa kuchukuwa hatua ya kuilazimu Israel kumaliza vita halijasikizwa.

Bila ya jibu, wacmabuzi wanasema kwamba sera za serikali ya sasa ya Marekani, zinaegemea upande wa Israel, hali inayoipa fursa ya kufanya watakalo katika ukanda wa Gaza. Rais Trump alizungumz ana Waziri Mkuu Netanyahu kwa kusema, "Fanya unachokihisi ni bora kuimaliza hamas huko Gaza."