Trump alijaribu kuzuia mzozo wa kijeshi kwa kumuandikia barua kiongozi wa Iran

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Mjumbe maalum wa Rais Donald Tump katika eneo la mashariki ya kati – Steve whitaker, amesema kwamba Rais wa Marekani aljaribu kuzuia mzozo wa kijeshi dhidi ya Iran kwa kujenga uhusiano wenye Imani na serikali ya Tehran.

Bwana Whitaker amesema katika mahojiano na mwandishi wa habari mwenye utata mkubwa - Tucker Wilson, ambaye anasemekana kuwa na uhusiano wa karibu na Rais Trump – kwamba " barua ya hivi maajuzi ya Rais Trump kwa kiongozi wa Iran haikutazamiwa kuwa tishio."

Akimtetea Rais Trump kwa hatua yake ya kuituma barua hiyo Iran, Bwana Whitaker amesema kwamba: " Donald Trump ana uwezo mkubwa wa kijeshi na ingekuwa vyema kwa Iran kutafuta suluhu ya Kidiplomasia. Lakini, ni Rais wa Marekani ambaye amelifanya hili."

Aidha, mjumbe huyo maalum wa Rais Trump, ameongezea kwa kusema kwamba : "Barua hiyo haikutumwa kwa sababu yeye ni mjinga, la! Rais Trump ni mwenye nguvu kubwa na ni miongoni mwa wanaume wenye nguvu kuu ambao nimewahi kutangamana nao maishani mwangu, na huenda hata akawa mwenye nguvu zaidi."

Steve Witkoff aliendelea kusema kwenye mahojiano hayo kwamba, yaliyokuwa ndani ya barua hiyo ni: " Mimi ni Rais wa amani. Hilo ndilo ninalolitaka. Hakuna haja ya kutatua mzozo huu kwa njia ya kijeshi. Tunahitaji kuzungumza. Tunahitaji kupata suluhisho ya masuala ambayo yamefanya sisi kutoelwana."

"Tunahitaji kubuni mbinu ya kudhibitisha kwamba hakuna mmoja kati yatu ambaye atakuwa na hofu ya kulenga mpango wa kinyuklia unaotengeza sialaha za kiwango cha juu…kwa sababu njia nyingine inayoweza kutumika katika hali hii, sio nzuri sana."

"Iran wametujibu. Sina idhini ya kuzungumzia waliyoyasema," alisema.

"Mazungumzo ya kutafuta makubaliano na taifa la Iran yanaendelea kupitia njia za siri na zinahusisha mataifa kadhaa na njia nyingine nyingi," alisema mjumbe maalum wa Rais Trump katika eneo la Mashariki ya kati, katika mahojiano na Tucker Carlson.

Aliongezea kwamba ," Trump yuko tayari kubuni nafasi ya kutatua matatizo kati ya Marekani na Iran kwa ajili ya taifa hilo kurejea katika utambulisho wa jamii ya kimataifa.

Na vile vile Iran isiwe inakabiliwa na vikwazo. Trump anataka kujenga uhusiano wa kuaminiana kati ya Marekani na Iran."

Rais Trump alisema haya wiki mbili zilizopita, kwamba alimuandikia barua kiongozi mkuu wa Iran, Ayatolla Ali Khemeni na kumpa mualiko wa kufanya mazungumzo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbas Araghchi aliambia kituo cha Habari kinachomilikiwa na serikali ya Iran kwamba : " Hatuna haraka ya kuijibu barua hiyo, kwa sababu kwa sasa tunatekeleza ibada ya Swaum katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na vile vile wako katika siku za Nowruz."

"Jibu litatolewa katika siku zijazo," alisema. Barua ya Trump, ni zaidi ya tishio, ila anadai kwamba kuna nafasi katika aliyotowa.

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Witkoff
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bwana Arachi amesema kwamba," Mwaka wa 1404 ni mgumu sana. Ila hatutafanya mazunguzo ya moja kwa moja."

Wiki moja baada ya Rais Trump kusema kwamba, alikuwa amemuandikia barua kiongozi wa Iran Mahmoud Gargash, mshauri wa Kidiplomasia wa Rais katika Ufalme wa Milki za Kiarabu UAE, alikutana na Bwana Araghchi mjini Tehran na kuwasilisha barua kwake.

Taarifa kwamba, barua hiyo ilikuwa imewasilishwa Iran, ilikuja wakati ambapo kiongozi mkuu wa Iran Ayatolla Ali Khamenei alikuwa anaelezea mualiko wa Marekani kufanya mazungumzo na kuwa na makubaliano kama njia ya , "uongo na kubadili maoni ya jamii ya kimataifa."

Katika siku ambayo Bwana Khamenei alipokea barua ya Rais Trump, alisema kwamba Iran haitafuti vita, ila inahakikisha kwamba iko tayari kujibu shambulizi dhidi yake.

Akizungumzia hatua ya Marekani kujiondoa kwenye mpango wa JCPOA, alimtaja Rais Trump kama mtu ambaye, " alitupilia mbali mkataba uliomalizwa, na kutiwa saini ."

Baada ya kushinda uchaguzi wa Urais mwezi Novemba 2024, Donald Trump alimteuwa Bwana Whittaker kama mjumbe wake rasmi wa Mashariki ya kati. Hana uzoefu wa Kidiplomasia, ila amekuwa akijishughulisha na mazungumzo ya kupata maelewano kati ya mashirika mbali mbali kwenye soko la kununua na kuuza nyumba na ardhi jijini Ney York Marekani kwa muda mrefu.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Leila Mohammed