Kenya: Maisha katika mazingira ya uhaba mkubwa wa chakula

Anne Soy

BBC News

vijana

Katika kituo cha usambazaji wa chakula katika kijiji cha Kachoda, mama mmoja anaguna huku akipokea nafaka na mafuta ya kupikia - lakini hana uwezo wa kubeba.

Kifurushi kinaanguka chini anapojaribu kukiinua kichwani. Lakini ni miongoni mwa wachache waliobahatika ambao wamechaguliwa kupokea msaada huo – kuna mamia ya watu wamekusanyika nje ya kituo cha usambazaji chakula, wengi wao wakiwa wamebeba magunia matupu.

Hakuna nyasi zinazoweza kuonekana katika eneo hili lenye vumbi na kavu, ambalo liko karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini.

Ninasafiri na Samantha Power, msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAid). Ametoa wito wa msaada zaidi wa kimataifa "kuepusha janga la njaa" katika eneo hili.

Marekani pekee haiwezi kukidhi mahitaji ya watu wanaohitaji msaada wa dharura barani Afrika, anasema.

Kiongozi wa jumuiya hiyo Enos Lochul amepoteza mifugo yake
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini hata yeye binafsi ameathirika. "Ninajisikia vibaya sana, inachoma moyo wangu," anasema, akielezea kuwa alikuwa ombaomba baada ya ukame wa muda mrefu kufuta chanzo chake pekee cha maisha - mifugo yake. "Watoto wangu wanakuja kuniomba chakula, lakini sina namna ya kuwapatia chakula. Siwezi kujizuia kulia, machozi yanatoka tu. Wanaomba ada ya shule, lakini sina chochote."

Watoto wake wamelazimika kuacha shule na mkewe amelazimika kuzalisha mkaa na kutafuta kuni ili kuuza. Bi Power, balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, anasema USAID imefanya uwekezaji wa $200m (£167m) katika virutubisho vya matibabu nchini Kenya, ambapo watoto milioni moja wana utapiamlo, "lakini zaidi inahitajika".

"Tunazungumza juu ya upotezaji mkubwa wa riziki na hatari ya upotezaji mkubwa wa maisha," anasema. "Na ndio maana Marekani imejitokeza, lakini mahitaji hapa ni makubwa zaidi kuliko nchi yoyote inaweza kubeba". Samantha Power akutana na wenyeji huko Kachoda.

Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, anasema USAID imefanya uwekezaji wa $200m

Mashirika ya misaada yakiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani yanasema kuwa takriban watu milioni 50 katika eneo la Pembe ya Afrika - yaani Somalia, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Uganda, Sudan Kusini na Sudan - wanaweza kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula mwaka huu ikiwa hawatapata msaada wa haraka wa chakula.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

"Kuna matukio makubwa ya utapiamlo katika ngazi ya jamii kati ya walio chini ya miaka mitano," anasema Emily Emoru, mhusika mkuu wa mkakati wa afya ya jamii.

Akina mama kadhaa wenye watoto wenye utapiamlo mkali wamekutana na Balozi Power katika kituo cha afya cha Kachoda.

Mmoja wao alikuwa Achwaa Katabo, mama wa watoto wanane. Akiwa amemshika mtoto wake aliyedhoofika wa miaka mitatu, anaeleza jinsi kila anapopokea chakula kinachotakiwa kudumu kwa mwezi mmoja au miwili, bado atagawana na jamaa na majirani, hivyo kinaisha ndani ya siku chache.

Mbuzi wake wote walikufa kwa njaa. Mtoto wake aliandikishwa kupata virutubisho vya lishe katika kituo cha afya, lakini Emily anasema athari kwa kawaida huwa ya muda mfupi.

"Baada ya kuruhusiwa kuingia katika jamii, katika kaya ambayo hawana chakula, watoto hawa kwa kawaida hurejea," anaelezea.