Uchumi wa Ruzuku: Je, gharama ya maisha itapungua Kenya?
Na Charles Gitonga
BBC News

Chanzo cha picha, Business daily/Twitter
Kwa Wakenya wengi, hali ya uchumi inaweza kuelezewa vizuri kwa kuangalia bei ya bidhaa muhimu –unga wa mahindi dukani.
Unga wa mahindi ndio kiungo kikuu cha ‘ugali’ - chakula kinacholiwa na watu wengi nchini Kenya. Bei yake inaangaliwa kwa karibu na wengi, kwa kuwa inaathiri bajeti za jamii nyingi moja kwa moja.
Hilo linaweza kuelezea kwanini taaarifa ya kupunguzwa kwa bei ya unga imezua gumzo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Kenya, ilieleza kwamba serikali ilikuwa imetangaza ruzuku ambayo ingepunguza bei ya unga - kutoka Ksh 210 ($1.77) hadi Ksh 100 (dola senti 84) kwa pakiti ya kilo mbili katika wiki nne zijazo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Hata hivyo taarifa hiyo imedhibitishwa kuwa isiyo ya ukweli, huku muungano wa wasaga nafaka nchini humo ukisema kuwa mazungumzo na serikali yanaendelea, ila mpango huo haujapitishwa.
Hii si mara ya kwanza kwa serikali nchini Kenya kutia mkataba na wasagaji wa mahindi ili kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya ruzuku. Mnamo 2017, wizara ya kilimo ilitoa kandarasi kwa wasagaji tisa kupunguza gharama ya unga wa mahindi.
Hata hivyo, makubaliano hayo yalishindikana baada ya wasagaji kushutumu serikali kwa kushindwa kulipa ruzuku hiyo.
Kwa nini ruzuku hiyo inaonekana kama chambo cha kampeni?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ingawa Wakenya watalazimika kusubiri kwa muda zaidi kunufaika na bei nafuu ya unga, muda wa ruzuku hiyo umewekewa alama ya kiulizo na baadhi yao na wanasiasa vile vile.
Wamedai kwamba hatua hiyo inakusudiwa kushawishi zoezi la upigaji kura Kenya, huku taifa hilo linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mnamo Agosti 9, 2022.
Kuna wagombea wanne walioidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwania urais.
Kati ya hao, wawili wamevutana sana katika kura za maoni, na inatarajiwa pakubwa kuwa mchuano kati ya Naibu Rais, William Ruto, na mwanasiasa mkongwe na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.
Ruto, ambaye alijitokeza kuwa mkosoaji mkuu wa serikali anayohudumu, amemlaumu Rais anayeondoka, Uhuru Kenyatta, kwa kumtenga na kumuidhinisha Bw Odinga kuwa mrithi wake.
Amehoji hadharani ruzuku iliyokusudiwa na serikali .
"Serikali inataka kupunguza bei ya Unga kwa sababu uchaguzi umekaribia," Ruto alisema alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni jijini Nairobi, Jumatatu.
Lakini baadhi ya wataalam wamekosoa kauli hiyo, na kusema kuwa mazungumzo ya ruzuku ya unga huenda yawe na msukumo tofauti. Tayari kumekuwa na maandamano jijini Nairobi, wakaazi wakiitaka serikali kupunguza gharama ya maisha.
"Pindi tu bei ya bidhaa fulani muhimu inapofikia viwango fulani, hilo linaweza kuleta matatizo makubwa kwa watu wengi, na kuifanya vigumu sana serikali kutawala," mwanauchumi Ken Gichinga aliiambia BBC.
"Tumeona matukio hapo awali ambapo haukuwa mwaka wa uchaguzi lakini serikali iliwalazimu wauzaji mafuta, kwa mfano, kudumisha bei ya mafuta," alielezea Gichinga.
Ruzuku ni nini?
Ni kiasi cha pesa kinachotolewa na serikali au shirika la umma kusaidia biashara kudumisha kiwango cha chini cha bei ya bidhaa muhimu.
Ruzuku pia inaweza kutolewa kwa sekta fulani ya uchumi, ili kusaidia bidhaa zinazozalishwa na biashara za kibinafsi kushindana sokoni kwa kuwa zenye bei nafuu.
Kwa mfano, mapema mwaka huu serikali ya Kenya ilitangaza ruzuku ya mbolea ya dola milioni 48.1, ili kuwawezesha wakulima kumudu mbolea. Hii ingeboresha mavuno yao, na kuwaruhusu kuuza mazao yao kwa bei nafuu. Bila ruzuku hiyo, bei ya mazao ingekuwa ya juu sana na hivyo kukosa ushindani sokoni.
Je, ruzuku inatekelezwa vipi?
Serikali, au mamlaka za seriali huzingatia kikapu cha bidhaa za kawaida.
"Kikapu kinatoa jumla ya kiasi gani familia hutumia, ambacho ni kikapu sawa wanachotumia kukadiria mfumko wa bei," anaeleza Ken Gichinga.
Kikapu hicho huwa na bidhaa kama vile unga wa ngano, wa mahindi, karoti, viazi, mafuta ya kupikia na maziwa miongoni mwa vitu vingine.
Pia huzingatia gharama nyingine muhimu kama vile mafuta ya petroli, umeme, sabuni na bei ya kukodi nyumba.
Ni bidhaa gani nyingine ambazo zinapata ruzuku ya serikali?
Huku ikikabiliwa na hali mbaya ya soko la mafuta ghafi duniani, Kenya imelazimika kutafuta mbinu za kudhibiti bei ya mafuta katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Wiki jana, serikali ilitangaza kuwa imetumia zaidi ya dola milioni 860 kuleta utulivu wa bei ya bidhaa hiyo nchini, kwa kuweka bei ya chini, na kulipa salio kwa makampuni ya uuzaji wa mafuta.
Hivi majuzi, serikali ilitoa ruzuku ya dola milioni 141. Fedha hizo zitatumiwa kupunguza bei ya mafuta katika mwezi Julai na Agosti. Bila ruzuku hiyo, lita moja ya petroli katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ingefikia dola 1.8, taarifa kutoka ofisi ya rais ilieleza. Kwa sasa, bidhaa hiyo hiyo inauzwa kwa $1.34, huku dizeli ikiwa bidhaa inayopewa ruzuku kubwa zaidi.
Nchi hiyo pia imefufua ruzuku ya gesi ya kupikia, na itatumia dola milioni 4.28 katika mwaka wa kifedha unaoanza mwezi Julai. Kwa sasa, Wakenya wanalipa Ksh 1,600 ($13.50) kujaza tena mtungi wa gesi wa kilo 6, na Ksh 3,400 ($28.69) kwa silinda ya kilo 13.
Je, ruzuku zina ufanisi gani?
Ruzuku za bidhaa, hata hivyo, zimekosolewa vikali na baadhi ya wataalamu wanaohisi kuwa bei zinapaswa kuamuliwa na soko huria.
"Haifanyi kazi," Nikhil Hira, mtaalam wa kodi huko Nairobi aliambia BBC.
"Lazima tuamue, je, sisi ni uchumi huria usio na udhibiti wa bei au tutachagua na kusema...sawa, tunahitaji udhibiti wa bei hapa."
Ruzuku hizo pia zimekosolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF. Shirika hilo limeeleza kuwa ruzuku hufadhiliwa na rasilimali za kodi za nchi, lakini hufaidi zaidi watu walio na uwezo wa kumudu bei ya kawaida.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Gharama ya maisha kuwa juu
Serikali ya Kenya imekusudia kuwa ruzuku zitapunguza gharama ya maisha nchini, ambayo imepanda juu zaidi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mfumko wa bei ulifikia 7.9% mwezi Juni, na kuzidi kiwango cha juu zaidi kilichowekwa na serikali cha 7.5%.
Hali hii imesababishwa na ongezeko kubwa la bei za mafuta, bidhaa za vyakula, pamoja na usafiri (nauli ya basi) miongoni mwa mengine.
Unga wa mahindi ni mfano. Pakiti ya kilo mbili ilikuwa na gharama ya chini ya dola moja, lakini sasa inauzwa kwa $1.77.














