'Wakati mwingine tunashinda bila chakula '

Baadhi ya familia zinakula mlo mmoja tu kwa siku, au hata kushinda siku nzima bila kula, kwasababu ya kupatanda kwa bei ya chakula , Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga ameandika kutoka Nairobi.
Mapema asubuhi, nilimpata Florence Kambua akisaka huku na kule kika dangulo la takataka nje mbele ya nyumba yake kukusanya plastiki, majani, nguo- chochote tu anachoweza kupata na kukiuza katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Kambua mwenye umri wa miaka 40 alikuwa amevalia sweta nyeusi na viatu vya buti za plastiki vya zilizofika kwenye mgoti. Kazi yake sio rahisi. Ni kazi hatari pia. Alikuwa akipita katika vyakula vilivyooza na nepi zenye uchafu katika makazi duni ya Mukuru Kwa Njenga.
"Wakati mwingine huwa napatwa na ugonjwa wa kuhara, wakati mwingine unapatya maambukizi ya kifua. Nimeweza kuvumilia, kwasababu sina njia nyingine ," Bi Kambua ananiambia.
Mama huyu wa watoto dsita amejipata katika hali ngumu kimaisha. Kwanza aliahamia Nairobi, mji mkubwa zaidi Afrika Msharaiki, miaka 19 iliyopita akitumai maisha yake yjayo yatakuwa mazuri.
Wakati huo alikosa kazi, baba wa watoto wake akamkimbia na kibanda kidogo cha kuuza chakula alichokua amekianzisha kilibomolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mwendo kasi inayopita katikati mwa jiji.
Kwahyo ni kazi gani atakayofanya ili kuweza kupata chakula. Hupata kaibu shilingi 100 za Kenya kwa siku (sawa na $0.85; £0.70).
Kwa kipato hicho cha chini Bi Kambua anasema angeweza kuilisha familia yake kabla ya bei za vyakula kupanda juu.
"Watoto wangu wanapenda wali, ningeweza kwenda dukani na kununua nusu kilo kwa shilingi 50 na kuwapikia. Sasa hivi huwezi."

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Bi Kambua amegeukia chakula kikuu kinachopendwa Kenya, unga wa mahindi unaotumiwa kupika Ugali ambacho kinaweza kushibisha lakini gharama ya bei ya unga pia imepanda .
Sasa anailisha familia yake mara moja kwa siku, na wakati mwingine hawalichakula kabisa "Nilikua nikinunua unga wa bei rahisi zaidi kwa sihilingi 85. Kwa sasa bei yake imepanda na kufikia hadi shilingi 150. Wakati ninaposhindwa pesa, tunalala njaa."
Wiki kadhaa baada ya kukutana , kuna habari mbaya zaidi kwa Bi Kambua, kwan wastani wa bei ya kilo mbili za unga wa ugali kwa sasa ni zaidi ya shilingi 200, ongezeko la 25% .
Data za hvi karibuni za Ofisi ya takwimu ya Kenya zinaonyesha kuwa ongezeko la bei chakula hadi 12.4% zaidi katika mwezi Mei 2022 kuliko ilivyokuwa mwezi Mei mwaka 2021.
Zao la mahindi ambayo hulimwa nchini Kenya na pia kununuliwa kutoka nchi jirani, ni chakula kinacholiwa na familia nyingi nchini Kenya.
Ni chaguo nafuu kwa wengi katika nyakati ngumu, lakini Kennedy Nyagah, Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya wasagaji wa nafaka , anasema kwa sasa kuna uhama wa bidhaa hiyo.
"Ninaweza kusema ongezeko la bei limetokana na ukosefu wa mavuno uliotokana na ukosefu wa mvua ya kutosha na matatizo kuhusu bei za bidhaa za kilimo kama vile mbolea," anasema.
Katika soko anakohemea Bi Kambua, biashara iko chini. Nilipotembelea mara mbili katika soko hilo, lilikuwa sio jambo la kushangaza kuwaona wateja wakinunua kitunguu au nyanya moja kwasababu gharama zake zimekuwa za juu.

Ingawa yuko mbali zaidi na Ukraine, anafahamu fika athari za vita kule na jinsi vilivyosababisha kupanda kwa bei ya mafuta na mbolea.
"Wakulima wanalazimika kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kununua mbole ya kukuza nyanya. Wengi wao wanaishia kuacha kabisa kilimo cha nyanya, kwasababu ya gharama ya mbolea na mbegu za nyanya ," Bw Nyabutohe ananiambia.
Mita mia kadhaa mbali na soko anaishi Bi Catherine Kanini – yeye hana ajira baada ya kufungwa kwa baa alikokuwa akifanyika kazi kubomolewa kwa ajili ya upanuzi wa barababara inayounganishwa barabara ya mwendo kasi.
Mama huyu mwenye umri wa miaka 30 hawezi kulipa gharama ya kodi ya nyumba, kwahiyo alijijengea mwenyewe kibanda kwa kutumia neti za kujikinga na mbu, vipande vya plastiki na mbao.
Alifika hapa kutoka Kaunti ya Kitui mashariki mwa Kenya na sawa na watu wengine wenye kipato cha chini katika maeneo ya mijini anategemea jamaa zake nyumbani wamsaidie wakakati bei za bidhaa zinapopanda.
Mama yake humtumia chakula kutoka kijijini, lakini ukame wa mud mrefu unamaanisha kuwa hawezi kufanya hivyo.
"Kwa sasa, hali ni ya ukame sana katika eneo la kijijini kwetu. Hakuna mvua. Inaponyesha ndio kunakuwa na chakula na mama yangu anaweza kunitumia chakula kiasi," Bi Kanini nanieleza. "kwa sasa anatutegemea sisi tumtumie kitu cha kula. Anatutegemea, huku na sisi tuna matatizo huku."

Kupanda kwa gharama za maisha kunakuja wakati ambapo Kenya inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 9 Agosti . Tatizo hiil limekuwa likijitokeza sana katika kampeni za wagombea wakuu wawili wanaotaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
Naibu wa Rais William Ruto anazungumzia kuhusu sera ya uchumi wa chini-juu "bottoms-up" ili kuboresha hali ya uchumi huku kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga ameahidi kuzipatia familia masikini pesa.
Bi Kanini ana ushauri wake binafsi kwao.
"Ningependekeza kwamba wafungue viwanda na kutupatia kazi. Wanapaswa kupunguza bei za bidhaa ambazo bei yake imeongezeka. Ili wakati unapoweza kupata pesa kidogo uweze kununua chakula."
Mchambuzi wa International Crisis Group Meron Elias anaonya kwamba mzozo wa gharama ya maisha unaweza kusababisha ukosefu wa udhabiti, hususan ni katika uchaguzi wenye ushindani mkali.
"Ingawa matokeo ya uchaguzi hayajulikani - tunahofia kuwa gharama ya juu ya chakula na hali mbaya ya kiuchumi kwa ujumla inaweza kutumiwa na wanasiasa kuwakusanya umati wa watu wanasikitishwa na hali hii kuingia mitaani. Pia inasababisha hatari kwamba vijana wasio na ajira wanaweza kuingizwa katika magenge ya kufanya ghasia wakati wa kipindi cha uchaguzi ."
















