Utafiti: Kwanini tausi dume hutoa sauti ya uwongo ya kushiriki tendo la ngono?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi wanasema tausi dume hutoa sauti kama anafanya ngono ili kumvutia tausi jike aliye mbali.
Watafiti kutoka Canada wanasema kuchezesha mkia wake pia ni sehemu ya kutoa mvuto wa kingo.
Tausi hutoa sauti za aina nyingi. Wana sauti tofauti kuendana na tabia fulani.
Wanabiolojia wamerekodi sauti hizo na kusema baadhi ya sauti wanazitoa ili kuvutia tausi jike.
Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la 'The American Naturalist'.
Kulingana na utafiti, tausi huonyesha kupitia sauti uwezo wao wa kujamiiana. Na hutoa mwaliko kwa tausi jike kupitia sauti vilevile.
Sauti maalumu ambayo tausi dume hutumia kuvutia tausi jike ni ile kali zaidi. Wanasayansi walijaribu kujua ni nini siri ya sauti hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dakt. Roslyn Deakin wa Chuo Kikuu cha British Columbia anasema, sauti hii ni kubwa zaidi kuliko ile inayohitajika ili kuwasilisha jambo, hii inaweza kusikika kwa umbali mrefu.
Kulingana na wanasayansi, aina maalumu ya hisia huwasilishwa kwa tausi jike kupitia sauti hii.
Dk. Roslin amechunguza makundi ya ndege hawa katika maeneo mengi. Alifanya utafiti katika mbuga za wanyama huko Amerika Kaskazini ambapo ndege hao wanaishi kwa uhuru kabisa na bila kudhibitiwa.
Katika makundi ya tausi, Roslin aligundua kwamba wakati tausi dume haoni tausi yoyote jike, ndipo hutoa sauti ya aina hiyo.
Anasema aina hiyo ya sauti ni ya kawaida kabisa kwa asilimia 60 ya tausi dume.















