Ndege adimu: Nusu jike, nusu dume amenaswa kwenye kamera

A bird seen from the front which has one half blue feathers and the other half green

Chanzo cha picha, John Murillo

Maelezo ya picha, Kuna ugunduzi mmoja tu kama huu katika kipindi cha zaidi ya miaka 100, kwamujibu wa watalaamu.

Kuna kitu cha kipekee kuhusu ndege huyu ambaye mtaalamu wa ndege John Murillo alikiona katika Hifadhi ya Mazingira ya Don Miguel huko Colombia, karibu kilomita 10 kusini-magharibi mwa jiji la Manizales.

Ndege mwitu aliyevutia macho yake - anajuulikana kama Green Honeycreepers. Upande wake wa kushoto - manyoya ni ya rangi ya kijani kibichi, rangi ya ndege majike wa spishi hiyo, na upande wa kulia manyoya ni ya buluu, ndege madume.

"Inafurahisha sana. Wapenzi wengi wa ndege huishi maisha yao yote na hawaoni ndege mwenye jinsia mbili. Kwa hivyo ni bahati sana kufaidika na ugunduzi wa John," anasema mtaalamu wa wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Otago, New Zealand, Prof Hamish Spencer.

Anasema, ni nadra sana ndege kuwa namna hiyo. Na hajui mfano wa ndege kama huyo katika nchi yake ya New Zealand.

Pia Unaweza Kusoma

Ni Nadra sana

A bird seen from behind which is one half blue and the other green

Chanzo cha picha, John Murillo

Maelezo ya picha, Majike kwa kawaida huwa na rangi ya kijana na madume rangi ya buluu

"Jinsia mbili ni hali ambayo upande mmoja wa kiumbe unaonyesha kuwa wa kiume na mwingine wa kike," Prof Spencer ameeleza katika makala iliyoandikwa pamoja na waandishi wengine na kuchapishwa katika jarida la Field Ornithology.

Ugunduzi huu ni mfano wa pili wa ndege mwenye jinsia mbili katika spishi hiyo katika kipindi cha zaidi ya miaka 100.

"Ndege wenye sifa dume na jike katika spishi ambayo kwa kawaida kuna dume na jike tu - ni muhimu ili kuelewa tabia za kujamiiana za ndege," Spencer anasema katika taarifa ya Chuo Kikuu cha Otago.

Je, inakuwaje ndege akawa hivyo?

"Tofautia ya kijinsia kwa ndege hutokana na muundo wa kromosomu au seli zilizo karibu, na sio kutofautiana kwa homoni katika miili yao," anasema profesa.

Hali hiyo iligunduliwa kwa wadudu, hasa vipepeo, wanya wenye maganda kama kaa, buibui na hata mijusi na panya.

Ndege kuwa na jinsia mbili, mtaalamu anasema hutokana na kosa wakati wa mgawanyiko wa seli - jike anapotoa yai, ikifuatiwa na kurutubishwa mara mbili na manii mawili."

Miezi 21 ya uchunguzi

Different angles of the rare bird

Chanzo cha picha, John Murillo

Maelezo ya picha, Picha tofauti za ndege huyo

Katika Hifadhi ya Mazingira ya Don Miguel, shamba lenye misitu na maeneo ya kulisha ndege. Ndege hupewa matunda na maji safi yenyee sukari. Mahali hapo ni pazuri kutazama ndege.

“Aina nyingi za ndege - zinaweza kuonekana katika makundi mchanganyiko kwenye malisho haya," waandishi wanaeleza katika makala yao.

“Ndege huyo wa kipekee aliyewavutia alikuwepo kwa miezi 21, na tabia yake kwa kiasi kikubwa ililingana na ile ya ndege wengine wa porini wa jamii ya Green Honeycreepers.

"Mara nyingi akisubiri hadi ndege wengine waondoke kabla nayeye kula matunda," wanaeleza wataalamu hao.

“Kwa ujumla, alijiepusha na ndege wa jamii yake, na ndege wa jamii yake pia walimuepuka. Yaonekana itakuwa tabu kwa ndege huyu kuwa na fursa ya kuzaa."

Hata ikiwa hataacha warithi, ukweli ni kwamba tayari ameacha alama yake kwenye ufalme wa wanyama.

Pia Unaweza Kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah