Mambo saba ambayo sayansi imefichua kuhusu viumbe wa ajabu

Chanzo cha picha, Emmanuel LaFont
Kwa miaka mingi, BBC Future imeangazia simulizi mbalimbali kuhusu jinsi maisha kutoka ulimwengu mwingine yanavyoweza kuwa, na nini athari ya kugundua viumbe vya ajabu vinaweza kuwa vipi.
Tunapoanza wiki ya makala maalum kuhusu viumbe wa ajabu - yote haya kuadhimisha miaka 60 ijayo ya mfumo wa maisha ya viumbe wa ajabu maarufu wa BBC, - tumechagua baadhi ya mambo ya ulimwengu usio wa kawaida.
Furaha yetu na maisha kutoka anga za juu
Mwezi, kama tunavyojua sasa, ni mahali pasipowezesha maisha ya binadamu. Lakini kabla ya wanaanga wa Apollo 11 kutua huko, hatukuweza kuwa na uhakika 100%.
Kwa kweli, kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba wanaume watatu kwenye misheni hiyo wangeweza kuleta mende wa anga la mbali duniani.
Wakati chombo cha Apollo kilipotua baharini baada ya safari yake kwenda kwenye mwezi, kulikuwa na taratibu kali za kuzuia uchafuzi ili kuzuia maisha kwa viumbe wa ajabu kuenea duniani.
Wanaanga walipaswa kukaa ndani, mlango ukiwa umefungwa, hadi walipoingia kwenye karantini.
Lakini kulikuwa na joto na hali isiyofurahisha, ikizunguka juu ya mawimbi, kwa hiyo waliruhusiwa kufungua mlango.
Ikiwa mende na mwezi wangeshikana katika safari hii, wangeweza kuchukua fursa hii kuingia Bahari ya Pasifiki. Kimsingi, ilithibitisha kuwa janga kwa maisha Duniani na kwa bahati kwetu, hilo halikufanyika.
Bahari iliyo kwenye Mwezi inawezakana kuwa mahali pazuri pa kupata viumbe wa ajabu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Aina kadhaa za Mwezi kutoka juu ya anga ndani ya mfumo wetu wa jua inaaminika kuwa na bahari kwa njia isiyo ya kawaida - yenye chumvi na kupashwa joto na hydrothermal. Sasa, wanasayansi wanafikiri bahari hizi za kwenye mwezi, pia zinaweza kuwa mahali pazuri pa kutafuta viumbe wa ajabu.
Mwezi wa Jupiter Europa, kwa mfano, unafikiriwa kuwa na maji mengi ya kioevu kuliko bahari zote za Dunia zikiunganishwa, huku mwezi wa sayari ya Zohali Enceladus ukitoa mifereji mikubwa ya maji ambayo huashiria matundu ya maji yanayotokana na maji kwenye sakafu ya bahari yake.
Ikiwa hizi zitathibitisha kuwa sawa na matundu ya kina kirefu ya bahari yanayopatikana Duniani, inaweza kuwa muhimu. Haya ndio ishara muhimu linapokuja suala la ambapo maisha duniani yanaaminika kuanza.
Mwezi aina nyingine nyingi yenye uwezekano wa kuwezesha maisha ni pamoja na Callisto ya Jupiter na Ganymede, na Titan ya Zohali.
Misheni kadhaa kuu za kwenye anga la mbali zinapangwa katika muongo ujao kutafuta vidokezo vya maisha katika bahari zenye viumbe wa ajabu. Lakini tunaweza kugundua maisha ya aina gani?

Chanzo cha picha, NASA/JPL/Space Science Institute
Kwa nini hatuko tayari kwa viumbe wa ajabu
Maisha kwa viumbe wa ajabu bado hayajagunduliwa, lakini ikiwa hivyo, je, tungelichukulia suala hilo kwa uzuri? Matukio ya kubuni hayajatoa matumaini mengi, huku viumbe vya ajabu vikifikiriwa kuwa kutofikia binadamu.
Hata miongoni mwa wakaaji binadamu waliopo katika sayari hii, haki za ulimwengu wote mara nyingi hazitekelezwi.
Hata hivyo, wanamaadili sasa wanazingatia kile ambacho kingetokea ikiwa mawasiliano ya viumbe wa ajabu yangewahi kufanyika.
Kuanzisha akili na hisia zao itakuwa hatua moja muhimu ya awali. Kuhakikisha nia yao itakuwa nyingine.
Na, haswa ikiwa tayari wana teknolojia ya kufika Duniani, tunaweza pia kuhitaji kuuliza kwa haraka ni haki gani ambazo watakuwa tayari kumpa binadamau kama malipo?
Sio ishara zote za " viumbe wa ajabu" zinatoka anga za juu
Wanaanga hutumia muda wao mwingi kutazama juu, wakichanganua anga la mbali kwa ishara zinazoweza kuwapa fununu kuhusu nyota za mbali, sayari na galaksi. Lakini wakati mwingine, wanahitaji pia kuweka chini vichwa vyao na kuangalia karibu na nyumbani.
Mnamo mwaka wa 1998, wanasayansi katika Kituo cha Australia cha Parke's Observatory huko New South Wales waligundua milipuko ya ajabu ya redio yenye urefu wa milisekunde chache ambayo iligunduliwa kwa wiki kadhaa. Cha ajabu, zilionekana kutokea tu wakati wa saa za kazi siku za wiki.
Kisha mwaka wa 2015, wanasayansi waliweza kufuatilia chanzo. Milipuko ilirekodiwa wakati watafiti walikuwa wakipasha moto chakula chao. Kufungua tanuri ya microwave kabla ya kuungua kulisababisha utoaji mfupi wa mawimbi ya redio ya karibu 2.4GHz ambayo yalichukuliwa na antena ya uchunguzi.
Kunaweza kuwa na viumbe kwenye Mirihi tayari

Chanzo cha picha, Nasa/Glenn Benson
Kabla ya kuzinduliwa, vyombo vya angani huwekwa safi sana ili kuepusha uchafuzi wowote wa viumbe ambao husafirishwa kutoka kwenye sayari yetu.
Mizunguko, wanaanga na vyombo vinawekwa pamoja katika vyumba safi na kufuata itifaki kali, ambayo ni pamoja na kuua vijidudu kila sehemu kabla ya kuunganisha.
Lakini haiwezekani kuweka vijidudu mbali na nyuso za chombo kabisa. Badala yake, huwekwa chini iwezekanavyo na inatumainiwa kuwa mazingira yasiyofaa katika anga yataua chochote kitakachosalia.
Viumbe vingine, hata hivyo, vimepatikana kuwa na uwezo wa kustahimili mchakato wa usafi na safari ya kwenda anga la mbali. Wanasayansi wamepata hata DNA kutoka kwa vijiumbe hivyo vyenye uwezo wa kustahimili mionzi, mazingira ya baridi, na utepetevu katika vyumba safi ambapo baadhi ya vyombo vya roboti vinazozunguka-zunguka kwenye uso wa Mirihi zilijengwa. Inazua swali - je, kunaweza kuwa na maisha katika sayari ya Mirihi?
Ongezeko kubwa la kuonekana kwa vitu visivyojulikana vikipaa (UFOs)
Wakati wa janga la Covid-19, wanasayansi waligundua hali ya kushangaza - kulikuwa na ongezeko kubwa la kuonekana kwa vitu visivyojulikana vikipaa (UFOs) kote Marekani. Wakiwa wamezuiliwa, ghafla watu walipata fursa ya wakati zaidi kutazama anga la usiku.
Je, macho hayo yote ya ziada labda yaligundua kitu ambacho tulikikosa hapo awali? Hii ilikuwa ni moja ya maelezo yanayowezekana.
Badala yake, katika matokeo ya utafiti, watafiti wanapendekeza maelezo mengine: umma ulikuwa ukitoa umakini zaidi kwa vitu vya kutiliwa shaka.
Tangu tathmini ya kwanza ya serikali ya Marekani ya UFOs mwaka 2021 - au matukio ya ajabu yasiyotambulika (UAPs) kama yanavyojulikana sasa - kumekuwa na ongezeko la kuonekana.
Mwaka jana pekee kulikuwa na zaidi ya 350 , ikilinganishwa na 144 kwa kipindi chote cha miaka 17 iliyopita. Baadhi ya wafafanuzi wamekita jambo hilo " enzi mpya ya UFO mania ". Nasa hivi majuzi ilianza kuchunguza ripoti hizi kwa mara ya kwanza.
Maisha kwenye Titan, lakini sio kama tunavyoijua
Takriban maili milioni 746 (km 1.2bn) kutoka Duniani, ni mwamba wa kushangaza, wenye maji maji mengi ya bahari na angahewa nene.
Ndani kabisa ya bahari hizi, vijidudu vinaweza kuchochea. Inafikiriwa kuwa mwezi mkubwa zaidi wa Zohali, Titan, unaweza kuwa na hali zinazofaa kwa maisha - katika bahari ya maji inayofikiriwa kuwa imefichwa chini ya ardhi na katika bahari inayojumuisha kioevy cha methane ambayo huosha uso wake.
Wazo moja ni kwamba Titan inaweza kuwa na "maisha ya vinyl" - seli zilizojengwa kutoka kwa sianidi inayopatikana katika angahewa yake. Sasa wanasayansi wanatarajia kupata majibu fulani. Nasa imependekeza kutuma manowari kuchunguza bahari ya methane kwenye ncha yake ya kaskazini, pengine wakati wa majira ya joto yajayo ya Titan mwaka wa 2047.














