Je hivi ndivyo viumbe wa ajabu wangeitawala dunia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama Sci-Fi na Hollywood blockbusters wametufundisha chochote, ni kuhusu wakati usioepukika utakapotokea uvamizi wa alien, itakuwa ni kelele, ukatili na kwa ujumla ni hali isiyofuharahisha kwa wengi wetu.
Vitu kama sauti za radi na ngurumo za mawingu Sauti za mawingu, na nyota za kung’ara vitatawala anga letu kuonyesha majuto kwa binadamu.
Lakini acha twende mbali na hayo kutoka kwa sayansi ya kufikirika na tuangalie sayansi yenye ushahidi halisi.
Ni nini kuhusu wanasayansi wakuu katika nyanja hii wanafikiria kuhusu uwezekano wa dunia kuvamiwa na alienu? Kuna ukweli gani kuhus kuwepo kwa alien? Je alien wangekuwa wanafananaje? Je ni mbinu gani ambazo wangetumia kujionyesha?.
Sayansi inachunguza uwezekano wa maisha yanayofanana na alien … na uwezekano wa shambulio.

Chanzo cha picha, © Mark Garlick | Getty
Je fursa ya uwezekano ipo kiasi gani?
Dunia yetu, inaning’inia katikati ya mfumo wa jua, ni nyota moja . Anga letu lina nyota bilioni 400 za ziada, zote zikifanya aina moja ya jambo, huku kukiwa na uwezekano wa sayari kama bilioni sita zinazofanana na dunia zinazozizingira.
Na unapoangalia huenda kukawa na nyota nyingine trilioni 2 duniani, kiasi hicho ni kingi cha namba kinachoweza kumfanya mwanamahisebu hata kulia.
Huku kukiwa na uwezekano wa kuwepo kwa maisha yanayozunguka kule angani, bila shaka kuna kiumbe kimojawapo kinachoishi huko? Na kama hilo linawezekana, je kama kiumbe hicho kina uwezo wa kuteketeza maisha kwingineko?.
Mwanasayansi na mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel mwanafizikia Enrico Fermi2 alishangazwa kwamba maisha ya alien hayajagunduliwa bado : Hakuna ushahidi wa kisayansi wa maisha ya ziada , lakini uwezekano wa kwamba huenda maisha yalikuwepo ni wa hali ya juu.

Chanzo cha picha, © Bryan Allen | Getty
Mnamo mwaka 1961, mtaalamu wa anga za mbali Frank Drake alibuni swali kukadiria idadi ya alien ambalo liko karibu nasi kuwahi kusikia kuanzia : N = RfpncflfifcL.4 Ukokotoaji wa karibu nasi , akitumia mbinu ya Drake Equation, inayoelezea kuwa huenda ikawa sio kweli kwamba sisi ndio viumbe wenye akili zaidi wanaoishi kwa asilimia 53 hadi 99.6.
Kuna mambo mengi yasiyojulikana ya kukokotoa kila kitu isipokuwa usahihi.
Kwahiyo, kwa ufupi ni kwamba huenda kukawa na viumbe wanaoishi wenye akili katika anga za mbali, au tunaweza kuwa ni sisi peke yetu.
Baadhi ya wanafizikia wa anga za juu wanaamini kuwa kunaweza kuwa na uumbwaji wa maisha katika sayari yetu ni tukio la ajabu ambalo haliwezi kurudiwa kokote kwingine.

Chanzo cha picha, © Victor Habbick Visions | Getty
Je viumbe wanaweza kuwa na ngozi ya kijivu na macho makubwa ?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini kama kuna viumbe nje ya sayari yetu, je vitaonekanaje? Sote tumesikua hadithi kuhusu hadidhi - hususan katika barabara za vijijini katika maeneo fulani ya Kati na kusini mwa Marekani – ambako elien walishuhudiwa wakiwa wanafanana . Wenye ngozi ya kijivu, macho makubwa, wasio na mtindo wowote wa mavazi kabisa.
Lakini je kuna ukweli wa alien kuwa na muonekano kama huu ?
Vitu vinavyounda maisha kwenye sayari yetu (nitrojeni, hydrogeni na Oksijeni) vimesambaa kote duniani. Kwahivyo, hii ingemaanisha kuwa , kama hali zinafanana kila mahali, maisha, kwa aina fulani, maisha ya viumbe yanaweza kujitokeza.
Hatahivyo, pia tunafahamu kuwa japo maisha katika sayari yetu yalianza mara baada ya kuundwa kwa dunia, yalibadilika kwa njia tofauti .
Wakati mmoja, kila mahali kuliwa na mkusanyiko wa viumbe waliojuklikana kama dinosaurs – lakini walipokufa, dinosaurs zaidi walijitokeza na kuchukua nafasi yao.
Badala yake aina mpya ya viumbe ilibadilika, ikionyesha kuwa hakuna aina moja ya maisha katika Dunia . Aina nyingi za viumbe wanaweza kuishi na kudumu katika sayari dunia, na kuwa tayari kufa na kutoweka.
Kwahivyo basi, maisha ya alien labda yangehitaji vitu vyote tunavyohitaji kuweza kuishi , kama vile nishati, kulindwa na mahasimu na njia ya kusafiri kutoka sehemu moja kuelekea nyingine – lakini zaidi ya hayo wangekuwa na muonekano tofauti.
Fikiria tu muonekano wa viumbe wa ajabu wanaoishi chini ya bahari ambao wanajongea na kutafuta chakula na kuepuka kuliwa lakini hawana muonekano kama wetu au kitu kingine.
Alien wote wangeweza kuonekana kama Vin Diesel, au kitu kingine ambacho ubongo wetu hata ohauwezi kukielezea.
Sawa na wasemavyo wanafizikia wengi wa angaza za mbali kuna majibu mengi sana, kuhusiana na uwezekano wa uwepo wa alien.














