Jinsi ya kudhibiti hamu ya kahawa wakati wa mfungo wa Ramadhan

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Manar Hafez
    • Akiripoti kutoka, BBC News Arabic
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Kukata mazoea ya kunywa kahawa kila asubuhi inaweza kuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya watu, kama ilivyo kwa Waislamu wengi wanaofunga wakati wa Ramadhani, ambapo wanajizuia kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jioni kwa muda wa mwezi mzima.

Lakini, kwa nini inakuwa vigumu kujizuia kunwa kahawa?

Je, kupenda kahawa kunaweza kusababisha uraibu unaoleta mkazo wakati wa kufunga?

Tutazame majibu ya wataalamu katika makala haya.

Kwanini ni vigumu kukata mazoea ya kunywa kahawa?

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

Hadithi inasema kuwa katika karne ya 9 BK, mchungaji mwenye asili ya Kiarabu alishtuka na tabia ya kundi lake la mbuzi baada ya mifugo hiyo kula mmea fulani.

Alipojaribu matunda ya mmea huo, ambao baadaye ulijulikana kama kahawa, aligundua kuwa ulimpa nguvu mwilini.

Kwa mujibu wa Encyclopedia Britannica, mimea ya kahawa ya mwituni ililetwa kutoka Ethiopia hadi Kusini mwa Arabia katika karne ya 15, ambapo ilianza kulimwa.

Hadi mwishoni mwa karne ya 17, Yemen ilikuwa chanzo kikuu cha usambazaji wa kahawa duniani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Leo hii, kahawa, inayotajwa katika mashairi kama "mpenzi mwenye ngozi nyeusi," imekuwa kinywaji cha kimataifa kinachotolewa moto au baridi na katika aina mbalimbali.

Kahawa ina kiasi cha kafeine kinachotofautiana kulingana na aina, kiasi, na njia ya maandalizi.

Hii ina maana kuwa kusitisha matumizi yake kunasababisha dalili za hali ya akili itokeayo kutokana na kuachishwa kitu ulichozoea, kama anavyoelezea mtaalamu wa lishe ya tiba, Faten Al-Nashash.

Kuhusu athari za kahawa kwa wale wanaofunga katika kipindi cha Ramadhani, Al-Nashash aliiambia BBC: "Sababu ya msongo wa mawazo kwa baadhi ya watu wanaofunga na kunywa kahawa ni dalili za kukosa kitu ulichozoeya zinazotokana na kusitisha matumizi ya kafeine."

Anaeleza kuwa "kujizoesha kuingiza kiasi cha kafeini kilichozoweleka katika mwili kupitia kahawa, iwe ni kiwango kikubwa au kidogo, na kuzoea kunywa kahawa kwa nyakati na kiasi fulani, kisha ghafla kuacha kunywa kahawa wakati wa kufunga husababisha dalili za kukosa kitu mwilini, kama vile maumivu ya kichwa na uchovu.

Kwa kuwa mwili pia unakutana na mfadhaiko mwilini kutokana na kufunga, hii husababisha msongo wa mawazo kwa baadhi ya watu."

Daktari wa magonjwa ya ndani na mshauri wa magonjwa ya moyo, Ghassan Kawar, anasema kuwa kufunga kula na kunywa hubadilisha mfumo wa mwili, na haoni tatizo la msongo wa mawazo au uchovu kuwa linahusiana na kahawa pekee.

Anasema kuwa mwili huzoea kufunga kadri Ramadhani inavyosonga mbele, na hivyo dalili zinazotokana na kuepuka chakula na vinywaji asubuhi hupungua.

Dkt. Kawar anasisitiza kuwa kafeine iliyomo katika kahawa ni "dawa yenye utata zaidi," kwani athari yake hutofautiana kwa watu tofauti.

Kwa mfano, inaweza kusababisha usingizi kwa baadhi ya watu, wakati wengine hawawezi kulala bila kunywa kahawa.

Hata hivyo, anashauri matumizi ya kahawa kwa kiasi, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

Daktari wa Neva Dkt. Babak Gharaei Moghaddam anaamini ukinywa kahawa iliyo na kafeine na kisha kuacha kwa sababu fulani ni sawa na kuacha kuvuta sigara, lakini kwa kiwango kidogo, lakini inahusishwa na uraibu na kuacha kubugia kahawa huleta maumivu ya kichwa ambayo hutofautiana kwa watu.

Lakini Muqaddam anaelezea BBC kuwa '' kuondoa uraibu wa kunywa kahawa hulingana na mtu binafsi.

Kwa mfano, iwapo mtu hunywa kiango kikubwa cha kahawa kuacha kwa siku au siku mbili au kwa wengine saa 4 ina madhara hasi.

Hata hivyo, sambamba na haya kunywa chai au kahawa haichukuliwi kama ni vibaya kama uvutaji sigara, ubugiaji pombe au kula dawa.''

Wakati huo huo anaeleza kuwa kunywa kahawa kuna faida kama vile husaidia kumakinika na humfanya anayekunywa kuwa mchangamfu na pia hutumika kutibu baadhi ya aina ya maumivu ya kichwa.

Kutokana na faida yake kafeine hupatikana kwa baadhi ya dawa zinazotumiwa kutibu kipandauso.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa kunywa kahawa kuna madhara hasi kwa usingizi, kwani inasababisha kurukwa na usingizi kwa baadhi ya watu.

Kwa vinywaji vya kuongeza nguvu ambavyo vina kiwango cha kafeine na huchangamsha baadhi ya neva kama vile Dkt. Muqaddam anasema athari zake hasi ni kubwa kwahivyo haipendekezwi kutumia kutokana na kuzidisha mapigo ya moyo.

Kliniki ya Mayo inaeleza: '' Kuacha mara moja kunywa kafeine kunasababisha dalili kama vile maumivu ya kichwa, uchovu, matatizo ya kumakinika na wasiwasi.Lakini dalili hizi hujitokeza na kupotea baada ya siku chache.''

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

Jinsi ya kuzoea ukosefu wa kafeini wakati wa mfungo wa Ramadhani?

Mtaalam wa lishe bora Al-Nashash anasema idadi ya vikombe vya kahawa unayokunywa inapendekezwa isizidi kila siku inahusiana na kiasi cha kafeini.

Anaeleza kiwango kilichopendekezwa cha kafeine kila siku kwa watu wazima kisizidi gramu 400- sawia na vikombe vinne.

Wajawazito au kina mama wanaonyonyesha hawawezi kunywa kahawa zaidi ya gramu 200 kwa siku.

Kwa watoto kati ya umri wa miaka 13 hadi 18, inapendekezwa wasizidishe kunywa kahawa gramu 100 kwa siku.

Lakini utumizi wa kafeine miongoni mwa watoto imekatazwa haswa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 12.

Al-Nashash anasema kuwa ni kosa kubwa kunywa kahawa pindi unapofungua saumu, na wakati muafaka wa kunywa kahawa wakati wa Ramadhan ni kusubiri hadi baada ya kufungua, kama saa moja au nusu ili kuepuka matatizo ya mmeng'enyo wa chakula iwapo utafuatanisha na kahawa.

Naye Dkt.Qawar anapendekeza kunywa kahawa wakati wa daku ili iingie mwilini polepole na hutohitaji tena mchana wakati unapofunga.

Mtaalam wa lishe Al-Nashash anashauri kupunguza kiwango cha kahawa unachokunywa siku kadhaa kabla ya mwezi wa Ramadhan.

''Ili kuzoesha mwili kutopata kahawa kutapunguza mfadhaiko wakati unafunga wakati wa Ramadhan bila changamoto yoyote, unapaswa kupunguza kunywa kahawa wiki mbili au siku 20 kabla ya Ramadhan.''

Anaongezea kwa kusema: '' Kwanza tunapaswa kujifunza kuchelewesha muda tunaokunywa kahawa.Iwapo tutaanza kuchelewesha kwa robo saa kila saa kwa siku 20 kabla ya Ramadhan, hii itasaidia mwiliktohitaji kafeine asubuhi.Kisha baadaye tupunguze kiwango cha kahawa tunachokunywa.''

Kulingana naye, hata kikombekidogo cha kahawa ambacho hupendelea kunywa wakati wa mapumziko au sherehe, ''kahawa ya kiarabu'' ina gramu 15 ya kafeine.

Japokuwa inakiwango kidogo cha kafeine tunapaswa kuwa waangalifu ni mara ngapi kwa siku tunakunywa kahawa.

Suluhu anayoielezakwa wapenzi wa kahawa ni: ''Kabla ya Ramadhan, wanawezakunywa kahawa isiyokuwa na kafeine.Kisha wakati wa Ramadhan, wanaweza kunywa kahawa kikombe kimoja kilicho na kafeine, na kuendelea na kahawaisiyona kafeine.''

Hata hivyo, Dkt.Moqaddam ambaye ameeleza athari zakuacha kunywa kahawa iliyo na kafeine kwa kauli yake anasema dini ya anayependelea kahawa itamsaidia na kuepuka wasiwasi anapoikosa.

''imani ya mtu ina athari kubwa kwa mfumo wa neva, na husaidia mwili kukubali mabadiliko yakutopata kitu kilichozoea.'' anasema.

Kliniki ya Mayo inashauri kubadilisha matumizi ya kahawa ni kwanza kutathmini viwango vya kafeine tunavyotumia kwa baadhi ya vinywaji na kuanza kunywa kahawa isiyo na kafeine.

''Kama wewe ni mpenzi wa kahawa, kafeine ni lazima kila siku,''anasema.

''Haitakuathiri kiafya lakini kuwa muangalifu na athari zake na kuwa tayari kupunguza kiwango iwapo utaona umefanya mazoea na kuwa kama uraibu.''

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid