Jinsi Ujerumani inavyojiandaa na uwezekano wa vita

h
Maelezo ya picha, Ujerumani imeidhinisha mswada unaoruhusu kuongezeka kwa uwekezaji katika Vikosi vya Wanajeshi wake
Muda wa kusoma: Dakika 6

Kombora lilifyatuliwa na kutimua wingu la vumbi la kahawia angani likielekea eneo la mstari wa mbele wa vita . Muda mfupi baadaye, askari wakaanza kuhesabu: "Tano, nne, tatu, mbili, moja... Fire!" roketi ikafyatuliwa angani.

Milipuko ya mazoezi haya ya mafunzo ya kijeshi ni ya mara kwa mara kiasi kwamba wakazi wa mji mdogo wa karibu wa Munster, Ujerumani , hawayaoni tena kama kitu cha ajabu.

Lakini maisha hapa sasa yamekuwa ya kelele zaidi.

Vikosi vya jeshi la Ujerumani, vinavyojulikana kama Bundeswehr, hivi karibuni vilipata vilipata ruhusa ya uwekezaji mkubwa baada ya bunge kuidhinisha muswada wa msamaha wa matumizi ya kijeshi kutoka ya kwa sheria kali za deni la taifa la nchi hiyo.

Mkuu wa ulinzi wa Ujerumani Jenerali Carsten Breuer aliiambia BBC kwamba kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi kunahitajika haraka kwani aliamini uchokozi wa Urusi hautakoma nchini Ukraine.

"Tunatishiwa na Urusi . Tunatishiwa na (Vladimir) Putin . Tunapaswa kufanya chochote kinachohitajika ili kukomesha hilo," Breuer alisema. Alionya kuwa NATO lazima iwe tayari kwa shambulio linaloweza kutokea katika miaka minne ijayo.

"Sio juu ya muda gani ninahitaji, bali ni muda gani Putin atatupa kuwa tayari," jenerali huyo anaongeza waziwazi. "Na kadiri tunavyojiandaa mapema, ni bora zaidi."

Uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine umebadilisha sana mawazo nchini Ujerumani.

Kwa miongo kadhaa, watu hapa wamelelewa kukataa nguvu za kijeshi, wakijua vizuri jukumu ambalo ililokuwa nalo Ujerumani hapo zamani kama mchokozi huko Ulaya.

"Tulianza vita viwili vya dunia. Ingawa imekuwa miaka 80 tangu kumalizika kwa Vita vya pili vuya dunia , wazo kwamba Wajerumani wanapaswa kujiepusha na mizozo bado liko katika vinasaba DNA ya watu wengi," anaelezea Markus Ziener wa shirika la misaada la German Marshall Fund lililopo Berlin.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine umeanza polepole kubadilisha mitazamo kuelekea vita vya Ujerumani
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wengine wanabaki na mashaka na chochote ambacho kitu chochoke cha kijeshi , na jeshi limekuwa na ufadhili mdogo wa muda mrefu.

"Kuna sauti zinazoonya: 'Je, kweli tuko kwenye njia sahihi? Je, mtazamo wetu wa tisho ni sahihi?'

Kuhusiana na Urusi, Ujerumani imechukua njia maalum.

Wakati nchi kama Poland na majimbo ya Baltic zilionya dhidi ya kukaribia sana kwa mashambulizi ya Moscow - na kuongeza matumizi yao ya ulinzi - Berlin, chini ya Kansela wa zamani Angela Merkel, iliamini kufanya biashara.

Ujerumani ilikuwa nchi tulivu, lakini baada ya kushuhudia Urusi ikiivamia Ukraine, mwezi Februari ,2022, Kansela Olaf Scholz, akiwa ameduwaa kwa kiasi fulani, alitangaza mabadiliko ya kitaifa ya vipaumbele, "Zeitenwende".

Hapo ndipo alipoahidi kuwekeza euro bilioni 100 ($ 120 bilioni) kuimarisha vikosi vya jeshi la nchi hiyo na kudhibiti "wachochezi wa vita kama Putin". Lakini Jenerali Breuer anasema hiyo haitoshi.

"Tumejaza mapengo kidogo," anasema. "Lakini hali ni mbaya sana."

g
Maelezo ya picha, Jenerali Carsten Breuer anaamini Ujerumani itahitaji kuongeza kwa kiasi kikubwa viwango vya wanajeshi

Anayataja matumizi makubwa ya Urusi ya silaha na vifaa, ya wapiganaji wa akiba na wa mstari wa mbele nchini Ukraine.

Pia anaangazia vita vya mseto vya Urusi: kutoka kwa mashambulizi ya mtandao hadi hujuma, pamoja na ndege zisizo na rubani zisizojulikana juu ya mitambo ya kijeshi ya Ujerumani.

Zaidi ya hayo Jenerali Breuer, anayataja matamshi makali ya Vladimir Putin, ambayo anayaona kama "mchanganyiko hatari sana."

"Tofauti na ulimwengu wa Magharibi, Urusi haifikirii kwenye mambo madogo. Sio juu ya wakati wa amani.

Anasema kuwa Ujerumani inahitaji kuchukua hatua haraka.

Mufanya 'machache kwa kila kitu'

Tathmini ya wazi ya mkuu wa ulinzi kuhusu hali ya sasa ya vikosi vyake inaambatana na ripoti ya hivi karibuni iliyowasilishwa bungeni. Bundeswehr, maandishi yalihitimisha, ilikuwa na "mambo madogo kwa kila kitu."

Mwandishi wa ripoti hiyo, Kamishna wa Vikosi vya Wanajeshi Eva Högl, alifichua uhaba mkubwa, kuanzia risasi hadi askari hadi kambi zilizochakaa. Alikadiria bajeti ya kazi ya ukarabati pekee kuwa karibu euro bilioni 67 ($415 bilioni).

Kusitisha ukomo wa deni, ili kuruhusu jeshi kukopa - kwa nadharia, bila kikomo - kutatoa ufikiaji wa ukomo wa ufadhili utakaosaidia kuanza kushughulikia tatizo hilo, kulingana na Jenerali Breuer.

Mpango huo wa kihistoria uliharakishwa na Friedrich Merz anayetarajiwa kumrithi Scholz, jambo ambalo liliwashangaza wengi . Aliwasilisha pendekezo hilo kwa Bunge muda mfupi kabla ya kuvunjwa kufuatia uchaguzi wa Februari.

Bunge jipya, la mrengo wa kushoto unaopinga wanajeshi na mrengo mkali wa kulia ambao unaihurumia Urusi, linaweza kuwa lisilofaa.

Lakini "mabadiliko" ambayo Ujerumani ilianza mnamo 2022 yalipata kasi mpya mwaka huu.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wajerumani sasa wanazidi kuwashuku marais wa Urusi na Marekani

Kura ya hivi majuzi ya YouGov ilionyesha kuwa 79% ya Wajerumani bado wanamwona Vladimir Putin kama hatari "sana" au "kabisa" kwa amani na usalama wa Ulaya.

Na sasa , 74% ya Wajerumani walisema vivyo hivyo kumhusu Donald Trump.

Kura hiyo ilipigwa baada ya hotuba huko Munich ambapo Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aliishambulia Ulaya na maadili yake.

"Hii ilikuwa ishara ya wazi kwamba kuna kitu kimebadilika kimsingi nchini Marekani," anasema Markus Ziener.

"Hatujui Marekani inaelekea wapi, lakini tunajua kwamba imani kwamba tunaweza kutegemea asilimia 100 juu ya ulinzi wa Marekani katika suala la usalama wetu - uaminifu huo sasa umetoweka."

Kuacha nyuma Historia

Huko Berlin, tahadhari ya jadi ya Wajerumani kuhusu maswala yote ya kijeshi inaonekana kutoweka haraka.

Charlotte Kreft, 18, anasema mtazamo wake kuhusu ushirikiano wa pasific umebadilika.

"Kwa muda mrefu, tulihisi kuwa njia pekee ya kufidia ukatili tuliofanya katika Vita vya Pili vya Dunia kuhakikisha kuwa havitokei tena [...] na tulihisi tunahitaji kuondoa jeshi," Charlotte anaelezea.

"Lakini sasa tuko katika hali ambayo tunapaswa kupigania maadili yetu, demokrasia na uhuru. Tunahitaji kuzoea."

"Wajerumani wengi bado wanaona ni ajabu kwamba tunawekeza sana katika vikosi vyetu vya jeshi," anakiri Ludwig Stein. "Lakini nadhani kwamba, kutokana na kile kilichotokea katika miaka ya hivi karibuni, hakuna chaguo jingine halisi."

 Charlotte na Ludwig anaona kuna haja ya kuongeza matumizi ya ulinzi nchini Ujerumani
Maelezo ya picha, Charlotte na Ludwig anaona kuna haja ya kuongeza matumizi ya ulinzi nchini Ujerumani

Sophie, mama mwenye umri mdogo, anaamini kwamba kuwekeza katika ulinzi ni "muhimu katika ulimwengu tunaoishi."

Lakini Ujerumani inahitaji askari pamoja na mizinga, na havutiwi sana na mtoto wake mwenyewe kuandikishwa jeshini.

'Uko tayari kwa vita?'

Bundeswehr ina kituo kimoja tu cha kudumu cha uandikishaji, kitengo kidogo kilichowekwa kati ya duka la dawa na duka la viatu karibu na kituo cha Friedrichstrasse cha Berlin.

Kituo hicho kinalenga kuvutia wanaume na wanawake kwenye utumishi wa kijeshi, lakini hupokea wageni wachache tu kwa siku.

Ujerumani tayari imekosa lengo lake la kuongeza safu yake kwa wanajeshi 20,000 hadi 203,000 na kupunguza wastani wa umri hadi 34.

Lakini matarajio ya Jenerali Breuer ni makubwa zaidi.

Anasema Ujerumani inahitaji wanajeshi 100,000 wa ziada ili kujilinda yenyewe na kwa ajili ya NATO wanajeshi 460,000, pamoja na askari wa akiba. Ndiyo maana anasisitiza kuwa kurudi kwenye utumishi wa kijeshi ni "muhimu" kabisa.

g
Maelezo ya picha, Ujerumani ilisimamisha utumishi wa lazima wa kijeshi kwa wanaume mnamo 2011

"Hutapata wale 100,000 bila mfano fulani wa utumishi wa lazima wa kijeshi," jenerali huyo alitangaza.

"Hatuhitaji kuamua sasa mtindo huo utakuwa nini. Kwangu mimi, ni muhimu tu tupate askari."

Mjadala huu ndio kwanza unaanza.

Jenerali Breuer yuko mstari wa mbele katika harakati za kukuza "mabadiliko" ya Ujerumani kwa haraka zaidi.

Kwa njia yake rahisi na ya kuvutia, anafurahia kutembelea kumbi za miji ya mkoa na kutoa changamoto kwa umma kwa swali moja: "Je, uko tayari kwa vita?"

Siku moja, mwanamke alimshtaki kwa kumtisha. "Nikasema, 'Sio mimi ninayekutisha, ni yule mtu mwingine!'" anakumbuka jibu lake.

Alikuwa akimaanisha Vladimir Putin.

"Wito wa mwamko" mara mbili - wa tisho kutoka Urusi na Marekani sasa unasikika kwa sauti kubwa nchini Ujerumani, jenerali anasema, na hauwezi kupuuzwa.

"Sasa unaeleweka kwa kila mmoja wetu kwamba tunapaswa kubadilika."