Shinikizo la kupunguza uzito baada ya kujifungua

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Sasa rudisha mwili wako wa zamani haraka’. ‘Kuwa kama ulivyokuwa awali." Wanawake wengi husikia maneno haya mara nyingi baada ya kujifungua. Mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko mengi wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Iwe ya kimwili au kiakili.

Mara tu baada ya kuzaliwa kwa binti yake wa kwanza mnamo 2012, jamaa walianza kumwambia Shreya Singh (ambalo ni jina bandia) "usile sana, utaongezeka uzito."

Baada ya kujifungua, uzito wake ulikuwa kilo 25 zaidi ya uzito wa kabla ya ujauzito.

Shreya ni mama wa watoto wawili. Binti yao wa kwanza alizaliwa mwaka wa 2012 na binti wa pili mwaka wa 2021. Alijifungua watoto wake wote wawili kwa njia ya kawaida.

'Usile kupita sana, utaongeza uzito'

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Akizungumza na mwandishi wa BBC Payal Bhuyan, Shreya anasema kwamba baada ya kuzaliwa kwa binti yake wa kwanza, alikuwa akisumbuliwa na matatizo mengi ya kimwili.

"Ikiwa ungeniona kwa macho, ungefikiri nilikuwa sawa," anasema. Lakini haikuwa hivyo. Nilikuwa nimeongezwa njia sana wakati wa kujifungua na kidonda kilichukua muda mrefu kupona. Wakati huu pia nililazimika kukabiliana na shinikizo. Ilikuwa uchungu sana. Hali yangu ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba nilikuwa nikitetemeka nikifikiria kwenda chooni."

Pamoja na hayo yote, Shreya pia alikuwa na maumivu mengi kwenye sehemu yake ya chini ya mgongo. Anasema kwamba wakati akipambana na haya yote, wakati watu wange "Usile sana, punguza uzito', mara nyingi hakuwa na jibu.

Hata hivyo, Shreya hakukumbana na ugumu mwingi katika kujifungua binti yake wa pili kama vile wakati wa kuzaliwa kwa binti yake wa kwanza. Mara ya pili alikuwa tayari amejitayarisha kiakili zaidi.

Matatizo ya kimwili na kiakili

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini hata ikiwa mwanamke hana matatizo haya yote baada ya kujifungua, mabadiliko mengi hutokea katika mwili wakati na baada ya ujauzito. Kwa mfano, unapitia mabadiliko mengi ya homoni kwenye mwili wako ili kudumisha uhifadhi wa mafuta.

Kadiri sehemu ya fupa la nyonga inavyopungua, virutubisho kutoka kwa mwili wa mwanamke anayenyonyesha hupitisha maziwa hadi kwa mtoto. Yote hii ina maana kwamba inachukua muda kwa mwanamke yeyote kurejesha mwili wake kuwa kawaida baada ya kujifungua.

Akizungumza na mwandishi wa BBC Payal Bhuyan, daktari Karnika Tiwari, wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya kinamama huko Noida, karibu na Delhi, anasema kuwa kuna matatizo mengi wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ambayo wanawake wengi wanapaswa kukabiliana nayo.

"Wakati wa ujauzito, kibofu cha mkojo huwa na shinikizo la kukidhi kijusi kinachokua," anasema. Kibofu kiko mbele ya tumbo la uzazi na matumbo yako nyuma yake. Mara nyingi, wakati kuna shinikizo zaidi kwenye kibofu, kutoweza kujizuia mkojo na wakati mwingine bawasiri yaani hemorrhoids hutokea.

"Wakati huo huo, kunapokuwa na shinikizo kwenye matumbo nyuma ya tumbo la uzazi, asidi huwa juu sana au kunaweza kuwa na malalamiko ya kuvimbiwa."

Dk. Karnika Tiwari anasema inaweza kuchukua wiki sita hadi nane kwa tumbo la uzazi kurejea ukubwa wake wa kawaida baada ya kujifungua. Katika kipindi hiki, wakati mwingine maumivu ya tumbo pia hutokea. Wanawake wengi wana nguvu kidogo kukabiliana na hili na huwa wanahisi uchovu haraka mno.

Anasema kwamba nafasi ya mifupa katika mwili hubadilika wakati wa ujauzito. Baada ya kujifungua, mifupa huanza kurejea tena mahali pake hatua kwa hatua. Kutokana na hili, wanawake wengi pia wanakabiliwa na maumivu ya mgongo. Mara nyingi, shida hii inaweza kudumu milele.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Unaanza kuonekana kama ulivyokuwa. "

Akizungumza na BBC Future, Sharon Oakley, anayeishi Yorkshire, Uingereza, anasema kwamba mnamo mwaka 2018 "baada ya kujifungua, watu walianza kuniambia ndani ya miezi michache. Lo! Unaanza kuonekana kama hapo awali."

Ingawa Sharon alionekana kurudi katika hali yake ya awali kimwili, ukweli ulikuwa tofauti.

Baada ya kujifungua, alikuwa amepungua uzito lakini kimwili alikuwa akipitia kipindi kigumu sana.

Alipata tatizo la kushindwa kujizuia mkojo.

"Inahuzunisha sana kwa jamii zetu kuhukumu kipindi cha mwanamke baada ya kujifungua kwa jinsi anavyoonekana badala ya anavyohisi," anasema Sharon.

Anaongeza kuwa alionekana sawa lakini bado anapambana na majeraha au mabadiliko ambayo yametokea kwenye mwili wake baada ya kujifungua.

Baada ya miezi kadhaa ya vipimo na ushauri wa kimatibabu, ilionekana wazi kuwa misuli ya Sharon ya fupa la nyonga ilikuwa dhaifu sana baada ya kujifungua na haikuwa katika hali yake ya kawaida. Kutokana na hilo alikuwa anakabiliwa na tatizo la kibofu kupitisha mkojo.

Sasa miaka mitano baadaye, hali inaendelea kuimarika. Lakini bado wakati mwingine anakabiliwa na tatizo la kuvuja kwa mkojo. Kwa hivyo hubeba chupi za ziada kila anapotembea. Sababu ambayo mara nyingi ilimfanya alifikirie kuacha kazi yake.

Wanawake ambao wanakabiliwa na matatizo hayo si lazima waonyeshe dalili yoyote baada ya kujifungua.

Pia theluthi moja ya wanawake wanakabiliwa na tatizo la kushindwa kuzuia mkojo ambalo linaweza kusababishwa na mvutano katika eneo la fupa la nyonga, kuumia kwa misuli au mishipa.

Aidha, baada ya kujifungua, mwanamke anaweza kukabiliwa na ugumu wa kutembea na kuinua vitu vizito.

Mfadhaiko wa kimwili kabla ya ujauzito

Akiongea na mwandishi wa BBC Payal Bhuyan, Dkt Bhavana Burmi, mwanasaikolojia mkuu katika Taasisi ya Forts Heart, Delhi, anasema kutarajia mama aliyejifungua mtoto wa kwanza kuwa na ngozi sawa na hapo awali kunaweza kuwa na athari kubwa kwa afya yake ya akili. Inaweza, pia, kuwa na athari mbaya ya kihisia kwake.

"Wanaanza kujisikia hawajakamilika, ambayo inaweza kusababisha kuchanganyikiwa, kujichukulia kuwa duni, huzuni na hata msongo wa mawazo, Daktari Burmi anasema.

Mara nyingi wanawake huanza kula chakula na kufanya mazoezi mengi ili kupata mwili wao wa kabla ya ujauzito. Lakini yote haya huathiri uwezo wa mwili kujiponya. Inaweza kuathiri mama na mtoto.

Chini ya shinikizo hili mara nyingi wanawake hujitenga na jamii. Anaanza kuona aibu juu ya mwili wake.

Hali hii inaweza kuongeza upweke kwa wanawake.

"Shinikizo la kurudi haraka kwa mwili wa kabla ya ujauzito linaweza kuongeza mfadhaiko kwa mama aliyejifungua," anasema Dk Bhavana Burmi.

Tunapaswa kuelewa kuwa "mwili wa kila mwanamke na kasi ya kupona ni tofauti."

.

Chanzo cha picha, Getty Images