Kwanini hamu ya kula wakati wa ujauzito ni changamoto?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sote tumewahi kusikia kuhusu simulizi za wanawake wajawazito kutaka kula aisikrimu na achari pekee, kuna wale wanaowatuma waume zao saa saba usiku kwenda kutafuta kuku wa kukaanga, ambao wana hamu sana ya kula chokoleti za aina fulani.
Pengine hata sisi wenyewe tushawahi kuwa na hamu za kiajabu ajabu aina hii.
Mara nyingi huwa inakisiwa kwamba hamu zingine wakati wa mimba huwa na madini muhimu yanayohitajika mwilini kwa mama au kujusi.
Hata hivyo, wakati mwingine huwa inachanganya.
Kubeba ujauzito kwenyewe ni muda mrefu, kunakochosha na wakati mwingine inakuwa kero na ikiwa kutakuwa na sababu ya kula kipindi hicho basi hiyo ni habari njema.
Hata hivyo, unapoangalia mtazamo wa utafiti wa kisayansi kuhusu suala hili, mambo yanayojitokeza ni ya kivutia zaidi.
Kutamani mchele
Wanawake wajawazito kuwa na hamu ya kitu fulani, sio kwamba ni kuna ambatani na utamaduni fulani, watafiti wamebaini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa wale ambao sio wazungumzaji wa Kiingereza ambako wakati mwingine wanawake wanasemekana kuwa na hamu ya kula kitu fulani, ni tofauti sana na Marekani, na Uingereza.
Kwa mfano kwa wanawake nchini Japani, imegulika kuwa utafiti huo pia, umeangalia ikiwa vyakula hivyo ambavyo wanawawake wa mimba hula husaidia mwili kwa madini fulani muhimu kipindi cha ujauzito na kubaini kwamba sio vyanzo vizuri.
Ladha ya chokoleti
Imesemekana kwamba, wanawake ambao wamekuwa na hamu ya kila kitu fulani wameonekana kuongeza uzito kuliko ilivyokawaida wakati wa ujauzito ambako kunaweza kuongeza hatari ya kupata matatizo.
Hilo halimaanishi kwamba wanawake wenye hamu ya kula hujifanyisha, lakini huenda hamu hiyo inachochewa na kitu tofauti mbali na virutubisho muhimu mwilini.
Lakini kuangalia kwa ujumla vyakula ambavyo watu hutamani kunaweza kufanya baadhi ya taarifa hizo kuanza kuangaziwa, amesema Julia Hormes, profesa wa saikolojia chuo kikuu cha New York, Albany, ambaye amesomea suala hili kwa misingi mbalimbali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mfano asilimia 50 ya wanawake Marekani hutamani sana chokoleti wiki kabla ya kuingia kwenye siku zao za hedhi, amesema Hormes.
Wanasayansi wamekuwa wakifuatilia kujua ikiwa hamu ya kula chokoleti ni kwa sababu ya virutubisho muhimu wakati wa hedhi
Katika jaribio moja, mwanasaikolojia aliwataka wanawake wafungua makasha na kula kilichomo wakati mwingine watakapokuwa na hamu ya kula kitu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya makasha yalikuwa na chokoleti za maziwa.
Makasha mengine yalikuwa na chokoleti nyeupe ambayo haina kakao ngumu inayofanya maziwa na chokoleti iliyokolea rangi lakini ina muonekano mzuri.
Na hatimae, makasha mengine yalikuwa na dawa zilizotengenezwa kwa kakao na virutubisho vya kakao ngumu.
Hata hivyo utafiti mwingine umeonesha kwamba kutamani kula kakao hakuna uhusiano wowote na kiwango cha homoni mwilini.
Na kama haitoshi, baadhi ya wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, bado wanaendelea kuwa na hamu ya kula.
Pale unapojihukumu kwa chakula unachokula
Ainasemekana kwamba vyakula anavyokula mama mjamzito wakati mwengine vinamfanya awe ni mwenye kuhisi amefanya makosa yaani kujihukumu.
"Nakita kweli, lakini sistahili kukila - tunafikiria kwamba utamaduni huu unahamasisha hamu ulio nayo," ameongeza.
Hususan, ikiwa umeshajiwekea kwa muda na kujiambia akili hutakula chakua fulani - inakuwa vugumu kujidhibiti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa hiyo unakula kipande cha keki badala ya kutosheka na kusonga mbele, unakula vipande vitatu zaidi.
Pia wanawake wanaweza kujiwekea kutokula chakula fulani wakati wa ujauzito, ama kwa sababu za kiafya au kwa maelekezo ya daktari.
Je ujauzito ni tiketi ya kula chochote utakacho?
Ujauzito pia unaweza kuonekana wakati mwingine kwamba kwa hali hiyo kula aina fulani ya kitu sana watu watachukulia sawa.
"Utamaduni huu unaonekana unafanya wanawake wengi kula vitu ambavyo hawakustahili," Hormes amesema.
Hormes anashauri kina mama ikiwa utatamani kuma chokoleti, basi upate ambayo itaongeza virutubisho muhimu ndani ya mwili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Thamani ya mjamzito kupata alicho na hamu nacho
Kitu kingine ni kifuatilia kwa makini na kujali hamu ya kitu unachotaka kula na kujitahidi kipite tu.
Linapokuja suala la mwanamke mwenye mimba na hamu ya vitu anavyotaka kula, huenda kukawa na mengine yanayochochea pengine ndivyo mimba hiyo inavyotaka na hivyo basi kuwa vigumu kujidhibiti.
Utafiti mmoja uliofanywa sehemu ya vijijini Tanzania, wanawake waliosema kuwa wana hamu ya kitu fulani, nyama, samaki, nafaka, matunda na mbogamboga ilionesha kwamba kupata wanachotaka ni njia moja ya mume pamoja na familia kuonesha kuwa wanajali.
Ukweli ni kwamba kumtuma mtu saa saba usiku akanunue kuku wa kukaang'a na akuletee, kunaonesha kwamba mtu huyo yuko kwa ajili ya mke wake mja mzito.
Hata kama chakula ni kitamu, ukweli wa kwamba mtu unayempenda amekuletea chakula hilo linaonesha thamani kubwa sana.












