Fahamu fukwe bora za bahari duniani mwaka 2023

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fukwe ya bahari ya Baia do Sancho , huko fernando de Noronha nchini Brazil imetangazwa kuwa fukwe bora ya bahari duniani 2023 kulingana na mtandao wa Utalii wa Tripadvisor.

Fukwe ya bahari ya Baia do Sancho , huko fernando de Noronha nchini Brazil imetangazwa kuwa fukwe bora ya bahari duniani 2023 kulingana na mtandao wa Utalii wa Tripadvisor.

Fukwe nyingine nne katika eneo la Amerika ya Kusini, ni pamoja na Varadero huko Cuba, Manuel Antonio huko Costa Rica, Ipanema huko Rio de Janeiro na Playa Norte huko Mexico - pamoja na fukwe nyengine kadhaa katika eneo la Caribbean - zimeingia kwenye orodha ya 25 bora zaidi duniani iliyochapishwa mwaka huu.

Orodha hiyo ya kila mwaka ya Tripadvisor inazingatia wingi na ubora wa hakiki na ukadiriaji uliotolewa na watalii kati ya Januari 1 na Desemba 31.

Uteuzi huo ulifanywa kutoka kwa makumi ya mamilioni ya maoni yaliyowasilishwa na mamilioni ya wasafiri wa kimataifa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ili kubaini fuo zinazopendwa sana na watalii mwaka huu.

Ulijumuisha mabara ya Amerika, Afrika, Ulaya, Asia na Pasifiki ya Kusini. Fukwe maarufu hutoa kitu kwa kila aina ya mgeni, kutoka jua hadi wale wanaotafuta kujitosa katika asili.

Mchanga wa dhahabu, ukanda wa pwani wenye miamba na maji ya buluu ya fuwele, fukwe zilizoshinda mwaka huu ni kipenzi cha watalii kwa kufanya kila kitu kutoka kulala katika mchanga hadi ujio wa chini ya maji, ni jinsi tovuti inaelezea vigezo ambavyo vilizingatiwa.

Ni nini kinachofanya Baía do Sancho kuwa maalum?

Tripadvisor inautaja ufukwe wa bahari wa Baía do Sancho kama "Ufuo mzuri wa mbali ambao unaweza kufikiwa tu kwa kushuka ngazi zilizopo katika mawe. Mwamba uliopo kando kando ya ufukwe huo utakufurahisha.Maporomoko ya ajabu yatakutoa pumzi."

Kwa upande wake, chapisho la kitalii la Lonely Planet linasema kwamba Baía do Sancho ni "sehemu ya mchanga yenye kuvutia zaidi kwenye kisiwa cha fuo nzuri" .

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baía do Sancho ndio "eneo bora" la ufuo katika visiwa vya Fernando de Noronha.

Ufukwe huo upo katika visiwa vya Fernando de Noronha. karibu kilomita 350 kutoka pwani ya Brazili, ambayo inaweza kufikiwa kwa mashua au ndege. Bado unachukuliwa kuwa kivutio cha watalii tu kwa watu wachache, kwa kuzingatia ugumu wa ufikiaji.

Hata hivyo, idadi ya watalii wanaotembelea visiwa vya Fernando de Noronha imekuwa ikiongezeka. Mnamo 2022, rekodi ya idadi ya watalii waliotembelea visiwa hivyo ilivunjwa ikiwa ni watalii 149,000, 30% zaidi ya mwaka uliopita.

Kwenye Tripadvisor, kuna maoni zaidi ya 8,700 kutoka kwa watumiaji wa Intaneti kuhusu Baía do Sancho.

"Ufuo huu ni wa kustaajabisha. Muonekano wake, maji na viumbe vya baharini unapofika ni vya ajabu," anaandika mmoja wa watumiaji wa tovuti hiyo.

Lakini wengine hawakubaliani.

"Sancho inakatisha tamaa, kwani kila mtu anasema ni ufuo bora zaidi duniani. Na umejaa watu," mtalii mwingine aliandika kwenye Tripadvisor.

Fukwe zingine zilizochaguliwa

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchanga mweupe wa Varadero, Cuba umekuwa juu kwenye orodha.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Fuo za Carrebean zinashikilia nafasi tatu kati ya kumi bora kwenye orodha ya 2023. Ufukwe wa Eagle wa Aruba umeshika nafasi ya pili, Ufukwe wa Visiwa vya Turks na Caicos' Grace Bay unashika nafasi ya tano, na Ufukwe wa Diamond unashika nafasi ya tisa.

kutoka Varadero huko Cuba.

Varadero aulielezewa na mtumiaji mmoja kama "Postcard perfect. Maji ni bluu ya ndani zaidi ambayo nimewahi kuona na mchanga kama unga mweupe. Mwaka jana, Varadero iliorodheshwa ya pili duniani.

Katika Amerika ya Kusini, fukwe za Manuel Antonio huko Costa Rika pia zilijitokeza, kutokana na "mawimbi yao machache, yanayoelea, ile ya Ipanema "safari ya kwenda Rio de Janeiro haikamiliki bila ufuo huu"; na Pwani ya Kaskazini huko Mexico ambayo ndio "kiini cha Paradiso" .

Sio tu mchanga wa kitropiki ulioingia kwenye orodha ya watalii. Maeneo ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa ya kutisha zaidi, kama vile ufuo wa Reynisfjara huko Iceland, na mapango yake, nguzo za basalt na mchanga mweusi, zilisajiliwa kati ya bora zaidi.

"Unahisi kama umenaswa katika ndoto. Mahali hapa hukufanya usahau kuhusu wakati," ilikuwa mojawapo ya maoni kuhusu ufuo huu ulioshika nafasi ya nne.

Mbali na Reynisfjara, fuo zingine zilizochaguliwa barani Ulaya ni pamoja na Praia da Falésia huko Olhos de Agua, Ureno, Spiaggia dei Conigli huko Sicily, Italia, na La Concha na Muro huko Uhispania.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mapango, nguzo za basalt na mchanga mweusi wa Reynisfjara hukufanya uhisi "umeshikwa katika ndoto".

Nungwi, Zanzibar

Zanzibar ikiwa katika pwani ya mashariki ya Afrika, inajivunia historia yake ya kupendeza kama kituo muhimu cha biashara wakati wa biashara ya viungo ya karne ya 16 hadi 17. Kisiwa cha Tanzania bado kinajivunia uzalishaji wake wa viungo kama vile karafuu na mdalasini lakini pia kimekuwa kivutio kinachokuja kwa kasi kwa wasafiri wa pwani.

Miongoni wa orodha hii ni fukwe maarufu ya Nugwi huko Zanzibar.

Ufukwe wa Nungwi ulio katika ncha ya kaskazini-magharibi ya kisiwa. Ni nyumbani kwa mchanga mweupe wa unga, maji ya samawati ya fuwele, na mimea na wanyama wa kigeni. Ni eneo la kuvutia pia kwa watalalii hasa mandhari yake ya kuvutia wakati wa machweo.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ufukwe wa Nungwi, Zanzibar

Orodha ya fukwe 25 bora ya 2023 kulingana na Tripadvisor:

1.Baía do Sancho - Brazili

2.Eagle Beach - Aruba

3.Cable Beach - Australia

4.Reynisfjara - Iceland

Grace Bay - Visiwa vya Turks na Caicos

Praia da Falesia - Ureno

7.Radhanagar - India

8.Spiaggia dei Conigli - Sisili (Italia)

9.Varadero - Cuba

10. Ka'anapali - Hawaii, Marekani

11.Siesta - Florida, Marekani

12.Driftwood - Georgia, Marekani

13.Manly Beach - Australia

14.Pwani ya Mile saba - Kisiwa cha Cayman

La Concha - Uhispania

Kelingking - Indonesia

17. Playa de Muro - Uhispania

18. Manuel Antonio Beach - Costa Rica

19.Ipanema - Brazil

20.Nungwi - Tanzania

21.Falassarna - Ugiriki

22. Nissi - Kupro

23.Pwani ya Kaskazini - Mexico

24.Magens Bay - Visiwa vya Virgin vya Marekani

2. Balos Lagoon - Ugiriki