Siquijor: Kisiwa cha kuvutia kilicho na umaarufu wa uchawi.

Na Simon Urwin

f

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Maelezo ya picha, Siquijor inafahamika kama ‘Kisiwa cha siri’ kwa sababu ya waganga wake na tiba zinazotolewa huko. (picha kwa hisani ya Simon Urwin)

Kisiwa cha mbali cha Siquijor ni cha kipekee – sio tu kwa taifa la Ufilipino , lakini kwa eneo zima la kusini mashariki kwa bara Asia. Kinafahamika na kutambulika tangu miaka ya zamani kama kitovu cha uchawi, mazingaombwe na ushirikina na vile vile tiba za asili.

Siquijor, iliopo katika eneo la kati mwa Visayas, huwavutia wageni kutoka Ufilipino wakiwemo wale wanaoishi ughaibuni, ambao hufika hapa kupata huduma mbali mbali za tiba asilia na vile vile kushuhudia tamaduni za dhehebu ya kikatoliki ambayo ililetwa hapa an Wahispania katika karne ya 16, ambapo pia kuna matambiko ya dini ya kishamani iliyotokea mashariki mwa bara ulaya ambapo waumini wanaamini miungu, pepo mbaya na kuwasiliana na roho za waliofariki.

Tiba mbali mbali asilia zinazotegemea matambiko ya kishirikina zinatambulika kama nguvu za kuondoa maradhi na magonjwa (bila ya kuangazia makali ya ugonjwa wa aiana yake) hali ambayo inaaminika kufanikishwa na moja kati ya masuala hayo matatu.

‘Sababu ya kwanza ni roho za pepo zilizokasirika,’ asema Luis Nathanie Borongan ambaye huwaogoza watalii hapa. ‘Pepo mbaya zipo kote na zinatuzingira, kwenye maporomoko yam aji, msituni, na baharini. Na ikiwa tunaisumbua au kuiingilia bila kupata idhini na wao hulipiza kisasi kwa hilo kwa kutupa maradhi, kutulaani au hata kutuuwa.’

Sababu ya pili anayoielezea Borongan innatokana na uchawi. ‘ Kuna aina mbali mbali ikiwemo HAPLIT (kumroga mtu kwa kinyago au mdoli ) na BARANG (kuwatumia wadudu kuwadhuru watu au chakula shambani.)’

Sababu ya tatu ambayo ni hafifu ni ya maradhi au matukio yanayotokea kwa kawaida, ambapo athari yake kwa mfano mafua au vile mazingaombwe ya ibada za kishetani zinaweza kutatuliwa kwa kumtembelea mganga wa tiba za kiasili MANAMBAL.

Imani kubwa imewek wa kwa misingi ya kwamba waganga wa kisiwa hiki wana uwezo wa kutekeleza mengi – na kusababisha hali ya wengi kuamini kwaman kisiwa cha Siquijor kina umuhimu mkubw ana kuvutia wageni kutoka nje ya Ufilipino n ahata raia wake wanaoishi ughaibuni.

‘Wageni wa kimataifa wanaozuru kisiwa hiki wanahitaji tu kumuuliza afisa wa utalii, au dereva wa taksi, kisha watawwapa maelezo muhimu,’ aseam Borongan. ‘Waganga wanaamini kwamba ujuzi wao ni zawadi kutoka kwake Mola, kwa hivyo hawatoi huduma zao kwa wachache bali kwa watu wote .’

Kwa sasa Siquijor inafahamika kama ‘Kisiwa cha siri’

f

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Kisiwa ambapo waganga wanaogopwa

Wakazi wa kisiwa cha Siquijor hutembelea waganga wa MANANAMBAL badala ya madaktari hospitalini. ‘Waganga hao wa tiba asili wanasemekana kufanikiwa katika baadhi ya magonjwa ambayo hushinda matibabu ya kisayansi.’ Asema Borongan.

Kipande muhimu cha matibabu hayo ni wagonjwa kutakiwa kutumia madawa ya kiasili na yale ya kutengezwa nyumbani. ‘Wao hutengeneza aina mbali mbali za madawa za kiasili, zaidi ya 300 kutoka kwa miti ya kiasili yenye dawa inayomea kisiwani. Kuwepo kwa aina mbali mbali ya miti ya aina hii ya kiasilia inayomea kisiwani kumetambulika kama sababu kuu ya watu kufika kisiwani kupata matibabu na kwa nini eneo hili ni muhimu kwa maisha yao kwa miongo mingi.’

g

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Umaarufu wa uchawi na ushirikina

Wasafiri kutoka Uhispania Juan Aguirre na Esteban Rodriguez walikuwa watu wa kwanza kutoka Ulaya kuwasili kwenye kisiwa cha Siquijor mnamo 1565.

Walikiona kisiwa hicho kutoka mbali na kudhani kwamba kilikuwa kina waka moto , wakalipa jina la ISLA DE FUEGO (Kisiwa cha moto). ‘Kwa kweli moto huo ulikuwa wadudu wanaofahamika kama kimemeta yaani FIREFLIES ambao walikuwa wanapepea wengi kisiwani juu ya miti ya aian aya MOLAVE,’ asema Borongan.

‘Hali hii ya kimazingira (ambayo hutokea nadra) ni sababu kuu kwamba Siquijor ilipata umaarufu mwanzoni kama kisiwa kilichojaa ushirikina na kwa nini wakazi wake na wale wa visiwa Jirani waliogopa kukitembelea.’

g

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Eneo ambapo tamaduni za madhehebu ya kishamani na kikatoliki zinakutana na kuoana.

Ufilipino ilikumbatia dini ya kikristo hasa madhehebu ya kikatoliki mnamo 1521, japo wamishenari hawakuwasili kwenye kisiwa cha Sijiquor hadi miaka ya 1700, huenda walizuiliwa na taarifa za ushirikina huko.

Tamaduni za madhehebu ya Kishamani ilikuwa imekitat mizizi kisiwani humo wakati huo, na wakati ambapo wamishenari walifika huko ilikuwa vigumu kubadili mambo.

‘Lakini muda ulipopita, Imani hizo mbili zilioana na kuwepo kwa pamoja: waganga walitajmbua kwamba ujuzi wao ulitokana an nguvu za juu ambazo walizitambuwa na kuziiita Mungu; wakaamua kutambua ishara za kidini, na wengi wao walikuwa wakazi katika Kijiji cha San Antonio. ‘

Antonio alikuwa mtakatifu wa waliopotea, na waganga wenye kutibu n ani ishara kuu kwao kwa sababu ya maradhi huashiria ukosefu wa usawa mwilini mwa binadamu.

f

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Dawa za mapenzi,matamanio na ufanisi.

Matumizi ya dawa za kiasili hufanyika kote kisiwani na hupatikana kwa haraka hata kwenye maduka yaliyopo barabarani kwa bei ya pauni 1 na senti 40. Mojawapo ya dawa yenye umaarufu ya kujaalia mapenzi ina asilimia 20 ya viungo vya kiasili ikiwemo PANGAMAY kijiti chenye umbo mithili ya mkono wa binadamu. ‘Ina ashiria kwamba mapenzi yanakuja.’ Asema lilia Alom, mtaalamu wa kutengeneza dawa hizi za mapenzi ambaye amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka 30. ‘Njoo kwangu’ inasema , iwe ni mahaba ya mapenzi au bahati njema ya kufanikiwa.’ Alom anaelezea kwamab dawah ii haiwezi kuhakikisha kwamba mapenzi yatakuwa ya kudumu milele – ‘Hufaa kw muda mfupi wa matamanio’ – lakini hufaa kuvutia ufanisi wa kibiashara. ‘Inaweza kukupa ujasiri na hali ya kuwa mwenye kuamini mazuri yatafanyika hasa kupata mali.’

g

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Matambiko ya 'Jumamosi Nyeusi' kwa ajili ya nguvu za kiroho.

Zaidi ya viungo 200 vinatumika kutengeneza dawa hii ya nta nyeusi {ELIXIR MINASA} ambayo huchomwa wakati wa kufanya matambiko ya to-ob ambalo linafanyika kuwasha moshi utakaotoa pepo mbaya na kutambua pepo zenye hila.

Ili kuiandaa MINASA, waganga hutembelea maeneo yenye nguvu za kiroho kwa ijumaa saba wakifuatilia kila wiki wakati wa msimu wa mfungo wa LENT ili kukusanya viungo vyote vinavyohitajika, kama wadudu mbali mbali, maua, mitishamba,asali ya mwituni, na nta ya kandili iliyowashwa kwenye makaburi na kuyeyuka .

Viungo hivi hupikwa kwa pamoja katiak siku moja muhimu yam waka. Inafahamika kama jumamosi nyeusi - siku inayofuata ijumaa njema ambapo Yesu Kristo alilazwa kwenye kaburi. Hii inatambulika kama siku ya maombolezi nchini Ufilipino ndio kwa maana siku ikafahamika kama jumamosi nyeusi.

f

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Mawasiliano na mababu wa zamani

TIGI ni tamaduni ambayo hufanyika kutibu magonjwa ambayo yaliletwa na jamaa aliyefariki. Mganga Pascal Oguc hutumia kijiti kuwasiliana na waliofariki na kuwatambuwa. – ‘Kijiti hicho hujikunja au hata hukuwa kwa urefu wakati ambapo jina lao linatajwa kwa sauti,’ anaeleza – kabla ya kuwasiliana na roho za waliofariki. ‘ Wao huniambia mara kwa mara kwmaba hawajafurahishwa au wnanakerwa na hali ya kusahaulika,’ anasema Ogoc. ‘Kwa hivyohii ndio njia ya wao kukumbukwa kwa kuwalenga watu.’

Tiba ni rahisi : aliyeathirika hutoa pesa taslimu kwa padri au kiongoziw a dini wa eneo la karibu na ibada maalum inafanyika kwa heshima ya alitefariki ili kuifurahisha roho yake.’

g

Chanzo cha picha, Simon Urwin

Kuondolewa kwa pepo mbaya na laana.

Ruhelio Lugatiman ni miongoni mwa watu wachache waliosalia wanaofanya tambiko za BOLO-BOLO.

Tambiko hili linafanyika kwa kujaza chupa maji safi, kuweka mrija na jiwe lenye uchawi ndani.. matone ya hewa yaanimaputo hupulizwa kwenye maji hayo huku chupa hiyo ikisongewa juu ya mwili wa mgonjwa: ambapo jiwe hilo linatarajiw akuondoa mapepo ambayo yanaleta maradhi na kuifanya maji kuwa meupe au ya kijivu, na kisha vitu hutokea ndani ya chupa hiyo kimiujiza.

Lugatiman anasema kwamba ameona mengi kwa mfano nzige kwenye tambiko la BARANG, na sindano iliyotokana na kutupiwa pepo mbaya kwa kutumia mdoli , na mengine mengi yakijitokeza wakati wa kupata tiba.

Tambiko hilo linarudiwa hadi maji yatakapo kuwa safi tena , kuashiria kwamba mgonjwa amepona.

g

Chanzo cha picha, simon Urwin

Kuleta tiba kwa watu

Waganga hawatozi ada ya kutoa huduma yao ya matibabu, laki wao huomba kwamba wagonjwa watoe msaada mdogo badala yake. ‘Ni taaluma ya kuwajali watu, na wala sio ya kutafuta faida; tunaishi maisha yasiyo na mambo mengi,’ amesema Juanita Torremacha.

Kwa sababu hiyo, idadi yao imeounguwa katika miaka ya hivi maajuzi. Ili kubadili mkondo huu, hafla ya kial mwaka ya SIQUIJOR HEALING FESTIVAL imekuwa ikiandaliwa kila mwaka katika wiki takatifu tangu 2006 kwenye mbunga ya kitaifa ya Mlima Bandilan. Wakazi hap ana wageni hukaribishwa kushiriki.

‘Kila mmoja anweza kutengenza dawa za mapenzi na kushuhudia matambiko haya wao wenyenwe,’ asema Borongan. ‘ tunataka kuinyesha dunia kwamba hii sio WOO – WOO . Tiba zetu zina nguvu na kwa miongo mingi ndizo zimekifanya kisiwa cha Siquijor kuwa cha kipekee. Hatutaki kupoteza nguvu hizo za kishirikiana.’

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed