Mchawi anayedaiwa kusaidia kushindwa kwa Wanazi kwa hila zake

ds

Chanzo cha picha, ALAMY

Maelezo ya picha, Uchawi wa Jasper Maskelyne uliripotiwa kusaidia juhudi za Jeshi Washirika katika Vita vya Pili vya Dunia.
    • Author, Lucy Davies
    • Nafasi, BBC

Katika miaka ya 1930, Jasper Maskelyne (1902-1973) - mchawi maarufu alifanya maonyesho mbele ya hadhira iliyojaa watu katika kumbi za muziki kote Uingereza .

Bango la matangazo la 1931 lililotangaza maonyesho yake katika ukumbi wa London Palladium lilimwita mchawi huyo, "mwanamazingaombwe mkuu nchini Uingereza."

Ukweli usemwe, alikuwa na tabia za ajabu – alifanana na mwigizaji wa filamu Errol Flynn (1909-1959), alikuwa na masharubu membamba na macho ya kung’waruza. Na pia alikuwa mwembamba, kama anavyoonekana katika filamu ya 1937 ya Pathé brothers, ya Ufaransa. Katika filamu hiyo, Maskelyne anaonekana akimeza viwembe kumi na mbili.

Lakini mazingaombwe makubwa zaidi ya Maskelyne aliyafanya katika jangwa karibu na jiji la Cairo, Misri, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Alidai alikwenda na timu ya kuunda "mbinu, ulaghai, na vifaa vya kuwachanganya na kuwahadaa makamanda wa muungano wa Axis (Germany, Italy nad Japan), kama alivyoeleza mwenyewe katika tawasifu yake ya 1949, Magic: Top Secret.

Mbinu za udanganyifu zilitumiwa na Maskelyne na wenzake katika 'Operesheni Bertram,' jina la mazingaombwe yao wakati wa vita vya pili vya El Alamein, nchini Misri, mwaka 1942.

Pia Unaweza Kusoma

Maonyesho Yake

D
Maelezo ya picha, Muigizaji wa Uingereza Benedict Cumberbatch atacheza kama Jasper Maskelyne katika filamu ijayo

Kuna filamu ya maisha ya Maskelyne iliyochezwa na mcheza filamu wa Uingereza, Benedict Cumberbatch ambayo iko katika matayarisho.

Maskelyne pia ndiye mada kuu katika maonyesho ya, ‘Spies, Lies and Trickery (Wapelelezi, Uwongo na Hila), katika Jumba la Makumbusho la Imperial Waar, huko London.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Maonyesho hayo yanaeleza kazi ya taarifa za uwongo, upotoshaji na udanganyifu wakati wa vita, kutoka Vita vya Kwanza vya Dunia hadi vita vya leo.

Maonyesho hayo yanajumuisha takribani vitu 150, kama vile vifaa, hati rasmi, filamu na picha. Maonyesho yanatoa mifano ya hadithi tofauti, nyingine zinazojulikana na nyingine sio maarufu.

Kama vile hadithi ya binti wa kifalme wa India, Noor Inayat Khan (1914-1944), mwanamke wa kwanza opereta wa redio aliyetumwa Ufaransa iliyokuwa ikikaliwa na Wanazi. Anajuulikana kama "Spy Princess".

"Tunataka kuonyesha kwamba vita havipiganiwi tu na kupata ushindi kwenye medani za vita au katika vyumba vya mikutano," anasema mmoja wa wasimamizi wa maonyesho hayo, Michelle Kirby. "Mengi hutokea nyuma ya pazi."

Tangu Maskelyne achapishe tawasifu zake, wakosoaji wanasema alitia chumvi michango yake binafsi. Lakini taarifa hizo za wakosoaji na za Maskelyne, ni vigumu kuzidhibitisha.

"Ukweli ambao tunapaswa kukabiliana nao ni kwamba mara nyingi ni vigumu kuthibitisha ushiriki wa kweli wa wale wanaohusika na udanganyifu katika vita," anasema Kirby.

Hadaa katika vita

D

Chanzo cha picha, IWM

Maelezo ya picha, Picha ya Jasper Maskelyne wakati wa Vita vya Pili vya Dunia

Maskelyne alikuwa na umri wa miaka 37 vita vilipoanza. Anatoka katika ukoo wenye heshima wa wanamazingaombwe. Babu yake alivumbua mbinu ya kuvifanya vitu vielee na akawa maarufu kwa mazingaombwe.

Wakati wa vita, Maskelyne alijitolea katika Jeshi la Wahandisi la Uingereza. Alidai mbinu za uchawi zinaweza kutumika kujificha.

Na alithibitisha madai yake kwa maafisa wasio amini kwa kuonyesha meli ya kivita ya Ujerumani katika Mto Thames wa London kwa kutumia maboksi na vioo.

Muda mfupi baadaye, Brigedia Dudley Clark alimpa Maskelyne amri ya kuongoza "Kikosi cha Majaribio ya Kujificha,” kilichopewa jina la utani Genge la Wachawi" au Genge la Vichaa.”

Genge hilo lilijumuisha fundi umeme, mkemia, mbunifu wa eneo la maonyesho, mbunifu majengo, mpiga picha, mchoraji na seremala.

Kwa pamoja, walikuwa wa ajabu – na muhimu zaidi, kulingana na Maskelyne, waliweza kulijificha jiji lote la Alexandria, Misri, lisishambuliwe na mabomu ya Ujerumani.

Ili kufanya hivyo, walitengeneza taa za usiku, majengo bandia, minara ya kuongozea na mizingra ya kudungulia ndege kwenye ghuba karibu kilomita 5 kutoka jiji halisi.

Na Jeshi la Anga la Ujerumani, Luftwaffe walipofika, walilipua kwa mabomu baadhi ya majengo feki - hivyo marubani wakaamini wamefanikiwa kufikia malengo yao.

"Kuna picha za Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Marekani (1861-1865) – za magogo yaliyoundwa kama mizinga yenye silaha, na katika maonyesho tuna kichwa bandia cha mtu ambacho kiliwavuta wadunguaji kwenye mitaro,” anasema Kirby.

Pia Unaweza Kusoma

Mafanikio Yake Makubwa Zaidi

sd

Chanzo cha picha, IWM

Maelezo ya picha, Moja ya mbinu zake za kuwapumbaza Wanazi ni matumizi ya vifaru bandia

Katika tawasifu yake, mchango mkubwa zaidi wa Maskelyne katika Operesheni Bertram ulikuwa ni kumfanya Kamanda wa Ujerumani, Erwin Rommel afikirie mashambulizi ya Jeshi Washirika, (Marekani, Uingereza na Umoja wa Kisovieti,) yangetokea kusini, wakati kwa hakika Kamanda, Bernard Montgomery alikusudia kushambulia kutokea kaskazini.

Mchawi huyo anadaiwa kutumia turubai na mbao kuficha vifaru 1,000 kwenye malori kuelekea kaskazini na kuunda vifaru 2,000 vya bandia, pamoja na reli bandia, bomba la maji bandia, mazungumzo ya redio bandia na sauti ghushi za ujenzi huko kusini.

Katika tawasifu yake, Maskelyne anasema Montgomery alimwambia, "vita vyote vitabadilika kulingana na kile kinachotokea hapa. Natumaini umeleta fimbo yako ya uchawi."

"Hayo yote yalisaidia Jeshi Washirika kufikia malengo kamili," anasema Kirby.

Kwa kweli, wanajeshi walipoingia vitani, Wanazi walijikuta hawajajitayarisha. Katika vita vya El Alamein, jeshi la washirika liligeuza mwelekeo wa vita vya Afrika Kaskazini.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill (1874-1965), "kabla ya vita vya Al-amein, hatukupata ushindi kamwe. Baada ya vita hivyo, hatukuwahi kushindwa tena."

Kundi la Magic Gang liliripotiwa kusambaratika baada ya vita hivyo, lakini mbinu za Maskelyne - zinaaminika zilitumika katika hujuma za uongo katika kiwanda cha ndege cha De Havilland huko Hatfield, kusini mwa Uingereza, mwaka 1943.

Ili kuhadaa timu za upelelezi za Ujerumani kuamini bomu lililipuliwa ndani ya kiwanda hicho, inadaiwa alitengeneza transfoma za mbao, mashimo bandia na vifusi.

Eddie Chapman, jasusi wa Uingereza na Ujerumani anayejulikana kama ZigZag (1914-1997) alitumiwa kuwafahamisha Wajerumani juu ya mafanikio yake. Na alipokea medani ya Iron Cross kutoka Ujerumani na ipo kwenye Jumba la Makumbusho la Imperial huko London.

Maskelyne hakutambuliwa rasmi kwa kazi yake wakati wa vita. Inasemekana alichukizwa na kusahauliwa, jambo ambalo pengine lilichangia kuchapisha kumbukumbu zake.

Katika wasifu wake Maskelyne anaelezea ushujaa na kujisifu bila kuchoka. Anadai alikuwa kwenye orodha binafsi ya Adolf Hitler ya watu wanaotafutwa sana.

"Ukweli wa yale yaliyotokea katika operesheni za vita ni vigumu kuyathibitisha. Pengine hatutoweza kujua ukweli wa kinachosimuliwa."

Pia Unaweza Kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah