Mauaji ya Holocaust: "Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha, Myahudi hata mmoja hangesalia Ulaya."

Holo

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo mwaka wa 1955, muongo mmoja baada ya kuachiliwa kutoka kambi ya Wanazi, Primo Levi alichapisha makala ya kutisha kuhusu "mashine kubwa ya kuua" ambayo Wanazi walikuwa wameunda kuwaua Wayahudi kama yeye, pamoja na jamii nyingine za watu wachache.

Alikuwa na wasiwasi kwamba uhalifu mkubwa zaidi unaoweza kufikiriwa, ambao bado ulikuwa wazi sana katika akili za walionusurika, ulikuwa katika hatari ya kusahauliwa na umma kwa ujumla na kukemea "ukimya wa ulimwengu uliostaarabu", ambao uliona kutajwa kwa kambi kama nia ya kuangamizwa kwa Nazi.

Mbali na kusahaulika, mauaji ya Wayahudi wa Ulaya polepole yakawa alama ya ulimwengu ya kuhukumu kutokuwepo kwa ubinadamu.

Mnamo mwaka wa 2005, miongo mitano baada ya swali la kejeli la Levi "Je, ukimya huu unahalalishwa?", Baraza la Umoja wa Mataifa lilitangaza Januari 27 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kukumbuka Mauaji ya Wayahudi.

Kufikia wakati huo, ustaarabu huo ambao ulizuia kuzungumza juu ya uovu uliotokea ulikuwa umebadilishwa na mtiririko usiokoma na mkubwa wa vyombo vya habari taaluma nyingi, ambamo "Ikiwa huyu ni mtu", ushuhuda wa Levi mwenyewe ya maisha ya kila siku huko Auschwitz ambayo hapo awali ilipokelewa kwa njia tofauti, ikaja kutambuliwa kama mojawapo ya "vitabu vya lazima sana", kama mwandishi Philip Roth alivyoeleza.

Katikati uandishi huu, "The Holocaust: A New History", na mwanahistoria Laurence Rees, inachukuliwa na wakosoaji kama moja ya utangulizi bora zaidi wa kile kilichotokea, ikijipambanua kwa kufuatilia sauti za wahasiriwa, wauaji na watazamaji ambayo mwandishi aliikusanya kwa miaka mingi katika mahojiano ya filamu zake za televisheni zilizoshinda tuzo.

Rob Attar, mhariri wa jarida la Historia la BBC, alizungumza na Rees ili kujaribu kuelewa ni jinsi gani hata baada ya mauaji ya Holocaust kumalizika, baadhi ya waliohusika walihisi wangeweza kuhalalisha hilo kimaadili.

holo

Chanzo cha picha, Getty Images

Ilikuwaje Ujerumani ikachochea mauaji ya Holocaust?

Hilo ni swali kubwa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Muhimu kukumbuka ni kwamba ukiangalia, kwa mfano, kile kilichokuwa kikitokea nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, kulikuwa na visa vingi zaidi vya mashambulizi ya kikatili dhidi ya Wayahudi kuliko Ujerumani.

Kwa hivyo ikiwa ungeishi katika miaka ya mapema ya karne ya 20 na kuulizwa kutabiri ni wapi jambo kama hilo lingetokea, kuna uwezekano mkubwa kwamba ungesema Ujerumani.

Kwa nini, basi, ilitokea huko? Nadhani mambo kadhaa yalikuja pamoja.

Kubwa zaidi lilikuwa hasara katika Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, ambavyo vilitengeneza mazingira ambapo watu walikuwa wakitafuta mtu wa kulaumiwa. Kulikuwa na unyanyasaji mwingi na hisia kwamba "Wayahudi walikuwa wametusaliti."

Ilikuwa ni ujinga, lakini kulikuwa na hisia halisi ya kutaka kuamini kuwa nlilikuwa ni kosa la mtu mwingine.

Wakati huohuo, kuongezeka kwa ukomunisti nchini Urusi kuliingia katika maasi mbalimbali nchini Ujerumani katika miaka ya baada ya vita yaliyohusisha Wayahudi kadhaa, kwa hiyo kukawa na mkanganyiko kwamba Dini ya Kiyahudi ililingana na Bolshevism (mpango unaotetea kupinduliwa kwa ubepari.)

Kwa hiyo kulikuwa na mchanganyiko wa hofu ya ukomunisti, baada ya vita, na hisia kwamba kuna kitu kibaya na hali ya Ujerumani.

Makundi mbalimbali ya wazalendo yaliibuka ambao walitaka kuwaweka watu wa 'Wajerumani' mbele, jambo ambalo lilimaanisha kutengwa kwa Wayahudi.

Na mtu ambaye alitetea halii hii kwa njia ya hasira tangu mwanzo alikuwa Adolf Hitler.

Kwa kweli, na nilipofanya mfululizo wangu wa awali wa kioindi cha televiseni " Wanazi: Onyo kutoka kwa Historia ", tuliita kipindi tulichofanya kuhusu mpango wa kuangamiza 'Barabara ya Treblinka'. Treblinka'), sio Auschwitz.

holo

Chanzo cha picha, Getty Images

Auschwitz (kambi ya mauaji) ilikuwa hali ngumu sana kwa sababu nyingi tofauti.

Ingawa iliishia kuwa mahali pa mauaji makubwa zaidi ya watu wengi zaidi katika historia ya ulimwengu, hiyo ilikuwa moja tu ya kazi ambayo ilitoa kwa serikali ya Nazi. Wakati Treblinka iliundwa kwa kusudi moja tu, mauaji ya watu wengi.

Hadi watu 900,000 walikufa huko Treblinka (ambayo ni sawa na kiwango cha Auschwitz cha milioni 1.1) na bado hakuna mtu yeyote anayetembelea eneo hili ikilinganishwa na Auschwitz.

Lakini ikiwa utafika huko utakuta kwamba hakuna kitu huko kutoka kipindi cha Nazi.

Hiyo ni kwa sababu Wanazi waliharibu Treblinka, ambayo ilikuwa imetimiza misheni yake mnamo 1943.

Kambi hiyo ilikuwa ndogo ikilinganishwa na Auschwitz, na hiyo kwangu inaongeza hofu kwa njia ya karibu zaidi ya kutembelea Auschwitz-Birkenau, kwa sababu unatambua kwamba ikiwa utafanya tu kuua watu utahitaji nafasi.

Umekutana na wahusika kadhaa wa Holocaust katika kazi yako. Ilikuwaje wangeweza kufanya vitendo viovu hivi, vikiwemo vya kuua watoto wachanga na watoto?

Mfano mzuri wa hili kwangu ulikuwa Oskar Groening (mwanachama wa Waffen-SS anayejulikana kama "mhasibu wa Auschwitz"), ambaye tulimhoji kwa ajili ya filamu yetu.

Tukamuuliza ni vipi Wanazi wangeweza kuua watoto na akasema kwamba adui si watoto bali ni damu ya watoto ambao wangekua Wayahudi.

holo

Chanzo cha picha, Getty Images

Sababu iliyowafanya wahisi kuwa wana haki katika matendo yao, na Heinrich Himmler (mkuu wa SS) alisema katika hotuba katika 1943, ilikuwa kwamba ukiua tu watu wazima, watoto wangekua walipiza kisasi na kuwafuata watoto wako mwenyewe. Kwa hivyo ikiwa kweli uliwapenda watoto wako basi unapaswa kuwaua watoto wao. Ikiwa ungekuwa na ujasiri wa kutosha, ungetatua tatizo milele.

Hiyo ndiyo aina ya kitu ambacho kilikuwa vichwani mwao, nadhani.

Kwa hiyo, hata baada ya Maangamizi Makubwa ya Wayahudi kuisha, je, baadhi ya wale waliohusika bado walihisi kwamba wangeweza kuhalalisha jambo hilo kimaadili?

Ndiyo, na hii ndiyo sababu mojawapo iliyonifanya niendelee kuchunguza mada hiyo kwa miaka mingi.

Unachimba unachimba na unachimba huwezi kufika chini maana mara nyingi hutegemei majibu unayopata.

Ikiwa unazungumza na, kwa mfano, washiriki wa zamani wa NKVD (polisi wa siri wa Stalin), ambao walihusika katika uhamishaji wa kutisha wa Kalmyks au wachechenia au Tata wa Crimea, watakachosema zaidi ni: "Kama singefanya hivyo wangenipiga risasi.' Na ni ngumu sana kwenda mahali popote kwenye mahojiano baada ya hapo.

Baadhi ya watu wa ajabu sana ambao nimewahi kukutana nao ni s onderkommandos wa zamani : watu ambao walilazimishwa chini ya maumivu ya kifo cha papo hapo kusaidia Wajerumani kuendesha mashine ya kuangamiza.

Walihusika katika kung'oa miili kwenye vyumba vya gesi baada ya watu kuuawa, wakipanga vitu vya Wayahudi, miili ya kuzika ... Kazi mbaya kabisa.

Kati ya matatizo yote ya kimaadili unayoweza kukumbana nayo, hili ni moja kati ya magumu na nisingeweza kumhukumu mtu yeyote katika hali hiyo kwa sababu wangefanya nini?

holo

Chanzo cha picha, Getty Images

Nitamkumbuka daima mtu, ambaye sasa amekufa, aitwaye Toivi Blatt, ambaye alikuwa sonderkommando katika kambi ya kifo ya Sobibor.

Nilimuuliza amejifunza nini kutokana na tukio hili na akaniambia-na ninanukuu-: "Nimejifunza kwamba hakuna mtu anayejijua mwenyewe, kwa sababu mpaka unajikuta katika hali kama hiyo, hujui wewe ni nani na una uwezo wa kufanya nini."

Aliongeza: "Wakati mwingine mimi huwaona watu wakitembea barabarani na kuniuliza nielekeze na huwa ninawatazama na kufikiria, 'Unaonekana kama mtu mzuri, lakini ungekuwaje huko Sobibor?'

Kwa kweli, ni sawa na kitu ambacho mwanachama wa zamani wa SS aliniambia: kwamba shida ya ulimwengu leo ni kwamba watu ambao hawajawahi kuwa katika hali mbaya huzunguka kutoa hukumu kwa watu ambao wamewahi.

Hilo halikunizuia kuamini kwamba alichokifanya ni cha kuchukiza na cha aibu, lakini kinakufanya ufikirie.

Je, unafikiri mauaji ya Holocaust yalikuwa uhalifu mbaya zaidi katika historia ya wanadamu?

Niliwahi kumuuliza swali hili Profesa David Cesarani, ambaye kwa bahati mbaya alifariki mwaka 2015, na akaniambia kuwa katika historia ya ubinadamu hawezi kufikiria kisa kingine ambapo kiongozi fulani aliamua kwamba kikundi cha kidini kitaangamizwa hadi hatua ya kifo, mtoto wa mwisho na kuunda, kwa muda mfupi, njia za kuifanikisha.

Na mimi nakubaliana na hilo.

Holocaust ilikuwa 'pekee'.

Kwa mfano, Stalin alikuwa mnyama mkubwa sana aliyesababisha vifo vya mamilioni ya watu, lakini hakuwahi kujaribu kuangamiza kundi zima la watu.

Idadi kubwa ya Wakalmyk na Wachechenia waliponea harakati zake. Ingawa katika maeneo fulani ya Ulaya hakuna Wayahudi.

Hakuna shaka akilini mwangu kwamba kama vita havingekwisha wakati viliisha, tungekuwa na hali huko Ulaya ambako hakukuwa na Myahudi hata mmoja..