Kwanini uchumi wa Urusi unaimarika licha ya vita ikilinganishwa na nchi za G7?

Chanzo cha picha, Reuters
Ilikuwa Machi 2022. sarafu ya Ruble ya Kirusi ilianguka, thamani ya London ya Gazprom kubwa na Sberbank ilishuka kwa 97%.
Mistari mirefu ilianza kujitokeza kwenye ATM huko Moscow. Yachts, timu za mpira wa miguu, majumba na hata kadi zao za mkopo zilichukuliwa kutoka kwa matajiri wakubwa Oligarchs. Urusi ilianguka katika mdororo mkubwa wa uchumi.
Haya yalikuwa ni matokeo ya mara moja ya jaribio la ajabu la nchi za Magharibi kuidhibiti Urusi kifedha baada ya kuivamia Ukraine.
Miongoni mwa hatua muhimu zaidi ilikuwa kutaifishwa kwa mali rasmi ya fedha za kigeni za serikali ya Urusi na, haswa, kufungia kwenye akiba ya benki kuu ya kiasi cha dola bilioni 300.
Serikali za Magharibi ziliepuka kwa makusudi kutumia misemo kama "vita vya kiuchumi," lakini kwa hakika ilionekana kana kwamba kulikuwa na vita vya kifedha na Kremlin.
Ilikuwa bora kuliko njia mbadala ya makabiliano ya moja kwa moja kati ya mataifa ya nyuklia.
Takribani miaka miwili imepita na mabadiliko makubwa yametokea katika muktadha huu wa kiuchumi.
Katika mahojiano marefu na ya kusisimua wiki hii, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwa furaha kwamba Urusi ndio uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Ulaya.
Wiki iliyopita, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) liliangazia nguvu ya uchumi wa Urusi wakati lilipoinua makadirio ya ukuaji wake kwa mwaka huu kutoka 1.1% hadi 2.6%.
Kwa mujibu wa takwimu za IMF, uchumi wa Urusi ulikua haraka kuliko G7 nzima mwaka jana na utafanya hivyo tena mnamo 2024.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hizi sio nambari tu.
Mkwamo wa Ukraine mwaka jana na kuongezeka kwa matarajio ya mzozo uliogandishwa baadaye mwaka huu kumechangiwa na kufufuliwa kwa uchumi wa Urusi kuelekea juhudi zake za kijeshi, haswa katika ujenzi wa maeneo ya kujihami mashariki na kusini mwa Ukraine.
Je, Urusi inaweza kuendeleza ukuaji?
Viongozi wa nchi za Magharibi wanasema kuwa mtindo huu hauwezi kudumu kwa muda mrefu. Lakini swali ni, unaweza kudumu kwa muda gani?
Urusi imebadilisha uchumi wake kuwa uchumi wa vita.
Matumizi ya kijeshi na usalama, ambayo yanachukua hadi 40% ya bajeti, yamerejea katika viwango vya USSR.
Maeneo mengine ya msaada wa serikali kwa idadi ya watu yamepunguzwa ili kukabiliana na ufadhili wa uzalishaji wa mizinga, mifumo ya makombora na ulinzi katika Ukraine inayokaliwa.
Juu ya hayo, na licha ya vikwazo vya Magharibi kwa mafuta na gesi ya Kirusi, mapato ya haidrokaboni yameendelea kuingia kwenye hazina za serikali.
Meli za mafuta sasa zinaelekea India na China na malipo mengi yanafanywa kwa Yuan ya China badala ya dola za Kimarekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzalishaji wa mafuta nchini Urusi unabaki kuwa mapipa milioni 9.5 kwa siku, kiasi ambacho ni chini ya viwango vya kabla ya vita.
Nchi imekwepa vikwazo kwa kununua na kupeleka "meli ya kivuli" ya mamia ya meli za mafuta.
Wiki iliyopita, Wizara yake ya Fedha iliripoti kwamba ushuru wa hidrokaboni mnamo Januari ulizidi viwango vilivyoonekana mnamo Januari 2022, kabla ya uvamizi huo.
Mtiririko unaoendelea wa fedha za kigeni katika mafuta ya Urusi, gesi na almasi pia umesaidia kupunguza mvutano kuhusu thamani ya ruble.
Viongozi wa Magharibi wanasisitiza kuwa hii haiwezi kudumu, lakini wanatambua athari zake.
Kiongozi mmoja wa dunia hivi karibuni alisema faraghani: "Mwaka wa 2024 utakuwa mzuri zaidi kwa Putin kuliko tulivyofikiri. Ameweza kupanga upya sekta yake kwa ufanisi zaidi kuliko tulivyofikiri."
Urusi yafichuliwa
Lakini aina hii ya ukuaji wa uchumi imeongeza sana utegemezi wa Moscow kwa mapato ya mafuta, China, na matumizi yasiyo ya tija ya vita.
Kadiri mahitaji ya mafuta na gesi yanavyoongezeka na ushindani wa uzalishaji wa Ghuba ya Arabia unakuja mtandaoni mwaka ujao, Urusi itafichuliwa.
Ongezeko la takwimu la pato la taifa (GDP) kutokana na uzalishaji wa mizinga na makombora ambayo hulipuka katika Donbas mashariki mwa Ukraine pia halina tija.

Chanzo cha picha, Reuters
Wakati huo huo, Urusi imepata shida ya raia wake wenye talanta zaidi.
Mkakati wa Magharibi haujakuwa kuzingirwa kwa uchumi wa Urusi, lakini kushiriki katika mchezo wa paka na panya ili kuzuia ufikiaji wake wa teknolojia, kuongeza gharama, kupunguza mapato, na kufanya mzozo usiwe endelevu kwa muda mrefu.
"Tungependelea Urusi itumie pesa zake kununua meli za mafuta kuliko matangi," afisa wa Marekani aliniambia. Katika soko la mafuta, lengo la sera sio kujaribu kuizuia India, kwa mfano, kununua mafuta ya Urusi, lakini kupunguza faida kutoka kwenye biashara hiyo kurudi kwenye vita ya Kremlin.
Lakini uthabiti huu na vilio vinaweza kudumu kwa takribani mwaka huu wote. Na hii inasaidia mkakati wa wazi wa Kremlin wa kusubiri mabadiliko ya uwezekano wa rais wa Marekani na kupunguzwa kwa fedha za Magharibi kwa ajili ya ulinzi wa Ukraine.
Mali zilizozuiwa
Ndio maana umakini sasa unarudi kwenye jukumu kuu la mamia ya mabilioni katika mali ya kifedha ya Urusi iliyohifadhiwa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliniambia mwezi uliopita: "Ikiwa dunia ina dola bilioni 300, kwa nini usiitumie?" Fedha hizo zote zilizozuiwa zinapaswa kutumika kufadhili juhudi za ujenzi wa Ukraine, alisema.
Kansela wa Uingereza Jeremy Hunt na Waziri wa Mambo ya Nje David Cameron waliunga mkono hatua hiyo.

Chanzo cha picha, Getty images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Cameron aliniambia, "Tumezuia mali hizi. Swali ni je, tutazitumia?"
Cameron alibainisha kuwa "kutumia baadhi ya fedha hizi sasa ni, kama utafanya, malipo ya awali ya fidia (ya Kirusi)" kwa uvamizi wao haramu wa Ukraine, na inaweza kutumika "kusaidia Ukraine na kuokoa fedha za walipa kodi wa Magharibi kwa wakati mmoja. "
G7 imewataka wakurugenzi wa benki zake kuu kuandaa mchanganuo wa kiufundi na kisheria. Inafahamika kuwa hili ni jambo linalowasumbua.
Mfadhili mmoja mkuu aliniambia kuna hatari ya kile alichokiita "kutumia silaha kwa dola." Kijadi, benki kuu hufurahia kinga huru kutokana na vitendo hivyo.
Mpango mmoja unaotengenezwa utatumia fedha au faida ya uwekezaji kukusanya makumi ya mabilioni ya dola kwa ajili ya Ukraine.
Ikiwa mali ya Kirusi inachukuliwa kwa njia hii, ni ujumbe gani unaotumwa kwa mataifa mengine, labda katika Ghuba, Asia ya Kati au Afrika, kuhusu usalama wa hifadhi zao katika benki kuu za Magharibi?
Putin hakika alitaka kuwasiliana kwamba China sasa inaibuka kama mbadala, ikiwa sio kwa Magharibi, basi kwa uchumi unaoibuka.
Warusi pia wameonesha kuwa watachukua hatua za kisheria, watachukua mali kama hiyo kutoka kwa kampuni za Magharibi zilizohifadhiwa katika benki za Urusi.
Hivyo vita kivuli juu ya uchumi wa Urusi ni muhimu kuelewa ambapo mgogoro huu na uchumi wa dunia unaelekea.
Sura sahihi ya ukuaji huu wa kifedha itakuwa na matokeo ya mbali zaidi ya Urusi na Ukraine.












