Wazo kwamba gereza linaweza kusaidia kuwarekebisha wafungwa lilitoka wapi?

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Magereza ni mahali pa mateso. Lakini kwa nadharia, lengo lake ni zaidi ya adhabu: kumrekebisha mfungwa.

Nchini Marekani, lengo la kuwarekebisha wafungwa lilianza tangu kufunguliwa mwaka wa 1876 kwa Kituo cha kurekebisha mambo cha Elmira katika jimbo la New York.

Ikitolewa kama taasisi ya "marekebisho ya tabia," ililenga sio tu kuwanyima wafungwa uhuru wao bali pia kuwabadilisha. Ingawa mwanzilishi wake, Zebulon Brockway, anayejulikana kama "baba wa magereza ya Marekani," alikuwa na sifa mbaya sana.

Majimbo mengine hivi karibuni yalikubali mtindo wa urekebishaji, na wazo kwamba magereza yalikuwa mahali pa kusahihisha watu likawa msingi wa mfumo wa haki.

Lakini wazo la kwamba kuwazuilia na kuwateseka ilikuwa vyema kwa wafungwa halikutokea katika karne ya 19. Mpango huo ulianza takriban miaka 4,000: kwa wimbo wa Mesopotamia - Iraq ya kisasa - uliosifu mungu wa kike wa gereza aliyefahamika kama Nungal.

Karibu muongo, nilipokuwa nimehitimu kama mwanafunzi wa utafiti juu ya utumwa katika Iraq ya zamani, nilipata maelezo kadha wa kadha zinazohusiana kufungwa.

Baadhi zilikuwa hati za usimamizi ambazo zilishughulikia habari za kila siku za uhasibu. Nyingine zilikuwa za kisheria, maandishi ya fasihi au barua za kibinafsi.

Nilivutiwa na kufungwa katika tamaduni hizi: washukiwa wengi waliowekwa kizuizini kwa muda mfupi, lakini katika maandishi ya fasihi na matambiko, kifungo kilionekana kama utaratibu wa kubadilisha na kutakasa.

''Nyumba ya maisha''

Karibu 1,800 BC, wanafunzi waliokuwa wakisomea uandishi katika mji wa kale wa Sumeri, mara nyingi kunakiliwa uteuzi wa kazi 10 za fasihi.

Wakitumia maandishi maalum, wale wanaotaka kuwa waandishi walinakili maandishi yalijumuisha mafanikio ya shujaa wa hadithi Gilgamesh alipokuwa akipigana na mnyama wa mwituni wa kuogopesha aliyejulikana kama Huwawa. Pia kuhusu mfalme mkuu wa Mesopotamia aitwaye Shulgi, ambaye alidai kuwa mungu.

DADEROT/WIKIMEDIA COMMONS

Chanzo cha picha, DADEROT/WIKIMEDIA COMMONS

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati mwandishi mkuu aliamuru maandishi haya, wanafunzi pia walisikia juu ya mungu wa kike wa magereza anayeitwa Nungal.

Ingawa haki yake haikuepukika, Nungal pia alisherehekewa kwa huruma yake.

"Nyumba" ya Nungal ilileta mateso kwa wafungwa, ambao maumivu yao yalisababisha maombolezo, lakini kupitia maombolezo haya, wafungwa wangeweza kutakaswa dhambi zao na kupatanishwa na miungu yao ya kibinafsi, ambao walikuwa watetezi na wapatanishi wao mbele ya miungu kubwa zaidi.

"Wimbo wa Nungal", ambao ulianza milenia ya pili au ya tatu KK. C. maelezo jinsi mfungwa mwenye hatia aliyehukumiwa kifo hakuuawa bali alinyakuliwa kutoka kwa “taya za uharibifu” na kufungiwa katika nyumba ya Nungal, ambayo anaiita “nyumba ya uzima,” lakini pia mahali pa mateso, kutengwa na maumivu.

Bado, wimbo huo unaelezea wafungwa waliobadilishwa na wakati wao gerezani. Mungu huyo wa kike asema kwamba nyumba yake “imejengwa kwa huruma, hutuliza moyo wa mtu huyo na kuburudisha roho yake.”

Hatimaye, aendelea kusema, wataomboleza na kutakaswa machoni pa mungu wao: “Atakapokwisha kuufurahisha moyo wa mungu wake, atakapousafisha kama fedha safi, atakapouangaza mavumbini. ” ; atakapokwisha kuitakasa uchafu, kama fedha ya hali ya juu kabisa... itawekwa tena katika mikono ya utakatifu ya mungu wake."

Ukweli dhidi ya uongo

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni kwa kiasi gani waliamini hadithi hizi kuhusu miungu ni suala la mjadala. Je, maandishi kama vile “Wimbo wa Nungal” yalikuwa mambo ya kweli ya dini au hadithi za hadithi tu ambazo hakuna mtu aliyezizingatia kwa uzito? Kwa kuwa ni maandishi ya kifasihi, pia si chanzo cha kutegemewa kuhusu mfumo wa mahakama.

Falme za Mesopotamia wakati huo zinaonekana kutumia magereza kuwazuilia washukiwa kabla ya kuwaadhibu, sawa na jela zinazowashikilia washukiwa leo kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Pia waliwaweka kizuizini watu ili kuwalazimisha kulipa faini au deni, na kuwalazimisha kufanya kazi, katika visa vingine kwa zaidi ya miaka mitatu. Lakini adhabu hiyo, ambayo kwa kawaida ilikuwa na madhara ya kimwili au ya kifedha, haikujumuisha kifungo cha jela.

Hata hivyo, kuwekwa kizuizini kulimaanisha kuteseka. Mfungwa mmoja alieleza gereza hilo katika barua kwa mkuu wake kuwa “nyumba ya taabu na njaa.”

Katika andiko lingine, mtumaji huyo anasema aliachiwa huru, lakini analalamikia vipigo alivyopata mfungwa mwingine ikiwa ni sehemu ya upelelezi, ingawa hataji asili ya kosa hilo.

Hata hivyo, wasomi Klaas Veenhof na Dominique Charpin walipata ushahidi kwamba Nungal alikuwa na jukumu katika mchakato wa mahakama.

Katika mahekalu mengine, viapo viliapishwa mbele ya wavu, sawa na ile iliyotumiwa kwa uvuvi, ambayo iliashiria haki isiyoweza kuepukika ya Nungal.

Maono yaliyoonyeshwa katika wimbo huo pengine yalijumuishwa katika mazoezi ya kitamaduni ya baadaye ambapo kifungo kilitumika kumtakasa mfalme.

Wakati wa sherehe za Mwaka Mpya, mfalme alikuwa akivua mavazi yake ya kifalme na kuingia katika gereza la muda lililojengwa kwa matawi, ambapo angetoa sala kwa miungu kwa ajili ya dhambi zake.

Kupitia maombi na matambiko, alitakaswa na angeweza kuendelea na kazi zake za kifalme.

Jana na leo

Watu wengi huenda walizuiliwa katika jela za Mesopotamia kwa muda mrefu lakini wakati wakiwa huko waliteseka sana

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Pengine ni uzoefu huo uliozaa matini kama vile "Wimbo wa Nungal," ambayo inachunguza jinsi uzoefu huo ungeweza kutumika kumrekebisha mfungwa kupitia maombolezo.

Dhana ya kwamba kufungwa kunaweza kuwa wazo zuri iko kila mahali, lakini je huo ni ukweli?

Jinsi mifumo ya magereza inavyofikiri kuhusu dhana ya mageuzi ni tofauti sana leo kuliko vile "Wimbo wa Nungal" ulivyokisia.

Hata hivyo, wazo lenye nguvu kwamba mateso yanaweza kuwa mazuri kwa wafungwa lina mizizi ya kihistoria : inaruhusu mifumo ya magereza kudai kuwa mateso ndani ya kuta zao ni ya kumrudi mhusika.