Nini kiliandikwa katika barua ya Saddam Hussein kwa Wapalestina kabla kifo chake?

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sadam Hussein
Muda wa kusoma: Dakika 3

Barua hiyo, iliyochapishwa katika magazeti mawili ya Jordan Agosti 2005, iliwasilishwa na Kamati ya Kimataifa ya Mwezi Mwekundu (ICRC) kwa mmoja wa marafiki wa Saddam aliyekuwa akiishi Jordan.

Watu waliowasilisha barua hiyo walisema - mwanaume huyo alikataa kutajwa jina lake. Inaaminika ndio barua ya kwanza kutoka kwa Saddam kabla ya kukamatwa Disemba 2003, iliyokwenda kwa mtu ambaye si mwanafamilia.

"Ninajitolea na uwepo wangu kwa Palestina yetu pendwa na Iraq yetu pendwa, ambazo zote zinateseka," inasema barua hiyo.

Tayseer Homsi, ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama cha Bacath cha Jordan, alisema barua hii iliyowasilishwa na ICRC, ilitumwa kwa mwanasiasa wa Jordan.

Kweli ni barua ya Sadam Hussein?

k

Chanzo cha picha, SOCIAL

Maelezo ya picha, Wapalestina wanaoishi Iraq walipiga kampeni haki zao kutambuliwa

Rana Sidani, ambaye alizungumza na ujumbe wa ICRC mjini Amman wakati huo, alisema: "ICRC ilithibitisha ukweli wa ujumbe uliochapishwa katika vyombo vya habari vya Jordan."

Rafiki wa familia ya Saddam, ambaye jina lake halikutajwa, alisema "mwandiko wa barua hiyo ni 100% wa Saddam."

Mabinti wawili wa Saddam, Raghad na Rana, waliishi Amman baada ya kuikimbia Iraq wakati Marekani ilipoikalia kwa mabavu.

Barua hii baadaye ilipata umaarufu wakati mashitaka kadhaa yalipoanzishwa nchini Iraq ya kumuondoa Saddam.

Mojawapo ni mauaji ya 1982 ya Washia 150 huko Dujail, kaskazini mwa Baghdad.

Saddam alikuwa Sunni, na walio wachache walikuwa Mashia, Wakurdi na wengineo.

Aprili 2003, aliondolewa madarakani baada ya Marekani kuivamia Iraq.

Saddam alivyowasaidia Wapalestina

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, 1988: Kiongozi wa Palestina Yasser Arafat akiwa katika picha na Saddam Hussein

Saddam Hussein aliponyongwa, kikundi kiitwacho Arab Liberation kiliweka mnara katika ardhi ya Palestina. Mji wa Qalqilya, ambapo mnara wa maombolezo ulijengwa.

Saddam amewaunga mkono Wapalestina kwa muda mrefu na kutoa mamilioni ya dola kwa familia za wale waliojilipua miaka ya 2000.

Ni maarufu miongoni mwa Wapalestina kwa sababu ya idadi ya makombora aliyorusha Israel wakati wa Vita vya Ghuba vya 1991. Mwaka huo, mabango ya Saddam yaliwekwa katika Ukanda wa Gaza.

Watu wengi katika ulimwengu wa Kiarabu walikasirishwa na mauaji ya Saddam.

Sadan Hussein, wakati wa uongozi wake nchini Iraq, aliwahakikishia Wapalestina haki kama zile za watu wa Iraq, kama vile kazi, elimu ya bure, posho na chakula.

Lakini serikali iliyomfuata Saddam iliondoa haki hizo, jambo ambalo lilisababisha maandamano ya Wapalestina wengi waliokuwa wakiishi nchini humo.

Jinsi Saddam alivyouawa

kk

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Saddam Hussein alipokamatwa

Siku ya Eid al-Adha mwaka 2006, kiongozi wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, aliuawa. Tarehe 30 Disemba.

Saddam alinyongwa kwa amri ya serikali ya Iraq kabla ya mapambazuko, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya Wairaq.

Mashtaka hayo yalihusiana na makosa yaliyofanyika zaidi ya miaka 20 kabla ya Marekani kumuondoa madarakani.

Asubuhi ya kunyongwa kwake, video ilitolewa kwenye televisheni ya Al-Iraqiya, runinga rasmi ya serikali, ilimuonyesha Saddam amevalia nguo nyeusi na kupelekwa kwenye chumba cha kunyongwa na wanaume waliofunika uso na kichwa.

d

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sadam Hussein aliponyongwa

Jaji wa Iraq, aitwaye Munir Haddad, ambaye alikuwepo, aliambia televisheni ya CNN wakati huo kwamba mmoja wa watu waliomnyonga Saddam Hussein alimwambia mbele ya uso wake, kuwa yeye ni dikteta aliyeiangamiza Iraq.

Hili mara moja lilizusha mabishano kati ya Saddam na mnyongaji, hadi maafisa wengine waliokuwa chumbani hapo walipoingilia kati.