Iraq miaka 20 baadaye:Jinsi kunyongwa kwa Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein kulivyoshtua ulimwengu mzima

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, By Feras Killani
    • Nafasi, BBC News Arabic, Baghdad

Mto Tigris unapopita katikati ya mji mkuu Baghdad, una siri nyingi. Hakuna anayejua ni miili mingapi imetupwa humo. Miaka 20 baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, bado ni vigumu kukubali jinsi mojawapo ya ustaarabu tajiri zaidi duniani, Babeli ya kale, ilivyoingia katika maafa kama haya.

Leo, licha ya utulivu fulani, Iraq bado inahusishwa na mauaji ya kidini, magari yaliyotegwa mabomu na kuibuka kwa wanamgambo wenye msimamo mkali wa Kisunni na Waislamu wa Shia. Baadhi ya mizizi iko katika miaka ya mapema ya 2000, wakati wa nguvu isiyo na kifani ya Marekani

Uamuzi wa kuvamia

Marekani ilikuwa ikilengwa na kundi la wanamgambo la al-Qaeda katika ardhi yake na mashambulizi ya 9/11. Washington ilipanga muungano wa kuivamia Afghanistan, kituo cha al-Qaeda, mwaka 2001.

'Mafanikio' hapa hivi karibuni yalishuhudia umakini wa Marekani ukirejea Iraq. Massoud Barzani, rais wa zamani wa eneo la Kurdistan la Iraq, anasema yeye na mwanasiasa mpinzani wa Kikurdi, walipokea mwaliko wa kutembelea Washington kwa siri mwezi Aprili 2002.

On 24 September, 2017, Kurdistan President Massoud Barzani speaks to the media at a press conference in Irbil, Iraq

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa zamani wa Kurdistan wa Iraq Massoud Barzani anaelezea uhusiano wake na Marekani uliodumu miongo kadhaa

"Uamuzi ulikuwa umefanywa wa kuupindua utawala wa Saddam iwe tulikubali au la, tulitaka kushiriki au la," anasema.

Barzani alipendekeza kuwa Washington iandae mkutano na kuwaalika viongozi mbalimbali wa upinzani wa Iraq, 'serikali inayoweza kusubiri' ambayo iko tayari kuchukua hatua mara baada ya Saddam Hussein kuondolewa. Ilifanyika London mnamo Desemba 2002 na sura ya serikali ya kidemokrasia ya Iraq ilikubaliwa.

Lakini Barzani anasema kengele za hatari zilikuwa zikilia alipokuwa akishuhudia kile anachokielezea kama "tamaa ya kulipiza kisasi" iliyoonyeshwa na baadhi ya vyama vya Shia. Chini ya Saddam Hussein, idadi kubwa ya Waislamu wa Shia nchini Iraq walikuwa wamekandamizwa kwa nguvu.

Kisha Marekani na Uingereza zilitoa hoja ya vita kwa kuzingatia kuwepo kwa 'silaha za maangamizi makubwa' nchini Iraq, ambazo hazikupatikana kamwe. Operesheni ya kijeshi ilizinduliwa tarehe 19 Machi 2003 kwa mashambulizi makali ya anga ya Baghdad.

Kuanguka kwa utawala wa Saddam

Wiki tatu baadaye, tarehe 9 Aprili, Saddam Hussein alifanya ziara yake ya mwisho katika kitongoji cha Sunni cha Adhamiya huko Baghdad. Vikosi vya Marekani vilikuwa tayari vimeingia mjini na ilikuwa ni saa chache tu hadi walipoiangusha sanamu yake.

Mwandishi wa habari wa Iraq Diyar al-Omari alikuwa Baghdad wakati huo. Anasema Wairaqi waliokusanyika katika uwanja huo hawakuweza kuangusha sanamu hiyo mwanzoni. Hii ilisababisha majeshi ya Marekani kutumia gari la kivita.

US troops enter central Baghdad and topple the statue of Saddam Hussein on 9 April, 2003

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mara baada ya Saddam Hussein kupinduliwa, muundo wa jamii ya Iraqi ulianza kusambaratika
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini msingi wa sanamu na miguu ya Saddam Hussein ilibakia ndani ya ardhi. Ilikuwa ni kionjo cha kile kitakachokuja - utawala wa Saddam Hussein wa Baathi ulikuwa na mizizi mirefu katika jamii ya Iraqi iliyojengwa kwa miongo kadhaa.

Baada ya kuanguka kwa Baghdad, rais wa Iraq na familia yake waliondoka kuelekea jimbo la Anbar. Ali Hatem Suleiman, kiongozi wa Kisuni wa Iraq, anahalalisha hatua ya Saddam Hussein.

"Anbar ni ngome ya Masunni na ngome ya koo za Waarabu huko Iraq na kwa hiyo ilikuwa salama kukimbilia huko.

Muungano wa Marekani uliamua kwenda ‘kuondoa katika jamii ya Iraq na chama cha Saddam Hussein kuondolewa katika siasa na jamii. Uanachama wa chama ulikuwa muhimu kupata aina yoyote ya kazi au elimu nchini Iraq. Uamuzi huu ulipelekea kuporomoka kabisa kwa jeshi la Iraq, usalama na taasisi za kiraia.

"Sehemu ya Sunni ndiyo iliyopoteza zaidi katika mchakato huu. Ilitengwa na jukumu lake kupunguzwa," anasema Ali Hatam Suleiman. "Ilionekana kuunga mkono utawala wa Saddam na hii haikuwa kweli."

Hii ilisababisha maafisa wa zamani wa jeshi na usalama wa Iraq kujiunga na mashirika yenye itikadi kali. Al-Qaeda walipata fursa ya kuinuka tena na kuanzisha uasi ambao ulidumu kwa miaka.

Wakati huo huo, Saddam Hussein alikamatwa na majeshi ya Marekani mwezi Desemba 2003. Miaka mitatu baadaye, alipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu na kuhukumiwa kifo.

Former Iraqi President Saddam Hussein talks to an Iraqi judge during his initial interview at an undisclosed location in Baghdad on 1 July, 2004

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kunyongwa kwa Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein kulileta mshtuko katika eneo zima

Kunyongwa kwake alfajiri ya siku ya Eid al-Adha, sikukuu ya dhabihu na moja ya siku takatifu zaidi katika Uislamu, kulisababisha wimbi la hasira katika majimbo ya Sunni nchini Iraq, na pia katika nchi nyingi za Kiarabu.

Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq, Nouri al-Maliki, ambaye alionekana kuwa karibu na Iran, aliambia BBC News Arabic kwamba alikuwa amedhamiria kuonyesha nguvu zake hata kama ingemaanisha kuwakasirisha Wairaki wenzake.

"Huyu ni kiongozi wa Waarabu wa Sunni (Saddam), vipi kiongozi wa Kishia (Maliki) anaweza kumtawala?" Anasema al-Maliki.

Al-Maliki anasema sababu iliyomfanya kusogea haraka na kunyongwa ilikuwa ni kukwepa jaribio lolote la kupinga uamuzi wa mahakama. Alihofia Saddam Hussein atahamishwa nje ya nchi na hatimaye kuachiliwa. Waziri mkuu huyo wa zamani pia anasema baadhi ya nchi za Kiarabu zilikuwa zikiweka shinikizo kwa mamlaka ya Marekani "kumwokoa Saddam".

Iraqi Prime Minister Nouri al-Maliki speaks during a meeting with the U.S. president at the White House on 1 November, 2013 in Washington, DC

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nouri al-Maliki alikuwa waziri mkuu wa Iraq kuanzia 2006 hadi 2014

Hali ilizidi kuwa ya utata baada ya video ya mauaji hayo kuvuja. Saddam Hussein alionekana mtulivu kwenye video hiyo ambayo ilikinzana na picha iliyochorwa na afisa mkuu wa usalama wa Iraq wakati huo. Alisema Sadam alikuwa akitetemeka huku akipanda kwenye eneo alikonyongwa

Hasira ya WaSunni

Idadi ya vifo ilipoongezeka, hatimaye Marekani ilishawishi koo za Sunni kujiunga na vita dhidi ya al-Qaeda na kundi hilo la wanamgambo kushindwa. Kufikia 2011, vikosi vingi vya Marekani na Uingereza viliondoka Iraq

Lakini chuki ya Wasunni wa mijini dhidi ya sera za Waziri Mkuu al-Maliki ilizua utata tena wakati vijana walipokuwa wakiketi karibu na Fallujah. Kiongozi wa Sunni Ali Hatem Suleiman anaorodhesha malalamiko yao.

"Kulipiza kisasi dhidi ya Sunni, kesi zisizo za haki, na kuingizwa siasa katika sheria na mfumo wa mahakama ya Iraq," anasema.

Al-Maliki anakanusha hili na anasema al-Qaeda ilikuwa imejificha nyuma ya walioketi, ikingoja fursa ya kurejea. Mwishoni mwa 2013, al-Maliki aliamuru jeshi kuvamia viwanja. Hii ilisababisha kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu ndani na nje ya mipaka ya Iraq.

Muslim devotees at Pasa mosque in Mosul during the first day of the holy Islamic fasting month of Ramadan on 23 March, 2023

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mosul ilishambuliwa vikali na vikosi vya Iraq na muungano ili kuwaondoa wanamgambo wa Islamic State

Al-Qaeda walirudi kupitia sura mpya, wakiwa na uwezo mkubwa na ukatili zaidi. Miji mingi iliangukia mikononi mwa kile kilichojulikana kama 'Dola la Kiislamu'.

Jeshi la Iraq lilionekana kutoweka mara moja. "Jeshi lililojengwa katika muda wa miaka 10 liliyeyuka katika muda wa saa 10," anasema Rais wa zamani wa Kikurdi Massoud Barzani.

Waziri Mkuu wa zamani al-Maliki anashangaa jinsi makamanda wa vitengo kamili katika jeshi waliweza kuondoka saa chache kabla ya IS. Haider al-Abadi alimrithi al-Maliki kama waziri mkuu, na anasema wazi kuhusu matatizo.

"Ilikuwa vita vya kidini ambavyo vilikuwa tatizo kubwa," anasema. "IS ni ya kimadhehebu lakini mfumo wa serikali pia umekuwa wa madhehebu."

Hata hivyo, al-Abadi anakataa kuelezea sera za al-Maliki kama za madhehebu, na ana maelezo yake mwenyewe kwa nini baadhi ya miji ya Sunni iliikaribisha IS.

People jump into the Tigris river to cool off during extreme hot weather in Baghdad on 18 June, 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iraq ni chimbuko la ustaarabu lakini watu wake wamevumilia mateso mengi

"Mfumo wa usalama ulikuwa mbovu na uliwapa usalama Wairaki kupitia ulaghai," anasema. "Raia wa Iraq amepoteza imani nao na alikuwa tayari kushirikiana na adui kujilinda."

Juhudi kubwa za usalama na kijeshi za Iraq zilisaidia kushindwa IS baada ya miaka minne. Lakini vita viliacha majeraha makubwa katika majimbo ya Sunni. Hii inaonekana kwa urahisi katika mji wa Mosul, mji muhimu zaidi wa Sunni.

Akiwa na sauti ya uchungu, sheikh katika moja ya misikiti mikongwe zaidi ya Mosul anaomba saa irudishwe nyuma na Iraq itawaliwe na mtu kama Saddam Hussein. Anaomba utambulisho wake ufichwe, kutokana na uzito wa pendekezo lake.

"Hatuna la kusema kuhusu kinachoendelea katika nchi hii," anasema. "Marekani inasema iliikomboa Iraq lakini ilikabidhi nchi hiyo kwa Iran kwenye sinia."

A female labourer covers her face to protect herself from the dust and sun in Baghdad on 7 March, 2023

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iraq ina viwango vya juu vya umaskini ingawa imebarikiwa na rasilimali za mafuta na gesi

Lakini ni nani anayedhibiti ni nini hoja ya kitaaluma wakati wa kujitahidi kuweka chakula mezani. Idadi kubwa ya watu wa Iraq ni vijana na hawana ajira.

Ikiwa Iraq inaweza kuwa nchi ambayo haisumbuliwi na anayeshika hatamu za serikali, fikiria ni nini taifa hili lenye rasilimali nyingi linaweza kuafikia.