Saddam Hussein: Ukatili wa Uday Hussein uliwatisha wengi Iraq hasa alipomuua mjomba wake

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo unataka kujua ukatili nini basi ungekutana na mwanae wa kwanza wa aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein Uday Hussein .
Uday angekuangalia machoni na Iwapo angehisi kwamba umemwangalia kwa jicho baya angeingiza mkono wake mfukoni na kuitoa bastola yake na bila kusita ungekutana na mauti yako.Iwapo ulikua na bahati ,ungekamatwa na kuteswa katika gereza lake la kibinafsi.
Hii ni simulizi ya Uday Hussein na baadhi ya matukio ni kama maigizo ya filamu ila ,yote ni kweli kwa mujibu wa mashahdi wengi pamoja na watu ndani ya utawala wa babake .
Uday Saddam Hussein alikuwa mwanasiasa wa Iraqi na mtoto wa kwanza wa Saddam Hussein. Alishikilia nyadhifa nyingi kama mwenyekiti wa michezo, afisa wa jeshi na mfanyabiashara, na alikuwa mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Iraqi na Chama cha Soka cha Iraq, na mkuu wa Fedayeen Saddam.
Uday Hussein alizaliwa Baghdad na alikuwa mtoto wa kwanza wa rais wa Iraq Saddam Hussein.
Uday alionekana kwa miaka kadhaa kama mrithi wa baba yake lakini alipoteza nafasi hiyo kama mrithi dhahiri kwa mdogo wake, Qusay Hussein, kwa sababu ya majeraha katika jaribio la mauaji. Kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani huko Iraq mnamo 2003, aliuawa pamoja na Qusay na mpwa wake Mustafa na kikosi kazi cha Marekani baada ya mapigano ya muda mrefu huko Mosul.
Uday aliripotiwa kuwa mkatili na mwenye kutisha kwa wapinzani waliotambuliwa na pia marafiki wa karibu. Jamaa , familia na marafiki wa kibinafsi mara nyingi walikuwa wahasiriwa wa ghasia zake na hasira. Madai ya Mashahidi yamesema alikuwa na hatia ya ubakaji, mauaji, na mateso, pamoja na kukamatwa na kuteswa kwa wanariadha wa Olimpiki wa Iraqi na wachezaji wa timu ya kitaifa ya mpira wa miguu kila walipopoteza mechi.
Mnamo 1984, Saddam alimteua mtoto wake Uday kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Iraq na Chama cha Soka cha Iraq. Katika wadhifa wa kwanza aliwatesa wanariadha ambao walikosa kupata ushindi . Latif Yahia, ambaye anadai kuwa alikuwa akitumika kujifanya kuwa Uday Hussein mara mbili, alisema, "Neno linalomfafanua ni la kutisha . Nadhani Saddam Hussein alikuwa utu zaidi ya Uday. Kamati ya Olimpiki haikuwa kituo cha michezo, ilikuwa ulimwengu wa Uday.Raed Ahmed, mmoja wa wanariadha wa Iraqi ambaye alitoroka, alisema, "Wakati wa mazoezi, angewaangalia wanariadha wote kwa karibu, aliwashinikiza makocha kushinikiza wanariadha zaidi ... Ikiwa hakufurahishwa na matokeo, makocha na wanariadha wangewekwa katika gereza lake la kibinafsi katika jengo la Kamati ya Olimpiki.
Adhabu ilikuwa gereza la kibinafsi la Uday ambapo walitesa watu. Wanariadha wengine, pamoja na bora zaidi, walianza kuacha mchezo huo mara tu Uday alipochukua Kamati.
Mauji katika karamu
Ingawa hadhi yake kama mtoto mkubwa wa Saddam Hussein ilimfanya kuwa mrithi anayetarajiwa wa Saddam, Uday hakumfurahisha baba yake. Mnamo Oktoba 1988, kwenye sherehe ya kumheshimu Suzanne Mubarak, mke wa Rais wa Misri Hosni Mubarak, Uday alimuua mhudumu wa kibinafsi wa baba yake na muonjaji wa chakula chake , Kamel Hana Gegeo, labda kwa ombi la mama yake.
Mbele ya wageni waliokuwa na hofu , Uday akiwa mlevi alimchoma Gegeo kwa kisu mara kadhaa . Gegeo alikuwa amemtambulisha Saddam kwa mwanamke mchanga, Samira Shahbandar, ambaye alikuwa mke wa pili wa Saddam mnamo 1986. Uday alizingatia uhusiano wa baba yake na Shahbandar kama tusi kwa mama yake. Mwana wa kwanza wa Shahbandar alikimbilia Jordan kwa sababu ya kusumbuliwa na Uday baada ya ndoa hiyo . Huenda pia aliogopa kupoteza urithi wake kwa Gegeo, ambaye uaminifu wake kwa Saddam Hussein haukuwa na shaka.
Kama adhabu ya mauaji, Saddam alimfunga mtoto wake kwa muda mfupi na kumhukumu kifo; Walakini, labda Uday alitumikia miezi mitatu tu katika gereza katika eneo la kibinafsi.
Mfalme Hussein wa Jordan, aliingilia kati na kumshawishi Saddam kumwachilia Uday, akimfukuza kwenda Uswizi kama msaidizi wa balozi wa Iraq huko. Alifukuzwa na serikali ya Uswisi mnamo 1990 baada ya kukamatwa mara kadhaa kwa kupigana. Kulingana na tovuti ya Jalopnik, magari makubwa na ya kifahari ya Uday Hussein yalichomwa na baba yake baada ya tukio la mauaji ya Kamel Hana Gegeo.
Kumpiga risasi mjomba wake
Mnamo 1995, wakati wa vita kati ya mjomba wake wa upande wa mama Louay na mjomba wa upane wa baba yake Watban, Uday alimpiga risasi mjomba wake mmoja pamoja na kuwafyatulia risasi wageni wengine kwenye sherehe hiyo. Uday kisha alimpeleka mjomba wake Watban hospitalini na kutoweka. Kwa sababu shemeji zake, Hussein Kamel na Saddam Kamel, walitoroka kwenda Jordan siku iliyofuata, shambulio la Uday kwa mjomba wake lilibaki kuwa siri . Saddam aliamuru Uday aulize mjomba wake ampige risasi jinsi Uday alivyompiga risasi, lakini Watban alikataa kufanya hivyo.
Mmoja wa waliojeruhiwa katika sherehe hiyo alisema kuwa sababu ya shambulio hilo ni kwamba mjomba wa Uday alikuwa amefanyia mzaha jinsi Uday alivyopata shida ya kuongea akitoa hotuba yake na mjomba wake mwingine alimuambia Uday kuhusu kejeli hiyo. Tangu kuzaliwa, taya la juu la Uday lilipanukia mbele kwa kiasi kikubwa sana, na kumfanya kupata ugumu wa kuongea vizuri. Katika sherehe hiyo, mjomba wake alikuwa amemuiga yeye kwa kejeli.
Muda mfupi baada ya tukio hilo, Saddam alikasirika alipomwona kaka yake wa kambo hospitalini ana shida ya kutembea, na akaamuru magari ya kifahari ya Uday yachomwe moto. Uday alikasirika na kaka yake Qusay kwa kutomzuia Saddam na akapatwa na mshtuko wa neva.
Qusay alisema alimzuia kuchoma karakana nyingine. Uday aliweka kizuizi mbele ya magari yake ya kifahari katika karakana nyingine ya karibu, akajihami kwa silaha, na kusubiri baba yake au watu wake waje. Kulingana na rafiki yake wa karibu Jaber, Uday angemuua baba yake iwpo angekuja kwenye karakana ya pili.
'Kufuatia hatua ya Uday kumpiga risasi [mjomba wake] Watban, Saddam alijaribu kuchukua na kulipua magari ya Udayy katika karakana moja. Lakini karakana hiyo ilikuwa na magari kumi na tatu tu. Saddam hakujua kuwa Udayy ana gereji zingine kadhaa; Ninajua angalau sita zaidi'
Jaribio la mauaji
Hussein alipata majeraha ya kudumu wakati wa jaribio la mauaji jioni ya tarehe 12 Desemba 1996.Alipigwa na kati ya risasi 7 hadi 17 wakati akiendesha gari huko Al-Mansour (Baghdad), `Hussein mwanzoni aliaminika kuwa amepooza. Alipohamishwa kwenda Hospitali ya Ibn Sina, mwishowe alipona lakini alichechechemea kwa njia ghahiri iliyomfanya kuonekana kilem a. Licha ya operesheni za mara kwa mara, risasi mbili zilibaki kwenye mgongo wake na hazingeweza kutolewa kwa sababu ya mahali zilipo.Kutokana na ulemavu uliofuata wa Uday, Saddam alimpa Qusay uwajibikaji na mamlaka, akimteua kama mrithi wake mwaka 2000
Mauaji ya wanawe Saddam - Uday na Qusay
Msaidizi wa karibu zaidi wa Saddam Hussein na katibu wa kibinafsi, Abid Hamid Mahmud, alikuwa amekamatwa, na kuwaambia waliomuhoji kuwa yeye na wanawe wawili wa Saddam walikuwa wamekimbilia Syria lakini wakarudishwa.
Asubuhi ya Jumanne Julai 22, 2003, Kikosi Kazi cha JSOC 20, kikisaidiwa na wanajeshi wa Jeshi la Marekani na Idara ya Usafiri wa Anga, walimzingira Uday, Qusay, na mtoto wa Qusay wa miaka 14 Mustafa wakati wa uvamizi wa nyumba moja Kaskazini mwa Iraqi. Katika mji wa Mosul. Uday alikuwa kipau mbele kwa waliofaa kukamatwa kwa mujibu wa kadi za karata zilizokabdhia wanawajeshi wa Mrekani .
Wakitumia habari kutoka kwa al-Zaidan, wanajeshi kutoka Idara ya 101 ya Hewa walitoa usalama wakati Kikosi Kazi cha 20 kilipojaribu kuwakamata waliokuwa katika nyumba hiyo. Wanajeshi 200 wa Marekani baadaye wakisaidiwa na helikopta za OH-58 za Kiowa, walizunguka na kufyatulia risasi nyumba hiyo, na hivyo kumuua Uday, Qusay, na mtoto wa Qusay. Baada ya takriban masaa manne ya vita, askari waliingia ndani ya nyumba na kupata miili minne, pamoja na walinzi wa ndugu wa Hussein.
Askari, ambao walijaribu kuingia ndani ya nyumba hiyo mara tatu, walipata upinzani wa mashambulizi ya bunduki za AK-47 na mabomu katika majaribio mawili ya kwanza. Uday, Qusay na mlinzi walichukua nafasi katika bafu mbele ya jengo, ambapo walikuwa na uwezo wa kufyatua risasi barabarani na kwa ngazi zinazoelekea ghorofa ya kwanza; Mtoto wa Qusay alijificha kutoka chumba cha kulala nyuma ili kujikinga . Vikosi vya Marekani kisha viliishambulia nyumba hiyo kwa mabomu mara nyingi na kurusha makombora.














