Wairaqi wengi wanasema nchi ilikuwa bora chini ya Saddam Hussein - utafiti

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Julien Hajj
- Nafasi, BBC Arabic
Wairaqi wengi wanasema hali ya nchi imekuwa mbaya zaidi tangu uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2003, kulingana na utafiti mpya.
Haya yanajiri wakati nchi hiyo ya Mashariki ya Kati yenye utajiri mkubwa wa mafuta ikiadhimisha miaka 20 ya kuondolewa madarakani kwa Rais Saddam Hussein.
Gallup International, shirika lisilo la faida la kimataifa la kura za maini lilifanya uchunguzi wa ana kwa ana katika majimbo yote 18 ya Iraq, kati ya sampuli wakilishi ya kitaifa ya watu wazima 2,024 mnamo Februari 2023.
Walipoulizwa kuhusu hali ya sasa ya Iraq ikilinganishwa na kabla ya uvamizi wa Marekani, 60% ya waliohojiwa walisema imekuwa mbaya zaidi, huku 40% walisema imeimarika.
Waarabu wengi wa Shia wa Iraq walipata nguvu kisiasa baada ya 2003, na kusababisha chuki miongoni mwa Waarabu wa Sunni wa Iraq, Wakurdi na jumuiya nyingine ndogo ndogo.
Na mgawanyiko huu wa kimadhehebu unaonekana katika uchunguzi huku wengi wa Waislamu wa Sunni, baadhi ya 54%, wakiamini maisha yalikuwa bora chini ya Saddam Hussein.

Licha ya tathmini hii mbaya, kuna dalili za maendeleo. Mmoja tu kati ya watatu kati ya waliohojiwa wanaelezea hali ya Iraq kama "maskini" leo.
Wakati Gallup International ilipoingia kwenye makavazi yake na kutafuta jibu la swali kama hilo mwaka 2003, iligundua kuwa karibu Wairaqi wawili kati ya watatu walisema hivyo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mwanamume mwenye umri wa miaka 45 anayeishi katika jimbo la Anbar aliiambia timu ya uchunguzi: "Ni vigumu kubainisha ikiwa hali imeboreka au kuwa mbaya zaidi. Mabadiliko yanaleta matumaini na tunaelekea kusahau yaliyopita. Uchumi unaweza kuwa umeimarika lakini uzalishaji na usalama umedorora’
Marekani iliivamia Iraq mwaka 2003 ikiamini kuwa nchi hiyo ina 'silaha za maangamizi' (WMDs) na kwamba utawala wa Saddam Hussein ulikuwa tishio kwa usalama wa dunia.
Lakini hakuna ushahidi wa WMDs uliowahi kupatikana. Badala yake, vita hivyo vilisababisha mamia ya maelfu ya vifo vya Wairaki na ukosefu wa utulivu wa kudumu nchini humo.
Licha ya uhalali wa vita uliotolewa na serikali ya Marekani, inaonekana Wairaki wengi wanabakia kuwa na mashaka kuhusu nia ya kweli ya kwenda vitani.
Asilimia 51 ya Wairaki wanaamini kuwa Marekani iliivamia Iraq ili kuiba rasilimali zake.
Maoni haya yana nguvu zaidi katika majimbo ya kusini-mashariki na jimbo la Anbar, ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.

Wakati huo huo, asilimia 29 ya waliohojiwa wanaamini kuwa lengo la uvamizi huo lilikuwa kuuangusha utawala wa Saddam Hussein. Sababu nyingine, kama vile kutumikia maslahi ya wanakandarasi wa ulinzi wa Marekani, kupambana na ugaidi na kuleta demokrasia nchini Iraq, zilikuwa chaguo zisizo maarufu.
Wakati uvamizi ulioongozwa na Marekani ulipozuka, wanamgambo wa madhehebu waliingia mitaani. Jirani Iran pia iliona njia ya kuingia nchini humo hasa kwa vile 60% ya wakazi wa Iraq ni Waislamu wa Shia, waliokandamizwa kwa muda mrefu chini ya Saddam Hussein.
Kutokana na kuongezeka kwa Islamic State ambao walipata uungwaji mkono miongoni mwa Wasunni waliokataliwa kaskazini, mapambano mapya kwa ajili ya nafsi ya Iraq yalianza mwaka wa 2014. Baghdad ilipata usaidizi mkubwa wa kijeshi wa Marekani na washirika wake na IS mwaka wa 2018. Tangu wakati huo, hali kama hiyo ilionekana utulivu umerejea.
Wairaqi wamegawanyika juu ya mustakabali wa ushiriki wa Marekani katika nchi yao, kulingana na utafiti huo. Idadi ya wanajeshi wa Marekani ilifikia karibu 170,000 katika kilele cha ongezeko hilo mwaka 2007 na kusimama hadi takriban wanajeshi 2,500 leo.
Wahojiwa wanaoishi katika sehemu ya kusini mwa Iraq wanapendelea Marekani kujiondoa mara moja huku wale wa sehemu ya kaskazini, ikiwa ni pamoja na eneo la Kurdistan nchini Iraq, wanaamini kwamba kiwango fulani cha uwepo wa Marekani ni muhimu.

Asilimia 75 ya Mashia wa Iraq waliohojiwa wanaona kuwasili kwa vikosi vya muungano vya Marekani kuwa mbaya. Wanaweka uungwaji mkono wao nchini Urusi kama mshirika wa kisiasa na usalama. Kwa kuzingatia uhusiano wa karibu kati ya Tehran na Moscow, hii sio jambo la kushangaza katika eneo lenye hali tete.

Kiuchumi, China imechukua nafasi ya juu zaidi katika Mashariki ya Kati katika miaka ya hivi karibuni ingawa eneo hilo limeanguka chini ya mwavuli wa usalama wa Marekani. Hivi majuzi Beijing ilitangaza 'upatanishi' kati ya Iran na Saudi Arabia ambapo walikubali kurejesha uhusiano wa kidiplomasia.

Lakini mustakabali wa vijana ni mbaya -- umeangaziwa na vuguvugu la kijamii la Tishreen ambalo lilianza katika mitaa ya Baghdad mnamo 2019 na lilikandamizwa kikatili.
Wakati 47% ya Wairaqi waliohojiwa wanataka kubaki na kujenga nchi mpya, 25% au mmoja kati ya wanne wa waliohojiwa wanataka kuondoka.
Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa aliuambia uchunguzi huo: "Idadi inayoongezeka ya vijana wa Iraq, hasa wanaume wanaoishi Baghdad, wanaona mustakabali mwema kwao wenyewe nje ya nchi."
Na unapoivunja kwa umri, inasimulia hadithi yake mwenyewe. Takriban mmoja kati ya Wairaki watatu wenye umri wa miaka 18-24 wanataka kuondoka – Matokeo makubwa ya tabaka la kisiasa nchini humo na matatizo ya muda mrefu ya rushwa.

Lakini utata wa Iraq hauwezi kupunguzwa kwa takwimu. Kwa mamilioni ya Wairaki, miongo miwili iliyopita imekuwa na kiwewe na machafuko.
Bado kizazi kipya kinaibuka, kikirithi mzigo wa zamani huku kikijitahidi kutengeneza mustakabali bora.
Kukiwa na angalau 40% ya wakazi wa Iraq chini ya umri wa miaka 15, kizazi hiki cha vijana kinaonekana kupendelea usalama wa kiuchumi na fursa za kazi, wakati pia wanatamani amani na utulivu.
Inatarajiwa viongozi wa Iraq na waungaji mkono wa kimataifa watakabiliana na changamoto hiyo.
Upeo wa makosa ni +/- 2.2%.Utafiti ulitumia hati ambayo ilibagua uteuzi wa waliohojiwa na kujumuisha ukaguzi mtambuka wa majibu ya maswali nyeti. Zaidi ya 50% ya wafanyikazi wa nyanjani walikuwa wanawake na wanawake waliohojiwa.
Uandishi Takwimu: Leoni Robertson
Miundo na Vielelezo: Raees Hussain and Ismail Moneer
Wahariri: Maya Moussawi and Johannes Dell















