Uday Hussein: Simulizi ya Kikatili ya Mtoto 'Mbakaji' wa Saddam Hussein aliyefanya Iraq itetemeke

Chanzo cha picha, Getty Images
Aliitwa 'Lal no Ekko' kutokana na hasira zake za papo kwa papo, tamaa, ukatili, ujeuri na pia na kejeli.
Baba yake alikuwa ameoa mwanamke mwingine. Mwanamke huyo alikuwa anafahamiana na mtumishi wake na alipata taarifa kwamba mtumishi huyo ndiye aliyehusika na ndoa ya pili ya baba yake. Hivyo alimuua mfanyakazi huyo kwa kumpiga na fimbo katikati ya watu 50-100 kwenye tafrija iliyofanyika nyumbani kwake.
Jina la mtu aliyekufa aliitwa Kemal na jina la mtu aliyemuua Kemal ni Uday Hussein, mtoto wa Saddam Hussein.
Kuna wakati Iraq ilishambulia Kuwait. Iraq imekuwa ikipigana na Iran kwa miaka minane. Jeshi lilikuwa limechoka. Vita moja baada ya nyingine, watu waliteswa. Walihitaji kiongozi mkuu.
Kiongozi huyo hakuwa mwingine bali ni Uday Hussain. Wakati mtoto wa Saddam Hussein alipojitokeza, jeshi lilikasirika. Jeshi lilijua kiongozi wake ni nani, lakini ni mtu mmoja tu aliyejua ukweli na huyo alikuwa Latif Yahya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Yote yalianza mwaka wa 1987. Wakati huo, Latif Yahya mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akifanya mazoezi ya kuwa afisa katika jeshi la Iraq. Jenerali akamwita wakutane mara moja. Latif alipoenda ofisini kwa Jenerali, Jenerali akamuuliza, "Je, alichukua uamuzi wowote?"
Latif alisema, "Hapana. sijui chochote."
Jenerali akasema, “Barua imekuja kwa jina lako. Umeitwa kwenda Ikulu huko Baghdad."
Latif aliandika katika wasifu wake kwamba “Nilishtuka. Nilijiunga na jeshi bila kupenda.
Alifika Ikulu ambapo Saddam Hussein na Uday walikuwa wakiishi. Alikuwa amefanana na mtoto huyu wa rais, Uday na walipokutana Ikulu, Uday alimshika bega kwa nyuma na kumuuliza "Ungependa kuwa mtoto wa Saddam?"
Miaka mingi baadaye Latif aliandika kitabu cha wasifu wake. kilichoitwa: I Was Saddam's Son kwa tafrisi isiyo rasmi kwamba 'Nilikuwa mtoto wa Saddam'.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Viongozi wengi duniani, wakiwemo marais wanakuwa na mtu anayefanana nao kabisa kama 'pacha' ambaye anatumika kwenda kwenye mikutano na shughuli zingine akidhaniwa kuwa ni kiongozi kumbe ni mtu tofauti na atapewa heshima zote lakini ukweli sio.
Na hii hufanyika kwa sababu za kiusalama. Kulikuwa na Hitler wawili, yule halisi na Hitler 'feki' aliyekuwa anitwa Himmler. Uday alimtaka Latif kuwa 'pacha' wake ili awe anajifanya Uday kwenye shughuli mbalimbali.
"Nilijua jinsi ilivyo hatari. Pia nilijua ni nini kingetokea ikiwa Uday atakasirikaa. Nikamuuliza, naruhusiwa kukataa? akajibu Uday kwa kusema "bila shaka, kila mtu yuko huru kufanya maamuzi hapa,” Uday alisema huku akitabasamu.
Latif akakataa kuwa Uday. Kilichomkuta akajikuta yuko kwenye chumba chenye giza ameswekwa huko. Siku ya saba, Uday akaja na kuniuliza, 'Ikiwa hutakubali ofa yangu, nitamleta dada yako hapa pia. 'Kwa maneno rahisi ilikuwa ni tishio kwamba kama ningekataa ofa yake, angemchukua dada yangu na kumleta hapa na kumbaka. Nilikubali ofa yake. Sikuwa na chaguo ila kufanya hivyo."
Chumba cha Ubakaji Iraq
Wakati Marekani ilipoivamia Iraq, Rais wa Marekani wakati huo George Bush alisema, "Watu wa Iraq hawahitaji tena kuogopa kambi za mateso na vyumba vya ubakaji."
Marekani ilidai kuwa wakati wa utawala wa Saddam Hussein nchini Iraq, watu wa kawaida walitolewa mitaani na ama kuteswa au kubakwa. Kulikuwa na vyumba maalum vya kubaka wanawake.
Chumba kama hicho kilikuwa katika kasri ya Uday Hussain, Latif alikiambia kipindi cha Hard Talk cha BBC, na kuongeza, "Uday alikuwa mtu mkatili. Aliwahi kumpeleka msichana mrembo kwenye chumba cha ubakaji nikishuhudia na kumpiga hadi kumuua.”
Kulingana na kitabu cha Latif, msichana huyo baadaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kufungwa kwenye zulia na kutupwa baharini.
Binadamu aliyechukiwa zaidi Iraq

Chanzo cha picha, Getty Images
Uday Saddam Hussein aliwahi kuchukuliwa kama mtu anayechukiwa zaidi nchini Iraq. Uday alikuwa mtoto mkubwa wa kiume na alitarajiwa kurithi mamlaka yote baada ya Saddam Hussein, lakini tabia ya Uday haikupendwa na Saddam Hussein pia.
Uday aliteuliwa kushika nyadhifa nyingi muhimu. Alikuwa rais wa Kamati ya Olimpiki ya Iraq. Alikuwa mkuu wa vyombo vya habari Iraq (Magazeti na TV). Alikuwa kiongozi wa Umoja wa Waandishi wa Habari wa Iraq na pia alikuwa mkuu wa kikosi cha 'mauaji' cha Saddam Hussein.
Uday Hussain pia alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Iraq. Alikuwa akimpigia simu mchezaji yoyote wakati wa mechi iliyokuwa ikiendelea na kumtishia kwamba 'tukifungwa nitakuvunja miguu.'
Alikuwa na kadi maalumu ya unyanyasaji kwa wachezaji. Mfano wakipoteza mechi, maelezo ya mchezaji gani wa kuadhibiwa, aliyesababisha kufungwa yaliandikwa kwenye kadi.
Kuichezea Iraq ilikuwa kama kuishi kwenye shimo la ugaidi kila mara. Ikiwa mchezaji hakucheza vizuri, Uday angemtesa kwa shoti za umeme au kuoga maji yenye madini yasiyofaa. Baadhi ya wachezaji walihukumiwa kifo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baba yake Rais Saddam Hussein alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke fulani kwa miaka mingi. Mwanamke huyo aitwaye Samira Shahbandar baadaye akawa mke wake wa pili.
Uday alihisi kuwa ndoa ya pili ya Saddam Hussein ilikuwa ni dharau kwa mama yake mzazi, Sajida. Wengine hata wanasema kwamba Udaya alishuku kwamba ikiwa Samira angezaa mtoto wa kiume, angerithi madaraka. Akiwa amekasirishwa na hilo, Uday alimpiga rafiki yake Saddam aliyemwamini sana aliyeitwa Kemal Hana hadi kufa kwa fimbo mbele ya umati wa watu kwenye tafrija aliyoandaa.
Uday alishuku kwamba Kemal alikuwa amepanga Saddam na Sameera wakutane na alikuwa ameficha habari za ndoa ya pili ya Saddam dhidi ya familia yake. Baada ya tukio hilo, Saddam alimfunga Uday kwa muda na baadaye kumpeleka Uswizi.
Kwa mujibu wa Latif, alitembelea jeshi mara kadhaa na kufanya mikutano na viongozi wa jeshi kama Uday, ingawa Uday halisi alikuwa Uswizi.
Uday Hussain anayeonekana kwenye picha akiwa na jeshi wakati wa Vita vya kwanza vya Ghuba sio wa kweli, kama Uday halisi alikuwa Uswizi wakati huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Walisoma pamoja
Latif na Uday walisoma shule moja. Kwa hiyo Uday alimjua vyema Latif Yahya na alikuwa anajua anafanana naye sana. Baada ya Latif kukubali kuwa 'Uday bandia', Latif alifanyiwa upasuaji wa plastiki. Kurewkebisha menona muonekano kidogo urandane kwa asilimia mia na Uday halisi.
Mnamo 1996, Uday alishambuliwa vibaya. Wauaji walilimiminia risasi gari lake. Risasi zilimpiga Uday kwenye uti wa mgongo, lakini akanusurika. Hakuweza kamwe kutembea vizuri baada ya hapo. Daima alihitaji fimbo kwa msaada.
Kutokana na tabia ya Uday, Saddam alianza kumuondoa kwenye nyadhifa mbalimbali. Baada ya shambulio dhidi ya Uday, mdogo wake akawa mtu wa pili mwenye nguvu nchini Iraq baada ya Saddam. Jina lake lilikuwa Kosai Hussein.
Watu wengi wanamwelezea mtoto mdogo wa Saddam Hussein kuwa mtulivu, mwerevu na mjanja.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kujifanya Uday kuliniathiri pia
Latif alikuwa Uday Hussain feki kwa takriban miaka minne. Kulingana naye, alitoroka Iraq mnamo 1991 kwa msaada wa CIA.
Katika kipindi cha BBC, Uday alisema, “Kujifanya Uday, kulifanya nifanane naye. Nilikuwa na hasira, wakati mwingine niliwapiga watu."
“Niliona unyama mwingi katika kipindi hicho hadi nikalazimika kutafuta msaada wa madaktari wengi wa magonjwa ya akili ili niishi maisha ya kawaida baada ya kutoroka Iraq. Nilijaribu kujiua mara kadhaa. Tazama, nilikata mshipa wa mkono wangu mara kadhaa,” alisema Latif akionyesha mkono wake.
Kwa hisia za Latif kuhusu Uday Hussain, ni kwamba, Saddam Hussein hakujua lolote kuhusu tabia ya Uday.












